Elius W Ndabila
JF-Expert Member
- Jul 17, 2019
- 322
- 645
TUSIHOFU, HII NDO VITA YA KIUCHUMI
Na Elius Ndabila
0768239284
Jana kumezuka mtifuano mkali kwenye mitandao ya kijamii baada ya kile kilichoelezwa kuwa ni maazimio ya bunge la EU kwa Tanzania. Lakini baada ya ufafanuzi wa Balozi wa Tanzania juu ya wapotoshaji hali imetengamaa. Lakini pamoja na utengamano huo inaonyesha sura ya kesho ya Tanzania namna tunavyopaswa kujidhatiti kujitegemea.
Sitaki kuzungumzia sana hilo, lakini ninataka kumzungumzia David James McAllister aliyepata air time sana na vijana wa CHADEMA na ACT wakiongozwa na akina Maria Sarungi.
McAllister ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya nje ya Bunge la EU anatoka nchi ya Ujerumani. Huyu ni mwanachama wa Christian Democratic Union (CDU). Chama Cha CDU ni mwanachama wa vyama vya Kidemokrasia Duniani. Chama cha CDU ndicho cha rafiki na ambacho kimekuwa kikitoa msaada wa Fedha kwa Chama Cha CHADEMA nchini Tanzania. Hivyo walichokifanya CHADEMA ni kumtumia David James McAllister kuwashawishi wajumbe wa EU kuwa wao wanaonewa na Tanzania ipewe vikiwazo. Walimtumia huyu bwana kwa kuwa amekuwa mshirika wao wa muda mrefu kama ilivyo kwa CCM kwa chama cha Kikomunisti cha China.
Ukimsikiliza kwa umakini akichangia hoja hii Ndg McAllister amesema kuwa EU iangalie njia mpya ya kuisaidia Tanzania. Amesema wanaweza kupitishia misaada yao kwa watu ambao wanaona misaada yao itakuwa Salama. Lakini anasisitiza kuwa wao walikuwa wakifuatilia uchaguzi wa Tanzania wakishirikiana na CHADEMA.
McAllister hajawahi kuipenda serikali ya Tanzania, yeye siku zote amekuwa anaipenda CHADEMA ambacho ndicho chama masilahi kwake.
McAllister hawezi kuisifia Tanzania, hata iweje. Linapokuja suala la Tanzania kwake nyeusi ni nyeupe. Ataisifia Tanzania tu, pale mtakapoona CHADEMA inaisifia CCM, kinyume na hapo hakuna lolote. McAllister ndiyo silaha ya CHADEMA kwenye vikao vya EU.
Tafakari.