Dark arts za intellijensia na utata wa kifo cha jasusi

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
18,914
28,524
Wakuu habari za mchana, natumaini wote wazima. Juzi nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha kuhusu mambo ya kijasusi cha "spies against armaggedon" humo nikakutana na term inaitwa DARK ARTS na katika kusaka maana zaidi mitandaoni nikakutana na case moja ya jasusi Gareth williams ambaye kifo chake kilihitimishwa kwa kusema aliuawa na mtu ambaye ni mtaalamu wa "dark arts" sasa kupitia case hii nategemea wajuzi wa hizi mambo mtusaidie je dark arts ni nini hasa kwenye tasnia ya ujasusi.

article-2122792-0D3205B9000005DC-252_306x491.jpg

Tarehe 23 august polisi wa nchini uingereza walikuta mwili wa kijana kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ndani ya bafu ambaye baadae mwili huo ulitambulika kuwa ni wa Gareth williams ambaye alikuwa anafanya kazi katika shirika la ujasusi la uingereza SIS (MI-6) katika kitengo cha mawasiliano. Kifo hichi kiliacha utata na maswali mengi kwa polisi kwa jinsi tukio hili lilivyotokea hadi kupelekea kifo cha jasusi huyu.

WILLIAMS NI NANI?
Gareth Williams alizaliwa
mwaka 1978 nchini wales iliyomo ndani ya United kingdom, na alikuwa "kipanga" wa hesabu ambapo aliisoma kwenye chuo kikuu cha Bangor na kuhitimu kwa mean GPA ya 1st class akiwa na miaka 17 tu!! Na aliendelea na masomo hayo hadi ngazi ya PhD na baadae kuajirwa katika taasisi ya kijasusi ya mawasiliano (GCHQ) ambapo baadae aliongezewa na majukumu ya ujasusi kupitia shirika la SIS maarufu kama Mi-6 ambalo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za kiintelijensia nje ya uingereza.Kazi kubwa ya bwana williams ilikuwa kulinda mifumo ya mawasiliano ya shirika la ujasusi na serikali ya uingereza huku pia akifuatilia mitandao ya watakatishaji pesa duniani

KIFO CHAKE
Baada ya kutoonekana kwa masiku kadhaa, marafiki waliwajulisha police kuhusu hofu yao hivyo mchana wa 23, august 2010 police walienda kukagua nyumba aliyopanga bwana williams. Walipofika walikuta mlango umerudishiwa vizuri, vitu vipo organized, ila hawakumuona na walipofika bafuni wakakutana na kibegi cha aina hii
article-2122792-0B22502B000005DC-531_306x385.jpg

Walipofungua wakakutana na mwili wa Bwana williamson ambao ulikwisha anza kuoza na katika uchunguzi huo wa awali hawakukuta alama yeyote ya kuumia,kupigwa au kunyweshwa sumu ambayo ingeweza pelekea kifo chake.
Pia wakiwa hapo bafuni hawakuona alama ya vidole vyake au vya mwingine yeyote kwenye kitu chochote ndani ya bafu au apartment hiyo hapo ndipo utata ulipoanza.

UTATA KWENYE UCHUNGUZI
1.Mwili wa williamson ulikutwa kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ajabu ni kwamba funguo ilikutwa ndani ya begi kwenye mgongo wa william na pia zipu ilifungwa vizuri na kufuli na ushahidi wote unaonyesha zipu ilifungiwa kwa ndani ila bado hakukuwa na alama ya vidole ya williams na wala hakuwa amevaa gloves je iliwezaje kufungwa kwa ndani ilihali kufuli ipo nje na funguo ipo ndani??

2. Nyumba waliikuta haijachezewa kokote sio dirisha sio mlango sio bafu yaani kilakitu kilikuwa kwenye mpangilio wake hivyo kama kuna muuaji basi mlango ungevunjwa au dirisha ila baada ya uchunguzi ikaonekana hakuna sehemu yoyote ya kuingia "iliyochezewa"

3. Pia CCTV camera zilizokuwepo hapo hazikuonyesha mtu akiingia wala akitoka katika makazi hayo ikimaanisha alijiua mwenyewe.

LAKINI.....

4. Baada ya kuanza uchunguzi kama alijiua walishangaa kukuta mwili wake haukuwa na dalili ya sumu yeyote kwenye mwili wake au damu wala jasusi huyo kuishiwa hewa kabla ya kifo hivyo swali likaibuka je alijiuaje??

