Daudi Mwakawago afariki Dunia

Status
Not open for further replies.

Sir Leem

JF-Expert Member
Mar 14, 2008
581
122
mwakawago.jpg


Mwanasiasa Mkongwe nchini Balozi Daudi Mwakawago amefariki dunia Jijini Dar e salaam.

Mwakawago alipata kushika nyadhifa mabli mbali za Kiasiasa nchini, Ubunge Iringa Mjini, Uwaziri, Balozi wa Kudumu UN
Balozi Mwakawago amepata kushika nyadhifa mbalimbali za kisiasa na kiserikali enzi ya uhai wake, zikiwemo za kimataifa.

Amepata kuwa mbunge wa Iringa Mjini kwa miaka mingi, Waziri katika Serikali ya Awamu ya Kwanza nay a Pili pamoja na kuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kabla ya kumpisha Balozi Augustine Mahiga anayeshikilia wadhifa huo hadi sasa.

Mwakawago alizaliwa mkoani Iringa mwaka 1939 na kupata elimu katika vyuo vikuu tofauti vya ndani na nje ya nchi vikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Makerere cha Uganda na Manchester cha Uingereza.

Baada ya kumaliza masomo yake Makerere, Balozi Mwakawago alikwenda kufanya kazi ya ualimu katika kilichokuwa Chuo cha Itikadi cha Chama cha Mapinduzi, Kivukoni na baadaye kuwa mkuu wa chuo hicho ambacho sasa kinaitwa Chuo cha Sayansi ya Jamii Kivukoni.

Aidha, Balozi Mwakawago amepata kushika nyadhifa kadhaa za kisiasa kwa miaka 20, akiwakilisha asasi tofauti zikiwemo za vyuo vikuu, vyama vya wafanyakazi na katika jimbo lake la uchaguzi la Iringa.

Serikalini, Balozi Mwakawago alishika nafasi mbalimbali ikiwemo ya uwaziri katika wizara mbalimbali ambazo ni Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni; Wizara ya Kazi; Wizara ya Utumishi, pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara.

Mwaka 1980 hadi 1982, Balozi Mwakawago aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Paul Mhaiki (sasa marehemu), baadaye akateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia kuanzia mwaka 1991 hadi 1993.

Utumishi wake haukukomea hapo, kwani mwaka 1994 hadi 2003 alikuwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na baadaye akawa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sierra Leone kutoka mwaka 2004 hadi 2005.

Pamoja na kustaafu, Umoja wa Mataifa umekuwa ukimtumia kama mmoja wa wakufunzi wake katika kutoa mafunzo kwa viongozi wa baadaye katika umoja huo.

Aidha, amekuwa akishughulika na asasi ya kimataifa isiyokuwa ya kiserikali ya Miracle Corners of the World (MCW) yenye maskani yake nchini Marekani, ambapo kupitia asasi hiyo alikuwa akishughulikia uongozi wa vijana kidunia katika maeneo yenye matatizo ya kisiasa kama Mashariki ya Kati na katika nchi zilizopita katika migogoro ya kivita.

Balozi Mwakawago alikuwa mzalendo wa kweli, na hivi karibuni alikuwa akichangia mijadala na kuelezea kuhusu maadili ya uongozi, huku akipinga tabia ya ufisadi ya baadhi ya viongozi ambayo imeifanya serikali ionekane haifai.
 
RIP Mwakawago. Poleni wafiwa wote. Mungu awafariji katika wakati huu wa msiba.
 
Mwanasiasa Mkongwe nchini Balozi Daudi Mwakawago amefariki dunia Jijini Dar e salaam
Mwakawago alipata kushika nyadhifa mabli mbali za Kiasiasa nchini,Ubunge Iringa Mjini,Uwaziri,Balozi wa Kudumu UN

Alikuwepo? Siku hizi nimeshasahau nani yupo na nani kashaondoka!
 
Mwanasiasa Mkongwe nchini Balozi Daudi Mwakawago amefariki dunia Jijini Dar e salaam.

Mwakawago alipata kushika nyadhifa mabli mbali za Kiasiasa nchini, Ubunge Iringa Mjini, Uwaziri, Balozi wa Kudumu UN
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala pema peponi.Ameni
 
RIP mzee wetu mwakawago,nakumbuka alitoa mchango mzuri kwenye kongamano la mwalimu Nyerere foundtion lililofanyika mwishoni mwa mwaka jana amabalo viongozi wetu wengi walilibeza sana.
 
Du! hata mimi nilimshuhudia star tv kwenye kipindi cha Mary rose Talk show,akiongelea kuhusu maadili.Alitoa ujumbe mzito kuhusu mafisadi na wezi wa raslimali za taifa.PUMZIKA MZEE!!!!!!!!!!!!
 
Tulifahamiana na Daudi Mwakawago na alikuwa Mzalendo wa kweli. Nilifurahia sana mijadala tulioshiriki pamoja.

Poleni wote wafiwa. Mungu awafariji na kuwaimarisha wakati huu mgumu.

Roho ya marehemu ipumzike mahala pema milele. AMEN.
 
- Ni jana tu nilipata info kwamba amepelekwa Nairobi ghafla, loh! Mungu amuweke pema, aliwahi kuwa jirani yangu nikiwa mtoto na mama yangu mzazi alikuwa secretary wake wa muda mrefu sana enzi hizo akiwa Mkuu wa Chuo Cha Kivukoni College kabla hakijawa cha CCM, na later in life he became my close friend, lakini as a political leader nitasema hukumu yangu later kwa sasa ngoja nimkumbuke kwanza he was a good man at heart!

- Salam zangu za rambi rambi kwa familia nzima Wakuu Kiye, Lulu, Tagge, Imani na Patrim, pamoja na mama, Mungu awape nguvu na busara katika hiki kipindi kigumu sana kwenu na sisi wote tuliomjua marehemu kwa karibu, poleni sana na tupo wote.

- Bwana ametoa na pia ametwaa, kazi ya Mungu haina makosa.

Respect.


FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom