Daudi anao watu wake Bwana!

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,834
155,782
Am I a sadist? No, I am not.

Juzi basi na mimi in the middle of nowhere nikajikuta nasherehekea Sikukuu ya Uhuru sijui Mapinduzi iliyofanyikia huko Kigamboni. Cha ajabu mambo ya huko wala hayanihusu, kimbelembele tu. Basi unajua furaha ikikuzidia, rahisi sana kukosa umakini.

Si na mimi natumiwa mavideo, nayaangalia, nacheka afu nayasambaza. Kuanzia za kujitilisha huruma, za kucheka na hata za kuweka mkwara. Asubuhi naona namba ngeni inanipigia Wosapu. Kwa kawaida spokeagi namba nsoijua. Kuingia kwenye Kundi Sogozi ambalo mimi ni Mgeni mwalikwa, nakuta watu wananijadili. Pamoja na ile namba ilonipigia.

Naulizwa vidio nilizorusha zinahusiana vipi na lile kundi Sogozi?
Nikakumbuka mule mi ni minority, nimealikwa tu. Zaidi ya Admin hakuna ninayejuana naye personally. Ndo nagutuka, kumbe usiku uliopita niliwehukwa na mambo za social media.

Nilipoteza umakini. Nikaomba radhi ili yeshe. Cse kiukweli hakuna sheria nimevunja, hakuna siku tuliwahi kupangiwa cha kupost, tunapost kuhusu mpira, tunapost kuhusu vibonzo na mambo mengine mengi. In fact hata yule jamaa anayefaidika na jina la Mwalimu Nyerere tulimpost alipopata habari zake toka kwa wala Dogs. Anyways, mtoto wa kambo hadeki. Nikaomba radhi. Admin akawahi kuitikia, akasema umesamehewa ila usirudie tena.

Kanuni mpya ikatungwa, marafuku kupost mambo ya siasa au jambo linalomuhusu mtu directly. Nikabaki najiuliza, unatuhumiwa vipi kwanza halafu ndo kanuni/sheria inatungwa. Wanasheria husema chochote ambacho hakijakatazwa basi kimeruhusiwa.

Nikahamisha mjadala chemba kwa Admin, kwa kuwa huyu ndo mwenyeji wangu. Nikaomba radhi tena, skulenga kumchafulia kundi lake. Akaniambia nisijali, pia nilitumia hekima sana kuwaomba radhi. Ndo akaning'ata skio!

Kumbe yule aliyekerwa ni best friend wa Toto Pendwa. Wanasema Toto Baya, Zuri kwa Mama ake. Naam, wapo wanaomtetea. Tena kwa nguvu zote. We all need such loyal friends, no matter what, they will stand with or for you. Daudi anao watu wake Bwana!

©®Alex Mayunga
 
Usiyempenda wewe amini kunawanao m

Jitu zima wivu wivu tu,
Sidhani Kama Kaka DAUDI BASHITE anachukiwa. Wanadaslamu wanapenda Sana, ila yeye alikosa upendo kwa watu wake.
Aliwateka, aliwasweka Ndani, aliwapora magari yao, aliwasingizia kuuza madawa ya kulevya na udhalimu mwingi aliwafanyia.
Ndio maana anguko lake kule pantonini liliwafurahisha wengi.
Tunaamini atarudi kuwa mtu mwema sasa
 
Kwenye ka group ketu nilikuwa nashangaa tu kuona clip za manju na gwiji wa mziki Afrika Mbaraka Mwinshee na kundi la Moro Jazz wakitoa burudani ya kibao chao moto moto kinachokwenda kwa jina la Jogoo wa Shamba.
 
Naamini kumbe Pompeo alikuwa na ushahidi wa kutosha kabisa
Hao wanaomtetea bado wanaamini baba yake atampitisha na hasipomtisha ataendelea na ile kazi yake ya Chief In charge wa Watu wasiojulikana aka kundi LA kuteka,kutesa na kuua watu.
 
Back
Top Bottom