5. Wachunguzi wakahisi itakuwa alipoingia kwenye begi alishindwa kujitoa hivyo aliishiwa hewa au alipata "ajali" nyingine akafariki lakini walipojaribu kuingia kwenye begi kwa kutafuta ''mtaalam'' wa gymnastics ambaye ana asili ya mwili kama wa williams bado ilikuwa ngumu kufunga begi kutokea ndani hivyo lazima alikuwepo mtu wa pili ambaye alilifunga!!

ILA......

Kama mtu wa pili alimuingiza akiwa hai polisi hawakuona dalili ya williams kupambana kuokoa uhai wake kabla ya kufariki ndani ya begi na wala hawakuona alama ya mikono kwenye zipu upande wa ndani wa begi!!

Hivyo kama kuna mtu alimuua je alimuua kutumia nni?? Hawakuona sumu kwenye damu wala kovu wala ushahidi kwamba alipigwa na kitu kilichopelekea kifo?? Je hapa nini kilimuua??
hoodedmanknife-1.jpg

TAARIFA MPYA YAIBUKA
Ilipofika mwaka 2015 alitokea jasusi wa kirusi ambaye alidai kuna majasusi wenzake wa kirusi walimuua Bwana williams kwa kumuingizia sumu kwenye sikio, lakini taarifa za Bwana huyu zilikosa ushahidi kabisa katika uchunguzi wa polisi na wataalamu wengine wa Mi-6 ukizingatia huyu jasusi alikuwa amekimbia urusi huku uingereza ikikataa kumchukua kwenye shirika lake la kijasusi wakiamini ni pandikizi hivyo taarifa zake zilipuuzwa maana walihisi anatafuta "kiki" ya kuaminika na kuingizwa kwenye shirika lao.

HITIMISHO
Ni kweli majasusi huwa wanatumia taaluma nyingi hata nyingine za kiroho maana kuna story za jasusi mmoja wa kiyahudi huko ufaransa aliyekuwa akipita mtaani ni kma upepo yaani hakuna anayejua kuwa kuna mtu kapita dakika hiyo na wala kwenye CCTV humuoni..... Sasa cha kujiuliza je dark arts inahusisha nguvu zingine za kiroho au ni mafunzo tu ya kiakili na kimwili ya hali ya juu ili kufanya kazi hizi za ujasusi kwa weledi?

Naomba kuwasilisha

cc Prof Richard Mshana Jr Malcom Lumumba Elungata ningeomba mpite huku
 
Dark arts ni techniques zinazotumiwa na majasusi au hata vikosi maalumu vya makomando ili kutekeleza jambo fulani.

Kaa kawaida mafunzo ya hizo mbinu hufanywa baada ya jasusi, au special forces trainee anapo maliza mafunzo kamili na ku graduate.
Hakuna anaejua sana ni nini kinafundishwa humo kambini.

Mafunzo haya bi ya siri sana kiasi kwamba hata wanaopata nafasi ya kufundishwa huwa hata hawasemi au hata kujaribu kutamka chochote kuhusu hizo mbinu walizofundishwa.

Mara nyingi vikosi vya kijeshi au kijasusi vyenye kujifunza hzi mbinu huwa vinalindwa sana na serikali. Mfano kikosi maalumu cha CIA kinachoitwa SAD(special activity division).. hiki ni kikosi maalum ndani ya C.I.A kinachohusika na mauaji, utekaji, kuvuruga aman ndani ya nchi ya adui.. na ukombozi. Lakin kikosi hiki ni cha siri sana kiasi kwamba serikali hukataa uwepo wake na hata budget yake huwa haijulikani.

Askari ndani ya kikosi hiko ni makomando waliotoka jeshini. Huchukuliwa na kufundishwa mbinu zaidi za kimedani... na dark arts.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu swala la kiimani ni suala la mtu individual. Mara nyingi serikali haziamini ktk uchawi. Huamini ktk science...
So ndani ya mashirika ya ujasusi kuna vitengo vya science ambavyo kazi yake kubwa ni kutengeneza kuvumbua technologia itayo wasaidia majasus kutekeleza kazi zao..
Ikiwemo kutengeneza sumu
maalumu, kutengeneza roboti.. au mfumo maalum wa mwasiliano.. na vingine vingi..

