DART wameomba SUMATRA nauli ziwe kati ya 1,200 - 1,400

kama huwezi, nunua gari yako uendeshe mwenyewe wese alfu 20 kila siku kwenda na kurudi kazini ndio utapata akili. mbona bia mnanunua alfu mbili mia tano moja, na mnakunywa hadi kumi, iweje mtu akubebe kwenye gari yake toka mbaali huko hadi posta kwa buku mia nne unaona garama? hiyo nauli ni sawa tu na nusu ya bei ya bia mnazobwia. pengine ndio mtapunguza na kulewa sana ili mbane hela kwaajili ya nauli. alaa

na ndo maana wengine tunakunywa gongo.... glass ndogo mia 4 na unalewa bwiiiiii
 
Kwa maoni yangu hiyo nauli ni ndogo watapata hasara, wangefanya japo 7,000 kwa watu wazima na 4,000 kwa wanafunzi
 
hao wanaolalamika ni wachache sana. wewe ukiona unachelewa kwenda kazini na hauna gari, nakuapia hata wangesema buku tano utapanda tu. mbona kuna kuwa na foleni hapo watu tunaogopa kuchelewa ofisini tunapanda bodaboda hadi posta kwa alfu kumi? everyday....kama unafikiri hiyo nauli ni kubwa sana, waulize bodaboda.
Acha upuuzi wewe.. Ndio maana huu mradi unatakiwa kua hudima na sio biashara, usijiangalie uwezo wako ukadhani wote wanaweza kumudu hiyo gharama, tatizo mmezoea kuiba iba kwenye ofisi za uma mnafikiri kila mtu mwizi.. Kwa nini dala dala za watu binafsi zicharge 600 kwa sasa halafu DART ambayo ni ya public itoze 1400? Labda tuangalie uwezo wa watanzania.. Unajua kima cha chini ni shs ngapi kwa sasa?
 
MBEZI POSTA KARIAKOO 700

SASA KMR KRKOO 600 LEO BILA HAYA 1200

MBEZI POSTA KRKOO ATI 1400. SHAME N U ALL

KILA ANAEENDA MJINI ASIPUNGUE NA 6000 USINIULIZE ANAKULA WAPII
Wacha wakome si walichagua sisiem....
 
hiyo ni nauli reasonable kabisa kwa mfanyakazi wa kawaida. mtu wa hali ya chini kabisa anaweza. wewe unapofikiri hawawezi, kuna watu hapo ubungo utakuta taxi zimepaki buku mbili hadi posta zinasanya kila siku na watu wanapanda. noah pia zinashanya sana kutoka kariakoo hadi mbezi alfu tatu. kuunganisha magari kumaliza alfu mbili au tatu ni kitu cha kawaida. hayo mabasi ni ya garama, hayajaokotwa, na si ya babu yako, ukitaka kizuri lazima ukigarimie, ulitaka wawatoze mia tano halafu wapate wapi faida ili wa maintain hayo magari na kununua mengine mapya? na zaidi ya yote kuna muda kampuni hiyo itakuwa listed DSE ili ununue hisa na wewe umiliki. na wakitoza hiyo ndio mtapata na akili ya kufanya kazi mtafute hela muache uvivu. mtu mchapakazi hawezi kusema anakosa hiyo hela kwa siku moja. acheni utani.
***** wewe
 
Mkuu hii public transport (serikali inapohusika) inatakiwa kuwa ni service na sio profit making.., na hapa anayeangaliwa na mwananchi mwenye kipato cha chini kabisa, kwahio kama magari private yanabanwa na kupangiwa nauli ndogo iweje hii ambayo kuna mkono wa serikali inapata guts za kuleta huu utani wa kuomba pesa kubwa zaidi ?
 
Jamaa washanza kuviharibu tayari! Vituo hivi vimeinuliwa sana sijui huyu dereva amefikaje huko?

New+Document.jpg
 
Ndugu Hute, kuna mahali naona sijaeleweka vizuri ,naomba nitoe ufafanuzi.
Kila mtu anapenda kusafiri kwa raha ,tatizo ni kipato cha walio wengi siyo kikubwa kama unavyofikiria. Jaribu kupiga hiyo gharama ya nauli kwa mwezi mmoja tu, linganisha na mishahara ama kipato cha wengi wapanda daladala. utaona kama pesa kubwa itaishia kwenye nauli tu.
Kusimama huku ukinusa vikwapa vya abiria wenzio ni kero ila ni shida ndiyo inayoleta uvumilivu. Wajaribu kupanga nauli zilizo chini ya hapo. Watatue tatizo la usafiri huku wakiangalia na vipato vya wananchi walio wengi. Kupanda daladala ni shida tu , kila mtu angependa amiliki gari yake ili asafiri kwa raha tatizo kubwa ni KIPATO kidogo kwa tulio wengi.

Au mwenzangu ni mdau kwenye huo mradi mbona unatetea sana hizo nauli ???? !!! ha ha haaaa
Ni wakati muafaka wa watu wasio na kazi za msingi mjini kurudi vijijini waende wakalime...

Maisha hayako mijini tu, after all unatokaje kwako Mbezi mpaka Posta kila siku kama haufanyi shughuli ya kuweza kulipa hiyo nauli ya 2800?? Maisha hayako mijini tu, kule vijijini ndiko unaweza toka haraka kuliko hapa mjini kama huna kazi ya kukuwezesha kulipa nauli ya 2800..
 
Acha upuuzi wewe.. Ndio maana huu mradi unatakiwa kua hudima na sio biashara, usijiangalie uwezo wako ukadhani wote wanaweza kumudu hiyo gharama, tatizo mmezoea kuiba iba kwenye ofisi za uma mnafikiri kila mtu mwizi.. Kwa nini dala dala za watu binafsi zicharge 600 kwa sasa halafu DART ambayo ni ya public itoze 1400? Labda tuangalie uwezo wa watanzania.. Unajua kima cha chini ni shs ngapi kwa sasa?
Mkuu sana, Mbezi Posta nadhani ni 800 na si 600...

Alafu pia mwambie huyo wa Daladala gari ijazwe level seat tu asisimamishe mtu kama atakubali kulipwa hiyo 800...

Lakini pia tusikimbilie kulaumu, hatujajua utumiaji wa mafuta wa hizo gari, bei za vipuri, services, mishahara na vitu kama hivo... Labda hiyo 1400 waliyoweka ni ili DART yenyewe iweze tu kujiendesha bila kutegemea rudhuku kutoka serikalini..

ALL in ALL tusubirie mchanganuo zaidi, sidhani kama ni vizuri waweke nauli ambazo itakula kwao alafu baada ya mwaka mmoja gari zote hoi then tuanze kulaumiana... hivi ile Treni iliyokuwa inachaji 500 sijui iliishia wapi???
 
Halafu mi nilijua huu ni mrad wa serikali kumbe una wenyew makubwa.. nauli hyo ni kubwa.. 1200_1400? Kwa kipto gani nilichonacho?!..
 
Ni wakati muafaka wa watu wasio na kazi za msingi mjini kurudi vijijini waende wakalime...

Maisha hayako mijini tu, after all unatokaje kwako Mbezi mpaka Posta kila siku kama haufanyi shughuli ya kuweza kulipa hiyo nauli ya 2800?? Maisha hayako mijini tu, kule vijijini ndiko unaweza toka haraka kuliko hapa mjini kama huna kazi ya kukuwezesha kulipa nauli ya 2800..

Hmmm!! kumbuka maisha ni kama upepo leo unaweza ukawa na uwezo wa kulipa hiyo nauli ,na kesho ukajikuta hauna uwezo wa kulipa hiyo pesa. Hivi umemfikiria yule anayelipwa 150000 kwa mwezi kwenye hiyo nauli ya 2800 kwa siku hapo hajanywa hata maji achilia mbali chakula kwa mama ntilie.
Pia jifunze kutetea na wengine pindi wewe unapokuwa na uwezo huo wa kiuchumi. Naamini hiyo nauli itapunguzwa tu japo wewe unashawishi watu wasiokuwa na kipato cha kutosha 2800 kwa siku warudi kijijini. Kijijini watarudi tu ukizingatia huko ndiyo kwao ila kila mtu kaja mjini kutafuta maisha. Sasa unapopata nafasi ya kupanda juu acha tabia ya kuharibu ngazi ili wengine wasipate nafasi ya kupanda ulipo. Siku utakayohitaji kushuka utaujua umuhimu ngazi uliyoivunja kwa ubinafsi wako.

Uongozi ni sikivu hiyo nauli itashushwa tu.
 
hiyo ni nauli reasonable kabisa kwa mfanyakazi wa kawaida. mtu wa hali ya chini kabisa anaweza. wewe unapofikiri hawawezi, kuna watu hapo ubungo utakuta taxi zimepaki buku mbili hadi posta zinasanya kila siku na watu wanapanda. noah pia zinashanya sana kutoka kariakoo hadi mbezi alfu tatu. kuunganisha magari kumaliza alfu mbili au tatu ni kitu cha kawaida. hayo mabasi ni ya garama, hayajaokotwa, na si ya babu yako, ukitaka kizuri lazima ukigarimie, ulitaka wawatoze mia tano halafu wapate wapi faida ili wa maintain hayo magari na kununua mengine mapya? na zaidi ya yote kuna muda kampuni hiyo itakuwa listed DSE ili ununue hisa na wewe umiliki. na wakitoza hiyo ndio mtapata na akili ya kufanya kazi mtafute hela muache uvivu. mtu mchapakazi hawezi kusema anakosa hiyo hela kwa siku moja. acheni utani.
acha kubwia viroba wewe maana utaanza kuvua nguo muda si mrefu mbele ya kadamnasi ila usiombe Nyoso awepo maana ataku-nyoso
 
Hmmm!! kumbuka maisha ni kama upepo leo unaweza ukawa na uwezo wa kulipa hiyo nauli ,na kesho ukajikuta hauna uwezo wa kulipa hiyo pesa. Hivi umemfikiria yule anayelipwa 150000 kwa mwezi kwenye hiyo nauli ya 2800 kwa siku hapo hajanywa hata maji achilia mbali chakula kwa mama ntilie.
Pia jifunze kutetea na wengine pindi wewe unapokuwa na uwezo huo wa kiuchumi. Naamini hiyo nauli itapunguzwa tu japo wewe unashawishi watu wasiokuwa na kipato cha kutosha 2800 kwa siku warudi kijijini. Kijijini watarudi tu ukizingatia huko ndiyo kwao ila kila mtu kaja mjini kutafuta maisha. Sasa unapopata nafasi ya kupanda juu acha tabia ya kuharibu ngazi ili wengine wasipate nafasi ya kupanda ulipo. Siku utakayohitaji kushuka utaujua umuhimu ngazi uliyoivunja kwa ubinafsi wako.

Uongozi ni sikivu hiyo nauli itashushwa tu.
Ebu mkuu tuache ushabiki, kuna mtu analipwa 150,000 anafanya kazi ya ofisini Posta au Kariakoo?? Ni kazi gani hizo, labda unitajie pia, maana hata wale Office Attendants kule Posta hawalipwi hiyo pesa...

Pili, kama ndivyo, basi serikali nayo iangalie swala la kuboresha maslahi ya wafanyakazi wake... Maana huwezi weka nauli 1400 alafu bado ulipe mshahara 150,000/=... nadhani both public & private scale kima cha chini ni zaidi ya hiyo 150k
 
Wapo wengi tu wanaolipwa hivyo, pia fahamu Siyo watu wote wanaoenda kufanya kazi posta ama kariakoo wanafanya kazi serikalini. Wapo wa serikalini pia wapo wanaofanya makampuni binafsi, majumbani, ujenzini na kadhalika na hawa ndiyo ninaowatete mimi juu ya hiyo nauli..
Nakubaliana na wewe 100% hapo uliposema Serikali iangalie suala la kuboresha maslahi ya wafanyakazi wa umma na binafsi.
 
Kwenye kampuni binafsi nadhani nimekujibu, mishahara iongezwe...

Wasaidizi wa maduka kule Kariakoo wengi almost 90% maboss zao wanawapa nauli... Hapa hakuna shida..

Mfanyakazi wa ndani, nadhani unaongelea wale kwa kwenda na kurudi kule kwa wahindi... nao wapewe nauli na maboss zao...

Wajenzi, hawa nadhani waangaliwe pia, ila najua sikuhizi kwa Dar kibarua haondoki na chini ya 10,000... Sasa wale wanaojenga majengo makubwa kule mjini ni Kampuni kubwa kubwa, waone pia haja ya kuwaboreshea vibarua wao posho...
 
Safi sana, sasa haya ndiyo maneno yaliyojaa utu na kujali ndani yake. HONGERA NYINGI KWAKO.:):)
 
mfanyakazi wa ndani kwa muhindi hapati zaidi ya laki na nusu, sasa nauli pekee 72,000 hujatoa hela ya kula, sabuni, pengine ana mtoto shule, pengine kapanga, hapo hujapigia mahesabu akiumwa, shit!
Au mlinzi wa kampuni.
 
Natamani nauli ziongezwe mpaka 20000 ili watu mpungue Dar. Mje huku mnapopaita mikoani mlimeeeeeeeee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom