David Kafulila: Mwanasiasa aliyedondoka toka ghorofa ya 10

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Nimesoma makala za David Kafulila za 2006 nikakumbuka kwamba huyu ndiye aliyedondoka toka ghorofa ya 10 mwaka 2008:

1. Je, hali yake inaendeleaje?

2. Uchunguzi umesema ajali ilitokana na nini hasa?


"Jumaa alisema kuwa, Kafulila alifikishwa kitengo cha MOI baada ya kuumia vibaya miguu kutokana na kudondoka kutoka ghorofa ya 10 hadi ya pili alipokuwa akishuka kwa kutumia lifti katika hoteli ya Concord. Awali ilidaiwa kuwa, Kafulila alikumbwa na mkasa huo wakati alipokuwa akitoka kwenye semina ya vijana na wanawake wa chama hicho, iliyofanyika katika hoteli hiyo.

Kwa mujibu wa Kafulila, baada ya kutoka kwenye semina aliondoka kwenda kupanda lifti ya hoteli hiyo ambapo aliikuta wazi.

Aliongeza kuwa, baada ya kukuta mlango wazi aliuliza na akaambiwa ndivyo lifti hiyo ilivyo na kuwa akiingia itajifunga, lakini alipoingia alijikuta akitumbukia moja kwa moja hadi chini."

Chanzo: Mtanzania
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom