David kafulila anastahili pongezi!

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
2,000
It is dangerous to be right when the government is wrong!Nimejikuta nakumbuka maneno hayo wakati nikikumbuka mapambano ya Kafulila sakata la Escrow!Lakini pia nikakumbuka Theodore Roosevelt aliyesema "Patriotism means to stand with the country,it does not mean to stand with the president"

Wakati wa sakata la Escrow,Kafulila aliweka maisha yake on a line kutetea maslahi ya nchi,hata pale ambapo Rais na serikali ya wakati huo walipokuwa against hoja zake!Aliishia kukejeliwa na mpaka kuitwa tumbili bungeni kwa kutetea maslahi ya wananchi!Ni watu wachache sana wanaweza jua hatari unayoweza kukutana nayo unapokiwa peke yako unapambania jambo lenye maslahi ya wananchi dhidi ya wenye nguvu!Kafulila hakutetereka wala kurudi nyuma kimsimamo!

Ccm na serikali wakaamua kwa namna yoyote ile,mbunge huyo hatarudi bungeni!Tuliokuwa kigoma tunajua mkurugenzi na Tume walivyomnyima ushindi wa wazi Kafulila,hii yote ilikuwa ni malipo sakata la Escrow!

Miaka miwili baadaye tunarudi pale pale,this time wanaopata credit ni watu wengine huku jemedari akisahaulika!Heshima kwako kafulila na hongera sana kwa kutetea nchi yako!Nikiangalia video hii,nakumbuka uzalendo wako!
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
12,148
2,000
Published on 20 Jun 2017
David Kafulila: anasimulia historia ya sakata la ESCROW ilipoanzia baada ya magazeti kuwa mstari wa mbele kuiibua na kisha David Kafulila kuombwa kulipeleka Bungeni. Anaelezea vyanzo vya nyaraka alizopewa vilizofikia 604 ili kuweza kuwashilisha ushahidi huo bungeni. Alipewa nyaraka hizo toka kila sehemu ikiwemo wabunge wa CCM n.k

Pia David Kafulila anachambua umuhimu wa Tanzania kuwa na mfumo/mifumo na taasisi pamoja na wafanyakazi wenye elimu ya kutosha kuendesha (capacity building) mifumo ya kuidhibiti serikali na watendaji wake kimaadili, kusaini wa mikataba ya kimataifa na utawala bora. Amegusia pia uendeshaji wa Bunge na Spika pamoja na wenyeviti wa Bunge kuwa na uwezo wa kusimamia wabunge na Bunge kwa kufuata kanuni na taratibu za haki.

KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Kafulila amesema anaunga mkono hatua zote zinazochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli juu vita ya ufisadi uliofanyika ikiwemo sakata la wizi wa fedha za umma, kupitia akaunti ya Tegeta Escrow na madini yanayosafirishwa ndani ya mchanga (makinikia).

Source: Global TV Online
 

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
2,000
Published on 20 Jun 2017
David Kafulila: anasimulia historia ya sakata la ESCROW ilipoanzia baada ya magazeti kuwa mstari wa mbele kuiibua na kisha David Kafulila kuombwa kulipeleka Bungeni. Anaelezea vyanzo vya nyaraka alizopewa vilizofikia 604 ili kuweza kuwashilisha ushahidi huo bungeni. Alipewa nyaraka hizo toka kila sehemu ikiwemo wabunge wa CCM n.k KADA maarufu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), David Kafulila amesema anaunga mkono hatua zote zinazochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli juu vita ya ufisadi uliofanyika ikiwemo sakata la wizi wa fedha za umma, kupitia akaunti ya Tegeta Escrow na madini yanayosafirishwa ndani ya mchanga (makinikia).

Source: Global TV Online
True definition of patriotism
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,226
2,000
Yes acha wapewe hongera na ni Rais wetu, yeye aliyaona hayo na sasa anayashughulikia akiwa Mkulu.

Kafulila angepiga hatua hata kuendelea baada ya kutemwa, basi naye tungempa hongera. Ila alinyamaza au sio? Kutokuwa bungeni hakumkatazi mtu kupigania anachoaminia tena awamu hii angekuwa huru sanaaaa kufanya hayo.

Kwa sasa atulie na wewe utulie, aliyoyajua wengi waliyajua pia sio kwamba ilikuwa breaking news.
 

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,434
2,000
Kwenye sakata hili wapiganaji walikuwa wengi, hata wabunge wa ccm walikuwemo. Mchango wa kafulila ulikuwa mkubwa na anastahili pongezi za watanzania wote bila kujali itikadi za kichama.
Lakini pls tusiwasahau wote wale waliochangia
 

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
2,000
Yes acha wapewe hongera na ni Rais wetu, yeye aliyaona hayo na sasa anayashughulikia akiwa Mkulu.

Kafulila angepiga hatua hata kuendelea baada ya kutemwa, basi naye tungempa hongera. Ila alinyamaza au sio? Kutokuwa bungeni hakumkatazi mtu kupigania anachoaminia tena awamu hii angekuwa huru sanaaaa kufanya hayo.

Kwa sasa atulie na wewe utulie, aliyoyajua wengi waliyajua pia sio kwamba ilikuwa breaking news.

Hii yote ni kutaka kutotambua mchango wako!Kwani unadhani ccm hawajui ufisadi uliofanyika,wanajua sana!Ila wa kuzungumza ni nani?Wengine kwa kuogopa,wakawa wanawapa siri wapinzani!It takes courage kufanya aliyofanya Kafulila!Hongera kwake!
 

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
2,000
Kwenye sakata hili wapiganaji walikuwa wengi, hata wabunge wa ccm walikuwemo. Mchango wa kafulila ulikuwa mkubwa na anastahili pongezi za watanzania wote bila kujali itikadi za kichama.
Lakini pls tusiwasahau wote wale waliochangia
Yes ni kweli,ila nimelazimika kumuandika Kafulila leo baada ya kukumbuka alivyodharauliwa na kuzomewa mpaka kuitwa Tumbili!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom