David Cameron Amkwepa (Waziri wa Mambo ya Nje Wa Tanzania) Amelazimika Kukutana na William Hague | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

David Cameron Amkwepa (Waziri wa Mambo ya Nje Wa Tanzania) Amelazimika Kukutana na William Hague

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muke Ya Muzungu, Feb 23, 2012.

 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Wazri mkuu wa uingereza amkacha JK na kumuacha William Hague waziri wa mambo ya nje ndo akutane na JK...Inaonyesha Waingereza nao wamechoka na safari zake....Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kazi kweli kweli. Heri ingekuwa Mwai kibai mwenye majeshi yake Somalia, wana Ethiopia eritrea na Uganda..sasa Jk jamani nin ilimlazimu kwenda? Membe asingeweza hizi kazi? Kwa maana kazi zote za membe Jk kaingilia !...........Pengine Cameron amemkwepa kuepuka moto na wabunge wake akiogopa kukutana na mkuu wa nchi iliyoiletea nchi yake scandal ya Rada za B.A.E
  [​IMG]
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Uuuh!
  Aibu kubwa!..Mwanzo wa mwaka 80 nilipata kusoma kitabu cha hadithi za Someni bila shida chenye shairi hili:

  1.Mgeni siku ya kwanza ,
  Mpe mchele na Panza
  Mtilie kifuuni
  Mkaribishe mgeni!

  2.Mgeni siku ya pili
  Pika wali wa Samli
  Mpekee chumbani,
  Apewe yeye mgeni.

  Mashairi haya yanamvumilia mgeni hadi siku ya tatu, lakini siku ya NNE mgeni si mgeni, anatakiwa apewe JEMBE akalime....ndiyo haya yanayompata JK!
   
 3. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Mbona hiyo picha anaonekana kama vile anaomba hela?
   
 4. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmm kweli mkuu hali mpaya sasa ni muda wa kupumzika, next time atapewa Mkuu wa Wilaya, tatizo lake muda wote akienda kwy izo meeting anapitisha bakuli. wamemchoka sasa, Mkuu pumzika punguza mitoko:A S embarassed:
   
 5. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Mimi simkubali Kikwete kabisa na kama walivyo Watanzania wengi ninachukizwa na tabia yake ya uzururaji, lakini sikubaliani na mleta mada kuwa David Cameron amemkacha. Kulingana na taratibu za kiitifaki siyo lazima rais wa nchi fulani akienda mfano Uingereza akutane na waziri mkuu.

  Kama ni "state visit", basi rais anayekwenda anakuwa mgeni wa malkia kwa sababu malkia ni "head of state". Kama ni "official visit", basi anakuwa mgeni wa waziri mkuu David Cameron, lakini kama ni "working visit" kama ambavyo ziara hii ilitangazwa, basi anakutana na waziri anayehusiana na shughuli iliyompeleka.

  Mpangilio huu unasababisha thread hii ikoshe mashiko kidogo.

  Ni hayo tu.
   
 6. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #6
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Wameshamchoka kila siku hodi na bakuli mkononi hata mimi mgeni wa hivyo namkimbia.
   
 7. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #7
  Feb 23, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Taifa liliomba Rais, tukapewa Kikwete!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kawaida kwa Nchi za Magharibi anapokelewa kwanza na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje halafu anakwenda kukutana na Waziri Mkuu au Rais hiyo ndiyo protocol yao.

  TUNA GAS; WATATUTAFUTA KWELI
   
 9. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #9
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Yaani ndugu yangu umetuona sisi mazuzu kweli kweli tusiojua lolote...dah!
   
 10. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #10
  Feb 23, 2012
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mkutano ni kesho na ndio utaongozwa na PM Cameron. Ni kawaida kukutana na waziri wa mambo ya nchi za nje kabla ya main conference.
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Nilivyosema Ni Vigumu kwa Sasa Wazungu kumkimbia Rolling Stone Kikwete... Wameonana

  [​IMG]
   
 12. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #12
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ndugu yangu, hizo ndizo Protocol za Nchi Za Magharibi Foreign Minister ndiye anayeieleze Siasa na Uchumi wa Nchi hiyo na Sio Rais wa Nchi kama Sisi ...
   
 13. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #13
  Feb 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,068
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  mkuu badilisha heading. kama vile imekosewa. sema rais kikwete sio waziri wa mambo ya nje. au ulimaanisha jk ndo waziri wa mambo ya nje?
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Feb 23, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Hivi unapata faida gani kutudangaya


  [​IMG]

  Rais Jakaya Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron walipokutana mjini Davos pembeni mwa Kongamano la Uchumi la Dunia jana Januari 26, 2012. Picha na Ikulu
   
 15. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #15
  Feb 23, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Maskini hamjui hata mnachokiandika, ili mradi roho zinawauma kwa jina tu la Kikwete, kila afanyalo, kwenu ni muhali. Poleni sana, nawasikitikia bado mna miaka 3 ya kulalama baada ya hapo mna zee la ma-mvi. MMasai yule, utani kwake unaishia mwisho wa fimbo yake, shauri lenu, mtakuja kuiona JF chungu.
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Feb 23, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Amealikwa na Viongozi wengine wa Africa kama Rais wa Ushelisheli na David Cameroon... Hiyo picha ni ya Zamani lakini nina Maanisha Wamekutana na wanajadiliana kuhusu Somalia... Ni kweli ziara ya kikazi
   
 17. j

  junior05 Senior Member

  #17
  Feb 23, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu maelezo mazuri kabisa lakini membe si kwamba alistahili kukutana na huyo waziri husika
   
 18. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #18
  Feb 23, 2012
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  ni vema kujua au kufanya tafiti kabla haujachangia najua kabla hajarudi mtakuwa mmejiridhisha
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Tena anatuombea sisi hizo hela!!! Duuh
   
 20. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Zingine ni ziara za nini? maana zimefanyika ziara nyingi mpaka zinachanganya. Siku hizi tumeamua kuongezea neno "ziara za kikazi" maana zingine hazijulikani zilikuwa ni za kufanya nini!
   
Loading...