Darling, I'm Sorry I can't go on

ChiefmTz

JF-Expert Member
Apr 15, 2008
2,937
938
Darling

Nadhani sasa ni miezi inayokaribiana na mwaka tangu tumeanza uhusiano wetu wa kimapenzi.Ndani yake tumefaidi mengi kutoka pande zote.Tumejifunza mengi. Tumefanya mengi.Tumeona mengi.

Darl naomba nikiri kwamba moyo wangu wa baridi juu ya mapenzi ya kweli ni wewe ndiye uliyeufanya ukawa moto na kujikuta ukiwa tayari kuhangaika kwa ajili ya kitu mapenzi.Na naomba nikiri kwamba safari yangu ya mapenzi ya kutafuta mapenzi ya dhati ilionekana kuwa hatimaye imefika mahala pake.

PENGINE UTASHITUKA LAKINI HUTASHANGAA KUPATA UJUMBE kutokana na kile ukiitacho KAWAIDA YANGU KULALAMIKA lakini naomba upokee ujumbe huu kama siyo kawaida yangu kwa kuwa nautoa nikiwa nimetulia bila ya hasira wala chochote ndani yangu.

Darling,moyo wangu umepata mateso sana kuona kuwa yale uliyoyataka hayapo, kama yapo basi hayaonekani, kama yanaonekana hayako katika uhalisia wake.Hali hii imeufanya ulie huku ukikaribia kutoa machozi ya damu.

Darl, naamini kwamba kwa kiwango changu nilijitahidi sana kukuonyesha ni kwa kiwango gani nilivyokukubali,na kwa kiwango nilikupenda na kiwango gani nilikuwa NIMEKUDONDOKEA. Hata hivyo nawe ulijitahidi kunionyesha kuwa nilikuwa wrong kukupenda kiasi hicho. Kwa hiyo tulifikiri tofauti.Lakini kwa bahati mbaya sikugundua hilo.

Lakini maneno yako ya mara kwa mara kuwa tunafikiria sambamba yalikuwa yakinipa moyo kiasi cha kunifanya niamini kuwa tu pamoja.

DARL naomba nikiri kwamba nimeutesa moyo wangu kwa kukupenda kwa kiwango hicho,nimetesa akili yangu sana kwa sababu ya kukupenda.nimeutesa mwili wangu kwa sababu ya kukupenda.Hata hivyo hayo yote ni mambo ya kawida katika mapenzi.

Lakini litakuwa ni jambo jema iwapo nitakuwa na uamuzi juu ya hili. Nao ni kusema "I'M SORRY I CANT GO ON" YOURS IN COLDED LOVE
 
Are you sure she will understand you? Mlikutana humu kwa JF? am sorry for her, very sorry....mmmh but its also possible wote mmepata wengine eeh...anyway yote ni maisha
 
Duuh hiyo yaitwa break up tena yenye majonzi makubwa sana. Pole Chiefmtz
 
Mkuu ChiefmTz sijaelewa.
Unamuaga mtu hapa JF?? Au wewe ni third part, yaani umeitoa mahali
?
 
Hii ina-prove theory yangu kwamba; Watu huwa makini sana katika kuandika message za break-up kuliko hata za kuomba uhusiano...
 
ChiefmTz, you are the man!Ni afadhali kumwambia mtu kuliko kumfanyia visa/cheatings. Poleni both kwa maumivu,but be there for her until she moves on!
I wish.......!
 
heee, mbona mapenzi yanakuwa shubiri kadiri cku zinavyosonga?.....haya mapenzi yangekuwepogo bwana khaaa.
 
ChiefmTz, you are the man!Ni afadhali kumwambia mtu kuliko kumfanyia visa/cheatings. Poleni both kwa maumivu,but be there for her until she moves on!
I wish.......!
I just wonder how did you know chiefmTz is a man and not a woman with broken heart??
 
Inasikitisha!

ChiefmTz pole sana!

Najaribu tu kuhisi hali uliyopo na nakuhurumia!

Nikupongeze tu kwa ujasiri; umekuwa mkweli kwa nafsi yako! najifunza kitu hapa!

Lakini napatwa na wasiwasi; naona imekaa kama kisasi hii bado!

Kwa nini nasema hivyo ni kutokana na ukweli mpaka dakika hii sisi hatukuwa tunafahamu kuwa ulikuwa na mpenzi humu ndani; hivyo bado uhusiano wenu ulikuwa ni wenu wawili! Sasa sijui ikiwa umekosa njia zote nyingine za kuwasilisha ujumbe wako lakini hii njia hata ka ahatumjui muhusika; bado ni kuwa umeweka hadharani kilichokuwa sirini!

Kwa namna moja kama muhusika nao mtazamo kama wangu miye; ni kuwa umemdhalilisha haijalishi yeye kuwa anonymous! Mie humuongelea mke wangu humu Mama Jr welll as far JF is concerned she is anonymous lakini si vyema kumdhalilisha hata kama hataingia JF milele.

Kumpenda mtu ni pamoja na kujali feelings zake hata kama unatofautiana naye kiasi gani.

Je umejiuliza yeye atajiasikiaje akikumbana na ujumbe wako? maana hata baada ya kuachana nyie mtabakia kuwa binadamu hai wenye feelings!
 
watu mna visA hapa,sasa mijadala ya divorce na break up inaongoza,mi nahisi mmeshaonjana sukari gulu yote imeisha sasa mnaonana kama makapi,haya mpasie FIDEL aitoe machungu,neeeeext:target:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom