Elections 2010 Database ya NEC kwa ajili ya kupiga kura hivi haiwezekani?

Wa Ndima

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
1,526
323
View attachment 15693
Hapa ningependa kuzungumzia kutengenezwa kwa Database kwa ajili ya wapiga kura.

Kwa mawazo yangu kwa wale ambao wako nje ya vituo vyao vya kupiga kura ingetengenezwa Database ambayo ingemuwezesha mtu yoyote kupiga kura akiwa kokote ndani ya Tanzania
kuchagua kiongozi wa jimbo lake, Diwani, Mbunge na Raiskwa kutumia Database hiyo ambayo itaonesha mtu kapigia kura kituo gani katika Tanzania.

Kila kituo kingekuwa na Laptop iliyounganishwa na Wireless internet kwa ajili ya kuhakiki kama mpiga kura huyo yupo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga kura, amejiandikisha kituo gani na kama tayari ameshapiga kura ama la. Hivi hili haliwezekani?

Ni mawazo tu!
 
Lina wezekana sana , mbona bank linawezeka kwamfano ukachukua fedha kwenye tawi A , ukienda tawi B utaonekana ulichukua fedha kwenye tawi A , muda, saa na jina la cashier au namba ya ATM iliyokupa pesa
 
Ila kuna jambo hapa NEC wananishangaza, kuna mtu hapa alipoteza kadi ilipokuja muda wa kurekebisha kwa wale waliopoteza akatengeneza mpya. Hivi juzijuzi wakati anafanya usafi akaiona kadi iliyopotea hapo mwanzo.

Sasa inshu ni kuwa kadi zote mbili zipo ACTIVE kwa jinsi tulivyoangalia hapa kwenye Website ya NEC. Je hii haiwezi kusababisha watu kupiga kura mara mbili. Na je huu sio mpango wa NEC kuiba kura? Nadhani CCM wanaweza kuutumia ujanja huu. Nashauri CHADEMA wafuatilie hili.

Nimemwambia jamaa kesho akaangalie jina lake kama lipo kwenye kituo kile cha kwanza alichojiandikisha kisha kadi ikapotea.

TAFAKARI!
 
lina wezekana sana , mbona bank linawezeka kwamfano ukachukua fedha kwenye tawi a , ukienda tawi b utaonekana ulichukua fedha kwenye tawi a , muda, saa na jina la cashier au namba ya atm iliyokupa pesa

kwa teknologia ya siku hizi mbona hiyo simple tu!!!!
 
Database inawezekana kuwa kwenye mtandao, uwezo wa kufanya hivyo Tz gov inao' wataalamu wapo, fedha zipo ILA WANAOGOPA TRANSPAReNCY.

Kama taasisi ndogo kuliko benki kama "vodacom" imeweza via m-pesa na benki zote JE SERIKALI INAYOWAMILIKI WOTE HAO PLUS MALI ZOTE ISHINDWE? Kuna dondoo iliyojificha kwenye hili.

Mtandao huo Si tu ungehisisha kupata tu database info ila hata MATOKEO YANGETOKA FASTA.
 
Database inawezekana kuwa kwenye mtandao, uwezo wa kufanya hivyo Tz gov inao' wataalamu wapo, fedha zipo ILA WANAOGOPA TRANSPAReNCY.

Kama taasisi ndogo kuliko benki kama "vodacom" imeweza via m-pesa na benki zote JE SERIKALI INAYOWAMILIKI WOTE HAO PLUS MALI ZOTE ISHINDWE? Kuna dondoo iliyojificha kwenye hili.

Mtandao huo Si tu ungehisisha kupata tu database info ila hata MATOKEO YANGETOKA FASTA.

Hapo umenena, vipi kuhusu hili la Majina kujirudia vituo tofauti?
 
Back
Top Bottom