Darasa: Maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania ila kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,337
113,178
Wanabodi!

leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania, yaani Tanzanian National Day, na sio Tanganyika. Kumbukumbu ndio ya Uhuru wa Tanganyika lakini maadhimisho na sherehe ni ya uhuru wa Tanzania!.

Kufuatia baadhi ya watu kuwa kwenye sintofahamu ni maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika ama Tanzania?.

Hivyo nimejitolea kutoa somo hili ambalo naamini litakuwa ni very benefisho kwako.
Wanabodi, leo ni tunasherehekea miaka 60 ya uhuru wa Tanzania na sio Tanganyika, kwa sababu maandimisho ni present, kilichopo sasa!, japo ni kweli iliyopata uhuru ni Tanganyika, which doesn't exist any more, kilichopo sasa ni Tanzania, tunasherehekea uhuru wa Tanzania.

Jee wewe mkuu usomae hapa, ile siku ulipozaliwa, jee unajua ulizaliwa bila jina?, unaposherehekea siku yako ya kuzaliwa, jee unasherehekea siku ya kuzaliwa yule mtoto aliyezaliwa siku ile bila jina, au huyu aliyepo mwenye jina?!.

Na kama ni mwanamke, anakuwa na Maiden Name, akiolewa ana change name, kuasume jina la mumewe, tuseme umeolewa na Pasco, hiyo, sasa ameolewa anaitwa Mrs. Pasco, siku ya kuadhimisha birthday yako tutaadhimisha siku ya kuzaliwa ya Mrs. Pasco, sio binti fulani wala ya yule mtoto asiye na jina!.

Tanganyika was an area with a Name Tanganyika. Now that name doesn't exist any more, kilichopo sasa ni Tanzania Bara, na eneo la ilipokuwa Tanganyika ndio eneo la Tanzania bara!.

Hivyo leo kumbukumbu ni ya uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho na kusherehekea ni uhuru wa Tanzania Bara kwa kifupi Tanzania

Pasco.
Wajameni ni katika kukumbushana tuu kuwa maadhimisho ya leo ni ya Uhuru wa Tanzania, na sio wa Tanganyika!.
Nawatakia sikukuu njema ya Uhuru na Jamhuri.
Paskali

Update;
Kiukweli humu jf, tuna vilaza wengi kuliko tunavyo jidhania!. Watu ni wazito kuelewa mpaka basi!.
What's wrong with you Pascal Mayalla ..?
Kwa sbb iko very clear kuwa, tarehe 9/12 kila mwaka ni kumbukumbu ya Uhuru wa nchi inayoitwa TANGANYIKA na siyo TANZANIA maana hiyo haipo na haikuwepo mwaka 1961....!

Kwa kifupi hujaeleweka na sijui kama utaeleweka hata ukiendelea kujitetea...!!
Mkuu Mti wa Muwese, The Palm Tree , huu ndio uelewa wa baadhi ya Watanzania, wewe ukiwemo, halafu mkiambiwa ukweli mna uwezo finyu wa uelewa, mnakasirika.

You are absolutely right, kumbukumbu ni za uhuru wa nchi iliyokuwa Tanganyika, lakini maadhimisho ni maadhimisho ya uhuru wa Tanzania!.

Kuna mambo mawili.
1. Kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika.
2. Maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania ambayo hapo zamani ilikuwa Tanganyika.

Sasa najaribu kukuelewesha kwa kutumia kiwango cha chekechea, usipoelewa sasa, utanisamehe bure.

Mfano,
  1. Kuna binti mmoja anaitwa Binti Mti wa Muwese, kila siku yake ya kuzaliwa anaisherehekea kama kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Binti Mti wa Muwese.
  2. Kila akisherehekea siku hiyo, ni sherehe za kukumbuka ile siku yake ya kuzaliwa, na anayesherehekea siku hiyo ni Binti wa Muwese.
  3. Ikatokea mimi Pasco Mayalla, nimempenda Binti Mti wa Muwese, nikamuoa, akabadili jina sasa haitwi tena Binti Mti wa Muwese, sasa anaitwa Mrs. Pasco Mayalla na nyumbani anaitwa Mama Junior, maana kanizalia kidume kinaitwa Pasco Junior.
  4. Siku ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Binti Mti wa Muwese, ila sherehe ni ya Mama Junior.
  5. Kumbukumbu ni ya kile kilichofanyika wakati kikifanyika, ni kumbukumbu ya kuzaliwa kale kachanga kalikoitwa Binti Mti wa Muwese, lakini sherehe, yaa birthday party, sio party ya binti Mti, ni party ya Mama Junior (Mrs Pasco)
Hivyo nchi iliyopata uhuru ile tarehe 9 Desemba 1961 ni Tanganyika, hivyo kumbukumbu ndio ya uhuru wa Tanganyika, lakini maadhimisho, sherehe, ni ya Tanzania, kwasababu yule Tanganyika amebadili jina na kuwa Tanzania Bara, kwa kifupi Tanzania.

P.
 
Ndio maana kuna swali nilijiuliza, hivi hii siku yetu ya uhuru na Zanzibar inasherehekewa? na kule kwao ni mapumziko kama huku bara? kama na Zanzibar wanasherehekea, vipi yale mapinduzi yao "matukufu" wanayaweka kwenye nafasi ipi?

Au ndio maana nasi huwa tunasherekea siku ya mapinduzi ya Zanzibar? kwamba tuko ndugu moja, lako langu... langu lako? anyway, hata kama ndio hivyo, sioni kosa kwanini hii siku ya uhuru isiitwe siku ya uhuru wa Tanganyika, sio Tanzania, naona iitwe hivyo hata kama itasherehekewa pande zote mbili.

Kumbe huwa kuna kosa la kiufundi linarudiwa kila mwaka kwenye maadhimisho ya hii siku, ni vyema sasa wahusika waamke.
 
Mdogo wangu Paschal nimeona unaungana na hoja ya Uhuru wa Tanzania SIYO Tanganyika. Naomba utusaidie kujua mambo yafutayo;

1. 9/12/1961 kulikuwepo na Tanzania?

2. Je Tanganyika au Tanzania Bara imewahi kubadili jina ikajiita Tanzania? If yes,lini na kwa hati gani?

3. Tukisema Uhuru wa Tanzania tunamaanisha hata Zanzibar walipata Uhuru wao 9/12/1961?

4. Kama Zanzibar inatarehe yake yakupata Uhuru ambayo naamini ni siku ya Mapinduzi, tunasemaje Tanzania ilipata Uhuru mwaka 1961 tukijua kilichopata Uhuru ni sehemu tu ya Tanzania ambayo ni Tanganyika?

5. Kwa uelewa wako Mapinduzi ya Zanzibar yanaweza kutambua kama siku ya Uhuru ya Zanzibar?

6. Hoja Yako ya kusherekea ya Sasa ( present) umeitoa kwenye nyaraka gani?

Nauliza haya baada ya kuona mada zako zote zimeacha lakuna kwenye maeneo hayo: Nikutakie siku njema ya Uhuru wa Watanganyika
 
Kuna tafsiri fulani ziko Tanzania tu huwezi kuzipata pengine duniani:

1) Maana ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
2) Uhuru wa Tanzania
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania...
Huo mfano wa kuzaliwa mtoto bila kuwa jina hauwezi kumfanya mtu kukuelewa maana sisi wengine tulipewa jina siku hiyohiyo baada ya kuzaliwa na paka sasa ndo jina langu
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania...
Sisi waTanganyika ni wanafiki Sana, tunaweza hata kujiroga wenyewe!
 
Watu mna maneno Yani mnasema kabisa eti Tanganyika kaolewa kwa Zanzibar na ndo Mana kakubali hadi kubadilisha jina lake,eti kisa kapenda hadi kafa kaoza ndo Mana kakabidhi kila kitu kwa Mme wake it means kashindwa hadi kujitawala hivo kaamua kumpa Mme wake amtawale.

Hii ni dharau kubwa maana ni zaidi ya umbumbumbu,nimeumia kwa kweli wachache wanatutawala wengi as if sisi huku Tanganyika ni mazuzu na sisi huku hatuluhusiwi kuongoza kwao ,huu ujinga ufike mwisho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Happy Birthday Tanzania.

Miaka 60 sio mchezo....tumefanya mengi mazuri na kazi bado inaendelea.

tunafahamu kuwa maendeleo sio kama vile kujaza maji kwenye ndoo......bali maendeleo ni jambo endelevu.........kazi iendeleee....
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho...

Mambo mengine ni kujiaibisha na kujishushia hadhi ya mtu kwenye jamii. Mambo mengine yako wazi na yaki kwenye kumbukumbu za maandishi na hakuna siku tuliyosikia kubadilika kwa kilichokuwepo tangu mwanzo.

Katika historia ya dunia hakuna nchi ilipata uhuru inaitwa TANZANIA.

Nchi iliyopata uhuru kwa tarehe hii na kwenye ardhi hii ni TANGANYIKA.

TANZANIA inatakiwa kusheherekewa siku ya MUUNGANO wa TANGANYIKA na ZANZIBAR.

Tusiyumbishwe na hulka zetu na kuoneana aibu. Kama kuna ushahidi dhidi ya hayo hapo juu yalete.

Hata wenzio wanakushangaa😂👇

20211209_091829.png
 
Happy Birth day Tanzania, 60 yrs.
Tumepiga hatua kubwa sana ktk nyanja zote;

1. Elimu=Elimu bure kuanzia primary hadi kidato cha 4, hivyo sasa watoto wengi wa kitanzania wanapata elimu bila kikwazo. Mikopo kwa elimu ya juu inatolewa na serikali bila matatizo hivyo watoto wengi wa kitanzania wanapata elimu ya juu bila kikwazo. Vyumba vya madarasa vimejengwa/vinajengwa ili kukidhi ongezeko la watoto wanao jiunga.

2 Afya= zahanati za kisasa zimejengwa kila kona ya nchi, pamoja na vifaa vya kisasa.

3. Uchumi= tupo ktk uchumi wa kati.

4. Miundo mbinu tuko safi sana.

n.k n.k

Tanzania oyeeee
 
Wanabodi
leo tunapo sherehekea maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru, ni maadhimisho ya Tanzania, japo iliyopata uhuru ile Desemba 9, ni Tanganyika na sio Tanzania, maadhimisho ya leo ni maadhimisho ya Tanzania...
Acha porojo ni uhuru wa Tanganyika, uko shule mlienda kusomea ujinga
 

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom