David Mataka aliyehukumiwa 20 Agosti, 2021 aliwahi kuhukumiwa Mwaka 2017 kwa kesi ileile na Mahakama ileile

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,220
12,939
Kuna jambo limenishangaza sana!

Jana Mahakama ya Akimu Mkaazi Kisutu ilimuhuku aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mataka kwenda jera miaka minne ama kulipa Faini Milion 8 kwa kuisababishia ATCL hasara ya Tsh Billion 71.

- David Mataka ahukumiwa kulipa faini Tsh milioni 8 kwa kuisababishia hasara ATCL ya Tsh Bilioni 100

Ajabu ni kuwa hii kesi iliwahi kusikilizwa mwaka 2017.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) David Mataka na aliyekuwa Kaimu Ofisa Mkuu Kitengo cha Fedha ambaye ni Askofu wa Kanisa la Pentecoste Motomoto, Elisaph Mathew.

Wawili hao wamehukumiwa kifungo cha miaka 6 jela ama kulipa faini ya Sh.milioni 35 kwa kila mmoja kutokana na mashtka yao sita waliyokuwa yanawakabiri pia Mahakama imewataka washtakiwa hao kulipa hasara waliyoisababishia ATCL kwa kununua magari chakavu 26, yalikuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 143 ndani ya mwezi mmoja.

Kwa upande mwingine, Mahakama imemuachia huru William Haji aliyekuwa mkaguzi mkuu wa hesabu za ATCL

- Mahakama imemhukumu aliyekuwa Mkurugenzi wa ATCL, David Mattaka kifungo cha miaka 6 au faini ya milioni 35

Je, Serikali imeamua kutuchezea mchezo mchafu wananchi? Kesi ilisikilizea Mahakama ya Kisutu na ikatolewa hukumu kama rufaa si ilipaswa ikatwe mahakama ya juu? Iweje kesi moja inatolea uamuzi tofauti? Kuna nini kipo nyuma ya pazia juu ya kesi hii? Au mkisubiri JPM afariki muanze sarakasi?

Screenshot_20210821-150157_Instagram.jpg
Screenshot_20210821-144100_Samsung%20Internet.jpg
 
Back
Top Bottom