David mattaka out ATCL

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,722
21,775
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwenye mitambo ya mi-chichemi zinasema
Aliekuwa mkurugenzi wa ATCL bw DAVID MATTAKA maji yamemfika shingoni kaamua kulitema mzigo wa ATCL.(RESIGNATION)
Akiongea kwa uhakika mtoa chanzo ambae aliomba jina lake lisitajwe amesema bwa mattaka aliamua hivyo baada ya kubanwa sana na wafanyakazi wakiwemo viongozi wenzake waliomo kwenye menejiment.......
for more info stay tuned:
 
Duh kwa hiyo kajiuzuru au wamemtemesha?
Hapo sasa kazi inaanza bora alivyo bwaga manyanga.
 
hii itakuwa habari njema, lakini muungwana anaweza kumbeba tena na kumpa the restructured nic
 
Mi nawasiwasi watu kama hawa utaona wanaibukia kitengo kingine hili swala la kubebana sijui mpaka lini nyie subili huko kabolonga mtaona anapewa kitu kingine kwa kigezo eti ufanisi wake wa kazi.....
Naililia Tanzania yangu.
 
He's probably a future Managing Director wa Tanesco au NIC....

Nchi hii inajengwa na wenye moyo nakuliwa na wenye meno.
 
hii itakuwa habari njema, lakini muungwana anaweza kumbeba tena na kumpa the restructured nic

umezaliwa siku ya mageneous duniani nini??
habari zilizopo na anavyowaaga wenzake zinasema mzee kaamua kumkabidhi NIC..SO cu
 
kwa walio wengi, bwn. mataka amechelewa kujiuzuru. he should have done this (retired) long time ago. kama amefenya hivyo amelinda heshima yake, pia, licha ya kuliokoa shirika.
 
Wakuu,

Nadhani tusubiri confirmation, maana Idris ali-"resign" baada ya muda akawa-"reinstated".!!!
 
Kujiuzulu tu haitoshi bali ni hatua nzuri. Anatakiwa awajibishwe kwa makosa ya wazi aliyofanya. Inakuwaje vile?
 
Mambo kama hayo kwa JK hayamsumbui, kesho utasikia kaambiwa na Rais arudi kazini kama ilivyokuwa kwa Idrisa Rashid wa TANESCO
 
Somo gani tumepewa leo????

HAWA MAFISADI NI KUKOMAA NAO. Tunawalea wenyewe na kuanza kumlaumu Kikwete. Nafikiri FMes na Mkandara wamekuwa wakisema sana hili. Sasa hivi tunaona kipenzi cha Kikwete kalazimishwa kuachia ngazi.

Nafikiri kuna haja ya TANESCO wakakomaa na Badra Masoud na Idriss ili waondoke.

YES WE CAN
 
Mambo kama hayo kwa JK hayamsumbui, kesho utasikia kaambiwa na Rais arudi kazini kama ilivyokuwa kwa Idrisa Rashid wa TANESCO

Subutu! Labda kama JK naye kachoka na kazi yake, maana kwa hili watanzania tusipoandamana tena against hilo mi nithama nchi! Tumechoshwa na haya majitu bwana.
 
duh! hapo atakuwa ameonesha dhana ya uwajibikaji ila kwa mashinikizo makubwa maana pale palishamshinda mda mrefu ,ila kwa kuwa muungwanwa yu pamoja nae basi ndo hivyo tena ataendelea kubebwa.
 
Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwenye mitambo ya mi-chichemi zinasema
Aliekuwa mkurugenzi wa ATCL bw DAVID MATTAKA maji yamemfika shingoni kaamua kulitema mzigo wa ATCL.(RESIGNATION)
Akiongea kwa uhakika mtoa chanzo ambae aliomba jina lake lisitajwe amesema bwa mattaka aliamua hivyo baada ya kubanwa sana na wafanyakazi wakiwemo viongozi wenzake waliomo kwenye menejiment.......
for more info stay tuned:

Kama ni kweli heri maana huyu naye kilikuwa kiwavi cha kula mashirika. Kote alikopita CV si nzuri. Wacha tusubiri confirmation. Lakini kama ni kweli pia inabidi jamaa achukuliwa hatua kwa maamuzi mabovu....
 
Mattaka ni "poodle" tu wa wakubwa. Nahisi atapelekwa kwenye shirika jingine akasimamie vizuri ukombaji.
 
Tusubiri confirmation but all in all the guy failed to turnaround the company, how could you have more than 200 employees with only about 4 small planes?
 
More info
ameondoka ana madeni ya million 80
million 100 alikopa kwenye gari merd-benz
akalipa ikafikia million 60....
Mchanganuo
katka million 20
million 10 amekuwa akichukua sehemu ya kununulia ticket million 2 kila wiki mwanzoni alidai za matumizi wakamshupalia alipe akadai liingie kwenye deni....million 10 iliobaki ni aibu.....
Akiwa ofisini kumekuwa na wasichana wakijazana ofisini mwake kuja kuchukua ticket za bure...anawaambia accounts niandikie deni....sasa tunauliza nana atalipa hizi???
Kazi kwelikweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom