David Kafulila: Wasukuma siyo watu wa kulalamika

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Mkuu wa mkoa wa Simiyu bwana David Kafulila wakati akitambulishwa kwa wakazi wa Simiyu amewasifu kwa uchapakazi na kusema wao siyo watu wa kulalamika, kwao ni kazi tu.

Bwana Kafulila amesema kabila la wasukuma kwa sasa wako kila mahali nchi hii palipo na fursa wakichapa kazi na hata jimbo analotoka la Kigoma Kusini wamejaa na wamenunua maeneo makubwa wakilima kwa bidii sana.

Bwana Kafulila amesema anajivunia kuwa mkuu wa mkoa wa Simiyu na kumuonya mtangulizi wake kuwa ataendelea kupokea vipigo kwenye nyanja zote kwenye mkoa wake mpya wa Dodoma.

Hiki jamaa kimesoma lakini hakijaelimika, kinazungumziaje habari za makabila karne hii ya 21!! ? Kama kiongozi anatakiwa kuzungumzia watanzania, anasahau kuwa kuwepo kwa wasukuma Kigoma kuna kuwepo kwa wanakigoma Mwanza na kwingineko na huo ndiyo utanzania
 
Hata ng’ombe hawalalamiki.
 
Hiki jamaa kimesoma lakini hakijaelimika, kinazungumziaje habari za makabila karne hii ya 21!! ? Kama kiongozi anatakiwa kuzungumzia watanzania, anasahau kuwa kuwepo kwa wasukuma Kigoma kuna kuwepo kwa wanakigoma Mwanza na kwingineko na huo ndiyo utanzania

Sababu wametukanwa sana,ila karibu wote wamekaa kimya.

Hata hapa JF wako kimya 20m people wanaangalia 3m matusi yenu hapa TZ. JF wapo zaidi ya 20% wako kimya, wako kimya.

Wanamlinda Rais, Serikali, wanakulinda wewe taratibu bila mbwembwe. Ukizingatia idadi yao yuko sahihi sana ni watu watulivu, wapenda amani.
 
Kweli kabisa mkuu
 
Nilikuwa na rafiki zangu Wasukuma enzi hizo majeshi. Tulipangwa combania moja. Enzi hizo tunapanua mashamba ya gendagenda. We bwana ee!! Ilikuwa raha sana wakati wa kung'oa visiki vya migunga. Ni nyimbo tu Kwa kwenda mbele: Mmoja anaanza: "Igogo pihinduka"
Wote tunajibu: "Igogo pihinduka, enhee, Igogo pihinduka"
Safi sana Wasukuma.
 
Hahaha
 
Sababu wametukanwa sana,ila karibu wote wamekaa kimya.

Hata hapa JF wako kimya 20m people wanaangalia 3m matusi yenu hapa TZ. JF wapo zaidi ya 20% wako kimya, wako kimya.

Wanamlinda Rais, Serikali, wanakulinda wewe taratibu bila mbwembwe. Ukizingatia idadi yao yuko sahihi sana ni watu watulivu, wapenda amani.
Nyie Ni wakabila hamna cha nn wala nn baba yenu alibeba sana
 
Back
Top Bottom