David Silinde: Tukishindwa kuwatoa CCM kwa kura tutawatoa kwa nguvu

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Mbunge wa Mbozi Magharibi,David Silinde ametamka bungeni leo kuwa iwapo tutashindwa kuwatoa CCM madarakani kwa kura basi tutawatoa kwa nguvu "tukishindwa kuwatoa kwa kura,tutawatoa kwa nguvu",alisema mh.Silinde.

Mh. huyo amesema hayo wakati akichangia taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti ,taarifa ya kamati ya bunge ya LAC na taarifa ya kamati ya PAC.

Katika hatua nyingine, mh.Silinde ametoa kali kwa kusema bungeni kuwa iwapo mafisadi wote watakamatwa basi vikao vya CCM havitafanyika kwa kukosa akidi.

Hii ni baada ya taarifa ya ufisadi uliokithiri katika halmashauri na maeneo mengine nchini kuwekwa wazi katika taarifa za kamati hizo bungeni.

MY TAKE:
Nasubiri kusikia wabunge wa CCM wakiomba muongozo kwa spika juu ya kauli hii ingawa binafsi naunga mkono kauli hiyo ya mh.Silinde.
 
Anaota huyo. Watanzania hatutaki fujo. Angalieni tu jirani zetu mjue kuwa vita si lele mama. Atawatoa kwa fujo! Yaani aanzishe vita? Ashindwe kabisa!!![
 
Mbunge wa Mbozi Magharibi,David Silinde ametamka bungeni leo kuwa iwapo tutashindwa kuwatoa CCM madarakani kwa kura basi tutawatoa kwa nguvu "tukishindwa kuwatoa kwa kura,tutawatoa kwa nguvu",alisema mh.Silinde.Mh. huyo amesema hayo wakati akichangia taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti na taarifa ya kamati ya bunge ya LAC na taarifa ya kamati ya PAC.

Ili CCM iweze kutoka madarakani,ni lazima haya yafuatayo yatokee
1.Ni lazima kuwe na mgogoro mkubwa ndani ya CCM na mgogoro huo usababishe CCM kufunjika vipande vipande.hii itasababisha baadhi ya wananchama kuhama chama na kujiunga ama kuanzisha vyama vingine.
kama hii kitu haiwezi kutokea CCM haiwezi kutoka madarakani.
2.Vijana waamue kuwa ni wapiga kura wa kweli,lakini kama itaendelea kama miaka yote itakuwa ni ngumu sana CCM kutoka.
3.Vyama vipanzani viungane na kusimamisha mgombea mmoja wa urais,hii inaweza kuunganisha kura chache toka kwa kila chama na kusababisha upungufu wa kura kwa CCM
4.ccm isimamishe mgombea wa urais asiyekubalika na wala kuwa na mvuto kwa wananchi,hapo lolote laweza tokea
zaidi ya hapo bado ipo safari ndefu ya kuitoa CCM madarakani,
inaweza poteza viti vingi vya ubunge na udiwani,lakini haiwezi kupoteza nafasi ya urais.
Kuhusu kutumia nguvu ni lazima wananchi waridhie,kwa jinsi watanzania tulivyo watu wa amani,itakuwa ngumu sana kuitoa CCM kwa nguvu,la sivyo njia nyingine zitumike,jambo ambalo kwa Tanzania hatutaweza kuruhusu hali hiyo itokee.
 
Japo sijamsikia kwa masikio yangu lakini kama kweli kasema basi amekosea sana. Ni watanzania pekee na kwa kupitia sanduku la kura wenye uwezo wa kuiondoa CCM madarakani. Hata hizo nguvu anazosema Mh Mbunge wataitumia siamini kama wanayo.
 
Anaota huyo. Watanzania hatutaki fujo. Angalieni tu jirani zetu mjue kuwa vita si lele mama. Atawatoa kwa fujo! Yaani aanzishe vita? Ashindwe kabisa!!![
sema mtanzania mm sitaki fujo kwani mm pia ni mtanzania na ikishindikana kwa box basi kwanguvu ccm watatoka
 
Anaota huyo. Watanzania hatutaki fujo. Angalieni tu jirani zetu mjue kuwa vita si lele mama. Atawatoa kwa fujo! Yaani aanzishe vita? Ashindwe kabisa!!![

By Lema

"Bora vita kuliko amani inayopumbaza"
 
Jamaa hakukosea, CCM ni mabigwa yaani majizi ya kura, na wakishindwa wana lazimisha mfano uliyo wazi kabisa ni uchaguzi uliyo famyika segerea... sasa sitegemei hata siku moja serikali hii itakubali kutoka madalakani kwa kuingiza kipande cha karatasi kwenye kiboksi cha kura, CUf wameshind amara ngapi zanzibar, lakini matokeo yanaonekana,,, hawa jama wanatumia uoga wetu kuendelea kututawala kizushi... jama hakukose kabisa
 
Na kama huu ndiyo utakuwa msimamo kwa 2015, basi jamaa wata achia ngazi mapema, maana hakuna asiye ogopa kifo! lakini hii ya kujifanya demokrasia ya kupelekwa kama wajinga haitasaidia kitu. ili mradi kuwe na ukweli katika matokeo ya upigaji kura...yaanikama walicho mfanyia bagbo ndiyo jibi la haya magamba
 
Mbunge wa Mbozi Magharibi,David Silinde ametamka bungeni leo kuwa iwapo tutashindwa kuwatoa CCM madarakani kwa kura basi tutawatoa kwa nguvu "tukishindwa kuwatoa kwa kura,tutawatoa kwa nguvu",alisema mh.Silinde.Mh. huyo amesema hayo wakati akichangia taarifa ya kamati ya bunge ya bajeti na taarifa ya kamati ya bunge ya LAC na taarifa ya kamati ya PAC.

Hii ni baada ya taarifa ya ufisadi uliokithiri katika halmashauri na maeneo mengine nchini kuwekwa wazi katika taarifa za kamati hizo bungeni.

MY TAKE:
Nasubiri kusikia wabunge wa CCM wakiomba muongozo kwa spika juu ya kauli hii ingawa binafsi naunga mkono kauli hiyo ya mh.Silinde.
Ni aibu kubwa sana kama mbunge kijana hafundishwi na chama chake siasa za ushindani,mshindi kwenye siasa ni mwenye kura nyingi....hili nalo ni tatizo la CDM kufundishwa kumchukia mpinzani, yaonekana dogo sasa akiambiwa kwamba 2015 kwenye jimbo lake kuna mtu mwingine wa CDM anatangaza nia atamjengea uadui kwamba ni mhaini/msaliti nk sasa naanza kuamini kwamba wabunge wa CDM wanafanya kazi kama genge la wahuni...ngumi mkononi rejea sugu,mbowe bunge lililopita.......nahisi bwana mdogo hajui kwamba siasa ni upepo, saa yoyote wananchi walewale waliokubeba wanakugeuka............Ni ngumu sana CCM kushindwa na upinzani hivi karibuni, kwa sababu mara kwa mara kwenye JF wafuasi wa CDM wamekuwa wakilinganisha wanaCCM mbalimbali wanaofaa kupewa bendera ya Chama 2015 mara utasilkia Lowasa,Membe,Nchimbi,Makamba nk..........sisi tunakusanya maoni ili tupeleke DODOMA ili nchi yetu ipate Raisi Bora kutoka CCM kama kawaida
 
Nilikuwa sijawahi msikia akichangia, jamaa yuko vizuri kwa mpangilio wa hoja, hana jazba anafanana na Mnyika katika kujenga hoja.
 
Ili CCM iweze kutoka madarakani,ni lazima haya yafuatayo yatokee
1.Ni lazima kuwe na mgogoro mkubwa ndani ya CCM na mgogoro huo usababishe CCM kufunjika vipande vipande.hii itasababisha baadhi ya wananchama kuhama chama na kujiunga ama kuanzisha vyama vingine.
kama hii kitu haiwezi kutokea CCM haiwezi kutoka madarakani.
2.Vijana waamue kuwa ni wapiga kura wa kweli,lakini kama itaendelea kama miaka yote itakuwa ni ngumu sana CCM kutoka.
3.Vyama vipanzani viungane na kusimamisha mgombea mmoja wa urais,hii inaweza kuunganisha kura chache toka kwa kila chama na kusababisha upungufu wa kura kwa CCM
4.ccm isimamishe mgombea wa urais asiyekubalika na wala kuwa na mvuto kwa wananchi,hapo lolote laweza tokea
zaidi ya hapo bado ipo safari ndefu ya kuitoa CCM madarakani,
inaweza poteza viti vingi vya ubunge na udiwani,lakini haiwezi kupoteza nafasi ya urais.
Kuhusu kutumia nguvu ni lazima wananchi waridhie,kwa jinsi watanzania tulivyo watu wa amani,itakuwa ngumu sana kuitoa CCM kwa nguvu,la sivyo njia nyingine zitumike,jambo ambalo kwa Tanzania hatutaweza kuruhusu hali hiyo itokee.

Ccm atasimama mh Makamba jr, iko vipi hiyo mkuu?
 
hahahahaha
swali zuri sana mkuu,nadhani unaelewa kuwa,kila mwanachama wa CCM ni ruksa kugombea nafasi ya kukiwakilisha chama ktk kupeperusha bendera ya chama kwenye nafasi ya Urais.swala la kupewa nafasi ama la litategemea na wapiga kura ndani ya CCM.lakini mpaka sasa kijana nafasi yake bado ni ndogo sana.
 
iwapo tutashindwa kuwatoa CCM madarakani kwa kura basi tutawatoa kwa nguvu "tukishindwa kuwatoa kwa kura,tutawatoa kwa nguvu",alisema mh.Silinde.

Inaonekana huu ni msimamo wa CHADEMA, maana hata LEMA amekuwa akitamka maneno haya kwa kuyarudia rudia mara kwa mara. Ila haipendezi Msomi kama Silinde kuzungumza hivi. Bora angewaachia LEMA au SUGU waongee.
 
Kumbe maneno ya huyu mpuuzi silinde, ccm ndio chaguo la walio wengi, huo udicteta upo chadema. Asitake kuiingiza nchi katk machafuko
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom