Mbonea
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 20
Wadau,
Najua mtakuwa mnamkumbuka sana huyu "mheshimiwa" kwa style aliyokuja nayo ya kupiga ufito wa rangi tofauti tofauti kwa kila daladala za jijini ili iwe rahisi kwa abiria kutambua gari husika linapoishia kitu ambacho mikoa mingine ilikuja ikaiga. Pongezi zake!
Lakini ilikuaje akapoteza nafasi yake na kupewa mtu mwengine?
Na je, mchango wake haukuwa "effective" to the extend of being withdrawn?
Where his he right now?
Mchango wa huyu Ndugu ni mkubwa kweli hasa kwa abiria tunaotumia usafiri wa daladala kwenda hapa na pale.
Utaratibu ulioanzishwa chini yake wa daladala kuandikwa njia unatusaidia sana hivi sasa na kutupunguzia gharama. Sipati picha ningekuwa natumia kiasi gani kwa siku kutoka na kurudi Kimara ninapojibanza. Sasa hivi hata konda akiitia mwisho Ubungo napanda tu ili mradi ni Kimara
Sijui yuko wapi, lakini mchango wake binafsi ninauthamini sana. Mwenyezi amjalie popote alipo Mheshimiwa sana David Mwaibula
====Huyu Mwaibula alifanya kazi ya kusimamia na kubuni njia mbalimbali ili kupunguza foreni na kutumia gharama ndogo kusafiri.Mfano alibuni njia ndefu kama kutoka G'lamboto Ubungo,Mbagala mwenge,n.k.Alikuwa na mikakati mingi mizuri.Je jembe hili limetupwa wapi na mpini wake?
UNAMFAHAMU ALIYEBUNI MISTARI YA DALADALA DAR ES SALAAM?
Mabasi ya usafiri wa abiria Jijini Dar es Salaam yametofautishwa kwa rangi kulingana na barabara yanazopipa mabasi hayo sambamba na maeneo yanakotoka.
Mfumo huu umekuwa msaada mkubwa kwa abiria kwa kuweza kuwarahisishia kufahamu kwa haraka barabara ambayo gari inapita hivyo kuondoa sintofahamu juu ya kule wanakoelekea.
Licha ya hilo, mfumo huu umelisaidia Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama Barabarani kuweza kuwadhibiti madereva wanaoiba ama kukatisha ruti.
Kama msafiri ni mgeni na anataka kwenda Temeke au Tandika basi daladala zenye mstari wa kijani ndizo atakazopanda.
Kwa abiria anayeelekea Banana, Kitunda na Gongolamboto daladala zenye mstari wa rangi ya chungwa linaloiva ndiyo anazopaswa kupanda.
Halikadhalika yule wa kuelekea Mbagala, Temeke au Mbande kupitia Kilwa Road basi daladala zenye mstari wa rangi ya jani kavu ndizo atakazopanda.
Kwa wale wanaopita Morogoro Road kuelekea Ubungo, Kimara hadi Kibamba gari zenye mstari mwekundu ndizo zenyewe hasa kupanda.
Kuna mistari mingi sana na tofauti ambayo kwa hakika kama tutaendelea kuielezea hapa hatutamaliza kuichambua.
Swali la kujiuliza hapa ni;
NANI ALIYEBUNI RANGI HIZI ZA DALADALA?
Mzee David Mwaibula almaarufu "Makofia" aliyekuwa Mwenyekiti wa Mamlaka ya Leseni za Usafiri Dar es Salaam (DTLA) ndiye mbunifu na muasisi wa mfumo huu wa kupaka daladala mistari.
Ubunifu wa Mzee David Mwaibula uliigwa hata na Mamlaka zingine za Miji na Majiji Tanzania Bara.
Mara ya mwisho kuonekana hadharani Mzee David Mwaibula ilikuwa mwaka 2016 kipindi ambapo Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipotembelea mradi wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART).
Hakika Mzee wetu David Mwaibula anastahili pongezi za dhati kwa ubunifu huu ambao umeweza pia kuzinufaisha Mamlaka kama VETA.
Tuwaenzi Wazee wetu.
Last edited by a moderator: