Doncy monco
Member
- Jul 26, 2019
- 38
- 101
Uongozi wa Serikali ya wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO), wamejibu tuhuma zilizotolewa na Mhadhiri wa chuo hicho Kitivo cha Sanaa ya ubunifu Dkt. Vicensia Shule, kuhusu uwepo wa baadhi ya wanafunzi wachafu na hawajui kuoga.
Rais wa DARUSO Hamis Musa, amesema kuwa kauli hiyo imewapa doa na kuwashushia hadhi wanafunzi kwa sababu kitendo cha kumwambia mwanafunzi wa chuo ananuka ni cha fedheha lakini licha ya uwepo mijadala mbalimbali baada ya kauli hiyo kutolewa lakini wanafunzi walielewa kwa sababu wao si wachafu.
''Ni kweli hiyo kauli Dkt Shule aliitoa, sijajua aliitoa kwa mlengo gani, lakini sisi kama Serikali ya wanafunzi hatujaipokea kwa mlengo mzuri kwa sababu inalengo la kutushushia hadhi sisi wanafunzi, unapomuambia mwanafunzi wa chuo haogi sidhani kama ni kitu kizuri'' amesema Rais wa DARUSO.
Aidha Rais huyo wa DARUSO akizungumzia suala la malezi katika familia, ametoa rai kwa wazazi kuwafundisha watoto masuala ya usafi ili wakikua waweze kujitegemea wenyewe na si kuwaachia wafanyakazi wa ndani kuwafanyia kila kitu.
Kujua zaidi jinsi Dr.Shule alivyowaponda wanafunzi kwamba wananuka, soma

Mhadhiri UDSM, Vicensia Shule: Wanafunzi wengi ninapofundisha hawajui kuoga
Mimi nafundisha pale chuoni asilimia kubwa ya wanafunzi hawajui kuoga, nafundisha masomo ya kuigiza pale mwanafunzi utakuta ananuka mpaka aibu. Dkt. Shule alishawahi kuwatetea mabinti vyuoni wanaoombwa rushwa ya ngono na wahadhiri Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Soma Mhadhiri Vicensia Shule...
www.jamiiforums.com