David Kafulila: Natofautiana na Zitto kuhusu ripoti za CAG na mwenendo wa uchumi

Chesty,
Acha ujinga Basi. Mtu aliyeweka Malengo ya Tsh
30000 akapata tsh.29000, halafu katika mazingira hayo hayo mwingine akaweka malengo tsh.100000 akampana akapata 60000, kwa akili yako utasema wa tsh.29000 amefanikiwa kwa vile amekaribia kutimiza malengo. Simple, huyu ni Mvivu! Na kama.nyie ndo wachumi naanza kueleewa kwanini Africa tunaendelea kuwa wasindikizaji.
Pole sana. Katafute hata darasa la ngumbaru, litakuinua kidogo kwenye uelewa. Inaonekana huelewi kabisa maana ya projection.
 
Kafulila; ndiyo maana Dr. Slaa alikuita kichunguu....kwenye mlima.
 
Malengo ni tofauti na matamanio au ramli. Kuna hesabu zinazokuongoza kuweka malengo fulani. Na ukishindwa kuyafikia, kuna mahali utakuwa umefanya makosa.

Malengo hutokana na mathematical projections, na hutumia takwimu za nyuma, ndiyo maana ukishindwa kufikia huashiria mapungufu katika utendaji wako.
Mkuu hawa uvccm wengi wana division zero au four mbaya Ila wana mdomo kusuku anasubili
 
Serikali ya JK iliandaa miundo mbinu mizuri ya ukusanyaji mapata.
Iliandaa Mshine za EFD, rada kwa polisi, ujenzi wa mizani za Tanroad nchi nzima.

Lakini pia Serikali ya JK ilikua haikusanyi kodi za Nyumba za Halmashauri na viwanja.
Sijajua kukusanya kodi mpaka za maji ya mvua ni kukua uchumi au ni vipi?

JK alichafuliwa kutokana na Uhuru wa vyombo vya habari na wanasiasa Uchwara kama Kafulila kujipatia nafasi ya kujulilana na kutafuta umaarufu lakini kiukweli Mwacheni Mzee JK apumzike zake Kule Msoga. Amefanya Mengi kwa taifa lake na wananchi wengi walipata kipato cha kuendesha maisha yao na ajira.

JK hakuwa mkoloni na hakuendekeza sana masheria ya kikoloni yanayomuangamiza binadamu na kuacha dunia ikiwa haina biumbe zaidi ya majengo marefu.

Kafulila aonyeshe ubunifu wake huko alipo na aachane na siasa nyepesi kama enzi za JK alivyokua anatafuta kiki.

JK aliwafukuza mawaziri wengi tu kwa ufisadi au alitaka awafanyeje!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pingeni hoja zake kama yeye alivyochambua za Zitto
sina shaka na hoja zake,kinachonikera ni kwamba haya anayoyaongea sasa akiwa upande ule wa pili hayaongei na aliyoyaongea kipindi yupo kule kwa kuwa yupo huku hawezi kuyaongea......

UNAFIKI MBAYA SANA
 
Kwa Kawaida siku zote Makadirio sio mapato halisia au si kit 1000 digits,

Je haya tumeyasahau mapema kiasi hiki?

Bajeti ya 2013/2014 ilivyoshindwa kufika lengo la ukusanyaji


Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kuanza kwa Bunge la Bajeti, Serikali imeshindwa kutekeleza bajeti ya mwaka 2013/14 kutokana na kukosa fedha na hivyo kusababisha miradi mbalimbali katika halmashauri nchini kukwama.

Katika bajeti ya mwaka 2013/14 Serikali ilitenga Sh4.2 trilioni kwa ajili ya halmashauri zote nchini, lakini fedha za maendeleo zilizofika katika halmashauri hizo ni asilimia 43 tu na za matumizi ya kawaida asilimia 76, hivyo halmashauri kushindwa kutekeleza miradi iliyojipangia kwa kipindi hicho cha mwaka wa fedha.

Juzi wakati akisoma Mwelekeo wa Bajeti ya mwaka 2014/15, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya alisema sababu ya kutotekelezwa kwa miradi mbalimbali ni kutokana na Serikali kushindwa kukusanya kodi ipasavyo katika mwaka wa fedha wa 2013/14.

Alisema pia kulikuwa na mapato pungufu ya kodi ya kampuni kuliko ilivyotarajiwa kutoka kwenye baadhi ya kampuni za madini kutokana na kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia.

Alitaja sababu nyingine kuwa ni kampuni za simu za mkononi kutokusanya tozo ya kadi za simu ambayo ilitarajiwa kuiingizia serikali mapato ya Sh178 bilioni

Chanzo mwananchi

Kwa namna yoyote Ile, Kafulila Yuko sahihi Kwa hoja zake
 
Mbona hamjadili hoja alizowasilisha, Bali mnafanya personal Attack?

Leteni hoja wakuu....Hii nchi yetu sote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kimsingi huyu kafulila hana hoja zaidi anataka na yeye aonekane ana uwezo wa kuchambua mambo kama zzk so anachofanya anasuhiri zito aanzishe hoja alf na yy anadokoadokoa alf anatengeneza hoja ili naye aonekane anajua lkn kwa kifupi anachofanya ss hv hana tofaut na musiba!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom