David Kafulila: CCM is the most dynamic and Flexible part in Africa, CCM inapambana kukidhi mahitaji ya wananchi kulingana na wakati

GUSSIE

JF-Expert Member
Dec 2, 2014
3,866
11,100
David Kafulila ambaye ni mkuu wa mkoa wa Manyara kwa sasa akihojiwa na Wasafi TV Katika kipindi cha msumari wa moto ameulizwa swali :

Kwanini ccm bado ipo madarakani wakati vyama vingine vikongwe barani Afrika vimeshajifia?

Jibu la David Kafulila,Kushindana na ccm ni ngumu sana kwa wapinzani kwani ccm ni chama kinachobadilika badilika kulingana na mazingira na wakati, CCM ni ile ile lakini haifanani toka awamu moja kwenda nyingine

David Kafulila, CCM ya nyerere ni tofauti na ccm ya Mwinyi, CCM ya Mwinyi ni tofauti na ccm ya Mkapa, CCM ya Mkapa ni tofauti na ccm ya JK na ccm ya JK ni tofauti na ccm ya JPM lakini CCM ni ile ile,

David Kafulila, CCM ni flexible sana Katika bara la Afrika, Zinapoibuka hoja za rushwa kwa wakati fulani wanawaletea mtu ambaye hataki hata kusikia neno rushwa hivyo hoja za rushwa zinajifia kwa wapinzani

David Kafulila, likiibuka swala la uhuru wa habari na demokrasia wanawaletea mtu ambaye anabadili upepo ghafla kwa kuacha watu kujibu hoja wapendavyo na hivyo upinzani kukosa hoja

David Kafulila kushindana na ccm ni ngumu sana kwani kuna wakati hoja zinazoibuliwa na upinzani zinageuka hoja za ccm na kufanyiwa kazi kwa ufasaha

David Kafulila anasema, ccm inapambana kujibu hoja za wananchi kwa wakati na wala haishindani kujibu hoja za upinzani

Anasisitiza ccm ina wa swap wapinzani,:waliokuwa wapinzani wa nyerere wakaja kuwa marafiki wa Mwinyi, na Maadui wa Mwinyi wakawa marafiki wa Mkapa na Wapinzani wa Mkapa wakawa marafiki wa Kikwete na wapinzani wa kikwete wakawa marafiki wa JPM na wapinzani wa JPM ni marafiki wa Rais Samia

Kafulila anasema ccm in wa swap wapinzani hivyo hakuna kundi linaloitwa wapinzani tangu Nyerere mpaka Rais Samia kwani ccm ina wa swap kwa kubadilika badilika

Tujadili kwa hoja, Je ni kweli ccm ina badilika badilika kulingana na mazingira? na Je ccm is the most dynamic and Flexible part in Afrika ndio maana hakijafa kama vyama vingine barani Afrika?
 
Ukila ukishiba, matokeo yake ndio haya!
Ukweli ndio huo angalia CCM ya Magufuli na CCM ya Samia ni vitu viwili tofauti lakini chama cha CCM ni kile kile.

Kipindi cha JPM watu walisema hakuna uhuru wa habari, Wakati wa Mama kuna uhuru wa habari.

Wakati wa JK watu walisema nchi ina pesa sana na matajiri wanatamba, JPM akabana lakini CCM ni ile ile.
 
Mh. Kafulila kamaliza kila kitu hapo hakuna haja ya kuongeza kitu, huo ndio ukweli mtupu na ndio maana kipindi cha JPM baadhi ya wapinzani walibadilika na kuhamia ccm na kubezwa kuwa wamenunuliwa ila mimi na amini walihama kwa kupendezwa na sera m za ccm za wakati huo hasa ile ya kupambana na rushwa. Ukitaka kujua hilo angalia aina ya wapinzani waliohamia ccm kipindi kile.

CCM ni wajanja sana na wanaakili kubwa mno upinzani hawalijui hili wao ni kama hawana pakushikia, wakistick kwenye sera fulani anakuja kiongozi wa ccm anapita nayo tena anaitekeleza kwa kasi upinzani wanabaki watupu wanaanza kumchukia na kumzushia, ccm wakigundua hila zao wanamleta kiongozi mwingine anakuja anawaponya majeraha yao upinzani wanasahau kuwa adui yao ni ccm wanahama tena kwenye mstari wanacheza na beat la kiongizi mpya.

Ili upinzani waweze angalau kushindana na ccm ni vyema wakastick kwenye sera zao na adui yao mkubwa awe ccm na siyo yule aliyekalia kiti cha urais maana yule atapita na ccm itaendelea kuwepo. Ni lazima wapandikize imani yao kwa wananchi ili hata ikifika kipindi cha uchaguzi wananchi waseme nachagua upinzani kwa sababu ya ABC siyo kwa sababu naichukia ccm au kiongozi aliyopo. Na akitokea kiongozi wa ccm anatekeleza sera zao sio waanze kumwambia a nguvu ya soda itafika mahali atachoka wanapaswa kumkazia kuwa tunaka zaidi ya hapo ili wananchi waone kuwa kumbe wapinzani tungewapa wangefanya zaidi ya huyu.

Nitatolea mfano ununuzi wa ndege tunafahamu ya kuwa upinzani ndio ulikuwa unalalamika bungeni kuwa sisi Tanzania hatuna ndege tunazidiwa hata na Rwanda. Alipokuja JPM ziara yake ya kwanza alienda Rwanda na aliporudi tukaona anaanza kununua ndege, wapinzani wakaanza kusema ndege sio kipaumbeke chetu mara ndege zenyewe mtumba maraa oooh kwa nini tununue ndege kwa cash wakati nchi yetu ni masikini.

Kwa upinzani wenye mpango wa kushika dola tulitegemea kwanza wangempongeza JPM kwa kuchukua sera yao na kuthubutu, kisha wangemtwishwa mzigo kwa kumwambia ndege ulizonunua ni chache au ni model ya zamani sisi tungenunua nyingi na kubwa na tungejenga viwanja kila mkoa na kununua ndege za bei nafuu ambazo, zingesafurisha raia wa daraja la chini kwenda mikoani kwa bei poa. Hapo wangeweza kueleweka kwa wananchi hata kama wangekuwa wanaongopa hii ingefanya wananchi waone kumbe tungechagua upinzani tungefanyiwa makubwa zaidi ya haya tunayofanyiwa sasa.
 
Kupambana na rushwa?
 
Back
Top Bottom