David Mathayo David......CV yako ndio hii, yanini kuwadanganya Watanzania???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

David Mathayo David......CV yako ndio hii, yanini kuwadanganya Watanzania????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Blood Hurricane, Jul 3, 2012.

 1. Blood Hurricane

  Blood Hurricane JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2012
  Messages: 1,151
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Jina
  Jina la kwanza ni Mathayo David Msuya. Ila baada ya kuingia anga za siasa, aliamua kulibadili jina lake kuwa Mathayo David Mathayo na kuondoa jina la ukoo "Msuya" ambalo ni jina la baba yake halisi David Msuye aliyewahi kuwa waziri mkuu.

  Masomo
  Matayo David Msuya alisoma Tosamaganga Iringa, alifanya CBG (1989-91) aliishi bweni la Mwenge. Uwezo wake wa kimasomo haukuwa mkubwa ila alishangaza wenzanke na waalimu alipopata daraja la kwanza kwa pointi 7. Alipata msaada sana kutoka kwa kaka yake aliyekuwa akifundisha chuo cha ualimu Mkwawa, Iringa.

  Matayo ulikwenda JKT itende, Mbeya. Baada ya hapo, alichanguliwa kwenda kusoma Makerere Uganda kwa kupitia mfuko wa mwalimu Nyerere. Mathayo alinufaika kwa fedha hizo ila hakwenda Uganda, akaamua kusoma SUA ya tiba ya mifugo (Bachelor of Veterinary Medicine) mwaka 1993-1997. Huko SUA Matayo alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyekuwa na radio yenye double deck, (system) na TV set.

  Uwezo wa kifedha ulisaidia kumpa Mathayo maisha ya kifahari chuoni SUA ambapo alikuwa na wasichana kadhaa ikiwa ni pamoja na Mugros na Betty Manase

  Mwanzo wa siasa
  Siasa alizianza rasmi mwaka 1995 alitumia TV yake kwenda kuonyesha vijijini madhara ya vyama vingi, alitumia mapigano ya Rwanda na Burundi kama kutishia wananchi wasikubali upinzani na kipindi kile wananchi walikuwa wepesi kuelewa kumbuka TV hazikuwa nyingi Tanzania kipindi kile. Alijijengea umaarufu sana ndani ya chama mkoani Morogoro na kitaifa.

  Aligombea ujumbe wa NEC mkoa wa Morogoro kundi la vijana alishinda. Mathayo alimaliza SUA 1997 na kupata kazi ya kufundisha chuo kimoja huko Serowe Botswana. Kwa kuwa mjumbe wa NEC alikuwa karibu na akina Lowasa, JK na vingunge wengine aliweza kuwa anaonana na akina Makamba na akawa ni mwanamtandao. Wakati huo Matayo alikuwa akirudi Tanzania kufanya shughuli zake za kisiasa wakati bado ni mwajiriwa wa serikali ya Botswana.

  Kwa mfano wakati mmoja alirudi Tanzania na kuwahamasisha wanafunzi wa SUA (kama 200 hivi) na kuwapeleka Dodoma kupokea kadi za CCM chini ya mwenyekiti wa CCM Mkapa. Wanafunzi walahidiwa wangepatiwa ajira kwa kufanya hivyo. Hii ilimjenga sana Matayo ambaye aliisha kuwa maarufu kwenye ofisi za chama Dodoma, kama mjumbe wa NEC na mkutano mkuu.

  Mwaka 2000 aligombea Ubunge Same Magharibi na kushinda na kuteuliwa kuwa waziri mdogo. Wakti huu aliisha tamka kwamba amesomea Afrika Kusini digrii ya falsafa (PhD). Prof Msolla wakati aliyekuwa waziri wa elimu ya juu na sayansi ambaye aliwahi kufundisha SUA alimjua sana Matayo na alimwita Matayo na kumuuliza kuwa PhD alifanya lini na wapi na pia aletee PhD thesis yake. Prof Msolla alisema "Matayo aliogopa sana na alikili mbele yangu, kuwa Prof mimi nimetumia hii title kisiasa zaidi, sina MSc wala PhD"1.

  Kashfa ya vyeti bandia

  Dr Mathayo ni mmoja wa wabunge vijana waliochaguliwa na Raisi Kikwete kuwakilisha ngwe yake ya "Nguvu mpya" kama naibu waziri. Katika awamu hii Kikwete alionekana amechagua vijana wenye vipaji na elimu. Vyeti vya Mathayo's zimeleta kizaazaa tangu alipochaguliwa kwenye uwaziri mwaka 2005. Matayo alihitimu chuo kikuu cha Kilimo (SUA) mwaka 1997 kama daktari wa mifugo. Baada ya hapo alitoka nje ya nchi kwenda kutafuta ajira Botswana ambako aliajiriwa na serikali ya Botswana kama mwalimu kweny chuo cha kilimo huko Serowe.

  Mathayo anadai kwa mwaka huo huo alianza digrii ya MSc 1998-2001, halafu PgDip (2000-2001), na PhD (2001-2003). Watu wengi wanaomfahamu ikiwa ni pamoja na waalimu wake wa SUA wanashangaa Mathayo aliwezaje kusomea vyeti vyote hivyo kwa muda wa miaka mitano huku akifanya kazi kama mtumishi wa serikali Botswana? Pia kashfa kwamba alikuwa akipokea mishahara miwili ya uwaziri na utumishi wa serikali ya Botswana haijajibiwa hadi leo.

  Source: Waliosoma nae.
   
 2. T

  TUMY JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 22, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mhh makubwa.mie sifahamu lolote kwa kweli kuhusu huyu Mheshimiwa.Ila shukrani kwa info.
   
 3. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa mwanachama wa magamba hilo siwezi kulishangaa. Akikabwa sana koo, utasikia anajitetea kwamba uDr wake ni wa tiba za wanyama na siyo PhD. Magamba ndiyo yanayoididimiza nchi hii kwa mavyeti ya kufojifoji tu ili mradi siku zinakwenda. Ole wenu siku zenu zinayoyoma kama barafu juani. Mwisho wa siku, mtatamani mkimbilie nje ya nchi kujiokoa.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  mtoto wa cleopa msuya kumbe!wanarithishana madaraka kama nyumba!siku moja mwanaasha utasikia ni waziri
   
 5. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Wacha ubishi umeambiwa ni DAVID MSUYA.
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  CLEOPA DAVID MSUYA aliwahi kuwa waziri mkuu we gamba,weka kumbukumbu zako sawa au unajifanya taahira
   
 7. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Acha kuchemka.
  Cleopa David Msuya, ni mbunge wa zamani wa jimbo la Mwanga na Waziri Mkuu wa zamani, waziri wa fedha wa zamani enzi za Mwinyi n.k.
   
 8. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hivi huyu jamaa yukoje vile? Maana kwa sura simjui uongo dhambi!!!

  Mweye picha yake aiweke basi...
   
 9. L

  Lihove JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Huyu ni Dr wa wanyama bwana full stop!!!!
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  nasikia akiwa Tosa alikuwa anasoma sana pamoja na kujihusisha na mambo ya siasa. Alikuwa ni kiongozi wa umoja wa vijana wa shule ya Tosa enzi hizo.kwahiyo ile division one haikuwa ya bahati mbaya. Hata hivyo CBG used to take the best!
   
 11. s

  simon james JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 283
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilaza!!
   
 12. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  yesu!! nchi ya wenyewe hii
   
 13. Kiwewe

  Kiwewe Senior Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nikweli huyu jamaa anafahamika kwa ujasiriamali kwenye kila kitu kilichombeleyake. Nakumbuka alikuwa akitumia VIDEO yake enzi hizo kwa kuonyesha mikanda yangono kwa kiingilio, wewe kama upon aye karibu muulize kisusio uoneatakavyostuka. Alinyesha mkanda wa yale maafa ya MV.Bukoba kwa kiingilio piapale multipurpose hall. Jina lake halisi ni David Mathayo Msuya ndilo alilokuwaakitumia. Na sote tulifahamu kuwa ni motto wa waziri mkuu mstaafu Mzee Cleopa DavidMsuya. Alikuwa ni kati ya wanafunzi wawili wa undergraduate wenye gari (ilailikuwa choka mbaya sana). Kuhusu Mugro naomba nilihifadhi hilo, ila ametushangazasana jinsi alivyopata PhD hiyo, na tulimsikia Spika Sitta enzi hizo akimsafishahuyu jamaa bungeni kuwa elimu yake ni ya halali. Pia kunawakati alishajiitaProfesa kwenye Nyanja za uchumi, ila hili alilipotezea hewani. Tunawasiwasisana na kushinikiza kitendgo cha accreditation cha Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU) watoe ripoti yake nzuri. Pia tunawasiwasi hata kuibiwa kwa computers nyeti pale TCU wanamweza kuwa wamehusika hawakatika kupoteza ushahidi wa kudanganya elimu zao. Pia tunawasiwasi kuwa nimmoja aliyemshawishi JK kumtosa Prof. Msola (Mbunge wa Kilolo-Iringa) asiwepokwenye uwaziri tena, kwani alipokuwa elimu ya juu alimuumbua kuwa huyu jamaahana PhD. Bahati mbaya sana vyombo vyetu vya serikali na watu wetu wa usalamahawashughuliki na kuhakiki CV za watu ambao wanakuja kupewa madaraka makubwakuliko uwezo wao na kupelekea ufanisi mbovu na kuliingizia Taifa hasara kubwa. Tumeshangaakuona tena Technician Stella Manyanya akijulikana ni Engineer na alishapewanafasi ya kuongoza Shirika la Tanesco, siajabu amechangia sana kuliuwa hilishirika. Nashauri Serikali ifanye uhakiki wav yeti kwa watumishi wote wa ummakama ilivyofanya kwa wanataaluma vyuo vikuu. Hili litasaidia kupatikana mtumwenye sifa halisi kulingana na majukumu anayopewa.
   
 14. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Lazima wewe unamfahamu vizuri na pia ulisoma naye SUA. Kwa jinsi ulivyoeleza haiwezekani source ikawa waliosomanaye maana ni 99 % true. Namfahamu Matayo ingawa siyo rafiki yangu na huyu bwana ni kweli at one time alikuwa Pretoria Msc in Animal Science na alikuwa anafanya thesis na pia ana mpango wa register for PhD Free State wakati anamalizia. Ila kitu ambacho siwezi kuthibitisha kama alimaliza hiyo PhD degree program yake maana sijaona publication yeyote kwenye google yenye jina lake. Kawaida vyuo vya RSA huwa vinapublish thesis kwenye mtandao. Halafu kitu kingine huwezi kugraduate PhD RSA bila kupublish paper!! Sasa unaweza ku-google ili kuthibitisha hilo baada ya kuandika hisia zako na kjalibu kumchafua mtu bila sababu.
   
 15. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  To hell with their PHDs' and DVDs' kwani zinaliwa ili watugawie na sie??
   
 16. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Mpaka mama wa kwanza amenuna bana

  [​IMG]
   
 17. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  MATAYO CLEOPA DAVID MSUYA: TAMAA YA UKUBWA WA KITAALUMA YA NINI? UNAJUA UNGEWEZA KUENDELEA NA MAISHA BILA BUGHUDHA YOYOTE .WATANZANIA WANAKUAMINI. LAKINI MIMI MWENYEWE HILI LIMENITIA SIMANZI. KWANINI UKANE JINA LA UKOO WAKO

  LAANA YA BABU ITAKUPATA TU. MAMBO MENGINE YASINGEJULIKANA LAKINI KUTOKANA NA KUJIKWEZA UMEUMBUKA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. AJIKWEZAYE HUSHUSHWA. KAMA NI UONGO LETA DATA ZA KIUKWELI HAPA DOGO. SASA MAMBO HADHARANI YAANI HADI MUGROS. KWA TAARIFA MUGROS (CHEAP GIRLS) NI WASICHANA WA KAZI WALIOKUWA WAKIWAPIKIA WANAFUNZI VYUMBANI KULE SUA. SIFA YAO NI KUWA TAYARI KUONDOKA NA YEYOTE BAINA YA MAROOM MATES. SOMETIMES . MAROOMATES HUGONGANA KWA KUSINGIZIA KUTOKWENDA AU KUTOROKA DARASA; KILA 1 AKIAMUA KURUDI KWA WAKATI WAKE NA MATOKEO NI KUGONGANA. LAKINI MBAYA ZAIDI MUGROS WALIKUWA PRONE TO STI KUTOKANA NA KUCONJUGATE NA WANAFUNZI TOFAUTI UNPROTECTEDLY.KWASASA CHUO CHA SUA KILIPIGA MARUFUKU SHUGHULI ZA KUPIKIA VYUMBANI NA HIVYO KUSITISHA VIBARUA VYA MUGROS TANGU WAKATI HUO AUTOMATICALLY.
  D. MSUYA, WENZIO WANASOTEA SUA 2-3 MSc, 3-6 PhD we mwenzetu unaukwaa kiulaini. kudos prof Msolla kwa kubainisha ukweli otherwise this guys would be respected undeservingly. adios amigo
   
 18. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
 19. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  Msanii mwingine huyo.
   
 20. N

  Ndakilawe JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 4,084
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280
  sasa kama ni mtoto wa Cleopa Msuya, kwa nn akaenda kugombe ubunge Same, na sio Mwanga nyumbani kwake?
   
Loading...