Kufuatia tuhuma zilizoibuliwa na mbunge wa kigoma kusini dhidi ya wabunge watatu kuomba rushwa kutoka halmashauri ya Tanga sasa spika Anne Makinda yuko mbioni kuunda kamati kuwachunguza. Wabunge wanaotuhumiwa ni Geofrey Zambi, Omari Badwel na Zabein Mhita wote ni wa CCM. Habari kutoka Dodoma zinadai kuwa kafulila alitoa shutuma hizo wakati akichangia hotuba ya bajeti ya serikali bungeni Dodoma. Iwapo kamati hiyo itaundwa litakuwa pigo lingine kwa makada hao wa CCM .
CHANZO GAZETI LA DIRA LA LEO