David Mataka aliyehukumiwa 20 Agosti, 2021 aliwahi kuhukumiwa Mwaka 2017 kwa kesi ileile na Mahakama ileile

Tumerudi yyale Yale ya awamu ya jakaya
Hakuna cha awamu ya jkaya mkapa mwinyi magu...
Mbona awamu ya jkaya yoga na mramba,walipigwa mvua hadi kufanyishwa kazi
Ya kupiga deki kufagia
Hukumu za nchi hii inategemea maelewano yako na watu wa mfumo
Ukiona umehukumiwa basi kuna kukomelewa etc

Ova
 
Kuna jambo limenishangaza sana!

Jana Mahakama ya Akimu Mkaazi Kisutu ilimuhuku aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kwenda jera miaka minne ama kulipa Faini Milion 8 kwa kuisababishia ATCL hasara ya Tsh Billion 71.

- David Mataka ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kuisababishia hasara ATCL ya Tsh Bilioni 100

Ajabu ni kuwa hii kesi iliwahi kusikilizwa mwaka 2017.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha ambaye ni Askofu wa Kanisa la Pentecoste Motomoto, Elisaph Mathew.

Wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 35 kwa kila mmoja kutokana na mashtka yao sita waliyokuwa yanawakabiri pia Mahakama imewataka washtakiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL kwa kununua magari chakavu 26, yalikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 143 ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande mwingine, Mahakama imemuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za ATCL

- Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mattaka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

Je, Serikali imeamua kutuchezea mchezo mchafu wananchi? Kesi ilisikilizea Mahakama ya Kisutu na ikatolewa hukumu kama rufaa si ilipaswa ikatwe mahakama ya juu? Iweje kesi moja inatolea uamuzi tofauti? Kuna nini kipo nyuma ya pazia juu ya kesi hii? Au mkisubiri JPM afariki muanze sarakasi?

View attachment 1901448View attachment 1901449
Unajua kama hujafanya utafiti wa kutosha sio vema kutoa lawama,hukumu za mahakama ni wazi wewe nenda huko mahakamani utapewa taarifa kamili

Sent from my SM-N960F using JamiiForums mobile app
 
Kinachokusumbua mtoa mada ni kukosa elimu na kujifanya unajua wakati hujui. Hapo hakuna kesi mbili zinazofanana bali ni mashitaka mawili yanayoshabihiana. Rudi shule ukasome japo kacheti ka sheria.
Kwa mantiki hiyo tufafanulie hii inamaana kesi ya Mwanzo ilikuwa ni hasara ya bill 100 ni tofauti na hii ya hasara ya bill 70s..?
 
Nchi ina matatizo sana hii kuna mtu alinunua boti chakavu kwa bilioni 8 na haikuwahi kufanya kazi hata siku moja tokea inunuliwe na hakufanywa chochote.
Hahaa nakumbuka ilikuwa inatoka Bagamoyo to Dar ilifanya kazi kama wiki 1 tu, ilikuwa inatumia masaa 4
 
Ukisikia deed assignments ndo hizo
Huyo hana tofauti na mzee simba kawawa aliyebebeshwa lawama zoote za serikali awamu fulani ya Uongozi

Alichokua anakifanya serikali au watendaji fulani muhimu wajuu walijua kila kitu ndo mana unakuta kila mtego alioingia kifungo cha kichekesho kikiambatana na faini...

Yeye ni mbeba lawama zotee kama alivokua kawawa

Sasa kwanini wanapoteza pesa na muda wa mahakama, sio ni bora wasingempeleka mahakamani.

Hiyo ilitakiwa iwe kesi ya uhujumu uchumi. Faini 300 billioni na miaka 10 ndani. Au kifungo cha maisha. Ndio njia sahihi ya kumaliza upigaji.
 
Hahaa nakumbuka ilikuwa inatoka Bagamoyo to Dar ilifanya kazi kama wiki 1 tu, ilikuwa inatumia masaa 4
Haikufanya kazi kabisa ilienda kwa majaribio ilitumia zaidi ya masaa matatu ilivyo rudi wakadai watakuja waliyoiunda waifanyie marekebisho ikawa ndio imetoka,halafu mtu huyo alipopata madaraka zaidi kazi yake ilikuwa ni kuwananga watangulizi wake na kudai nchi ilichezewa sana huku yeye akijiweka pembeni akijifanya ni mtakatifu.
 
Hapo ndipo napoyapendea mafisadi yana umoja kweli.

Mambo yakiaribika kuna ‘fall guy’ ila wakipata nafasi tu wanakuokoa. Majamaa loyalty kwao ni muhimu sana.

Yule wa mwendokasi nae sio muda mrefu atakuwa uraiani.
Huna taarifa wa mwendokasi yuko nje kitaaambo anakula mema ya nchi wewe usicheze na sukuma gang wewe
 
Kuna jambo limenishangaza sana!

Jana Mahakama ya Akimu Mkaazi Kisutu ilimuhuku aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kwenda jera miaka minne ama kulipa Faini Milion 8 kwa kuisababishia ATCL hasara ya Tsh Billion 71.

- David Mataka ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kuisababishia hasara ATCL ya Tsh Bilioni 100

Ajabu ni kuwa hii kesi iliwahi kusikilizwa mwaka 2017.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha ambaye ni Askofu wa Kanisa la Pentecoste Motomoto, Elisaph Mathew.

Wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 35 kwa kila mmoja kutokana na mashtka yao sita waliyokuwa yanawakabiri pia Mahakama imewataka washtakiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL kwa kununua magari chakavu 26, yalikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 143 ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande mwingine, Mahakama imemuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za ATCL

- Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mattaka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

Je, Serikali imeamua kutuchezea mchezo mchafu wananchi? Kesi ilisikilizea Mahakama ya Kisutu na ikatolewa hukumu kama rufaa si ilipaswa ikatwe mahakama ya juu? Iweje kesi moja inatolea uamuzi tofauti? Kuna nini kipo nyuma ya pazia juu ya kesi hii? Au mkisubiri JPM afariki muanze sarakasi?

View attachment 1901448View attachment 1901449
Sidhani kama hili limefanyika, lakini kama kuna ukweli wowote basi kutakuwa na uzembe mkubwa kwa upande wa Mahakama za Tanzania.

Kesi ileile haipaswi kusikilizwa mara mbili na Mahakama ileile ikuhusisha watu walewale na kosa lilelile, kitaalamu hii inaitwa res judicata.

Nafikiri mtoa mada utakuwa hujafuatilia vizuri. Inawezekana hizi ni kesi mbili tofauti (two different offences).

Naomba kubakia.
 
Back
Top Bottom