So kwa kesi ya jamaa. Kuna possibility kulitumika technologia au sumu ya aina yake kumuua..
Lakin pia majasus hawa huwa wanafundishwa jinsi ya kuua bila kuacha halama( bila kuacha ushahidi)

so unaona wametekeleza kazi bila kujulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duniani kuna siri nyingi sana...
Hii Dark art lazima itakua imeegemea kwenye ushirikina sasa tunataka kujua huo uchawi ulifanyikaje mpaka mtu akaweza kujitumbukiza mwenyewe kwenye Begi ...
Ila sisi wa Afrika tunatumiaga Majini ambapo linampumbaza mtu nakuweza kujiua yeye mwenyewe kwa kujitupa kutoka mbali au kujinyonga au kujizamisha Mtoni au Baharini

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
Write your reply...wanaposema jasusi anapita kama upepo haonekani kwenye cctv,haina maana kuwa kweli hupita pale kimazingara,hawa watu kabla ya kwenda kufanya tukio sehemu,wanastudy eneo na kuangalia camera ziko angle gani,kwahiyo anapopita anapita angle ambayo camera haitamnasa,na kama coverage ni ngumu kuikwepa wanahack mfumo wa cctv usiweze kunasa matukio kwa mda atakaoukua anaingia hadi kutoka mahali
 
Kuhusu swala la kiimani ni suala la mtu individual. Mara nyingi serikali haziamini ktk uchawi. Huamini ktk science...
So ndani ya mashirika ya ujasusi kuna vitengo vya science ambavyo kazi yake kubwa ni kutengeneza kuvumbua technologia itayo wasaidia majasus kutekeleza kazi zao..
Ikiwemo kutengeneza sumu
maalumu, kutengeneza roboti.. au mfumo maalum wa mwasiliano.. na vingine vingi..

So kwa kesi ya jamaa. Kuna possibility kulitumika technologia au sumu ya aina yake kumuua..
Lakin pia majasus hawa huwa wanafundishwa jinsi ya kuua bila kuacha halama( bila kuacha ushahidi)

so unaona wametekeleza kazi bila kujulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nashukuru kwa nondo zako nimekusoma haswaaa ila hapo kuhusu uchawi je ni kweli serikali "haziamini" katika uchawi maana kuna kipindi nlisoma ripoti moja iliyokuwa declassified ya CIA inaelezea kuhusu wapiganaji wa mai mai DRC ambao walikuwa wakipigwa risasi hazipenyi kwenye mwili...... Lakini cha kushangaza wakienda wazungu hayo hayatokei maana walishajua kuwa wakikanyaga miguu kwenye ardhi hauwezi kuwaua ila wakiwa kwenye gari au mti au eneo lolote ambalo miguu haishiki ardhi basi risasi zitapenya!!! How do you know that kama huamini katika uchawi..... Na labda nikiuliza hivi huko iraq tumesikia rebels wanatumia majini sana tu lakini mbona hayakufanya kazi kwa wazungu!! Je hakuna uwezekano nao walitumia "nguvu mbadala"??
 
Duniani kuna siri nyingi sana...
Hii Dark art lazima itakua imeegemea kwenye ushirikina sasa tunataka kujua huo uchawi ulifanyikaje mpaka mtu akaweza kujitumbukiza mwenyewe kwenye Begi ...
Ila sisi wa Afrika tunatumiaga Majini ambapo linampumbaza mtu nakuweza kujiua yeye mwenyewe kwa kujitupa kutoka mbali au kujinyonga au kujizamisha Mtoni au Baharini

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
Dark arts si ushirikina mkuu. Ni mbinu ambazo ni za siri sana lakin ni very effective.
Darks arts inajumuisha silaha mbalimbali.. martial arts na mbinu za kutumia chochote kilicho kwenye mazingira yako kama silaha......na vingine vingi..

Hwenzetu hawaamini ktk uchawi.. wanamaamini ktk science.. ama sayansi. Ndio maana ndani ya mshirika ya ujasusi kuna vitengo maalumu ndani ya mashirika haya.. kazi yake kubwa ni kuvumbua na kutengeneza technologia mpya zitakazo wasaidi majasus kwenye kazi zao.. hizi zinaweza kuwa sumu kali , silaha ambazo uraiani hazijawahi kuonekana, chemicali za kuyeyusha mwili wa mwanadam kwa haraka sana.
Technologia hizo ni za siri sana na kiasi kwamba ni maafisa wachache wa serikali wanafahamu. Tena wale wa ndani ya vitengo.
Rais wa nchi anaweza hata asijue, na hata wakiulizwa watakana kuwa hazipo

Hebu tuadisie kwa maono yake huyu jamaa Williams ilitumika njia gani kumuua kwa style ile?

'HOW MUCH IS TOO MUCH?'
 
93 Reactions
Reply
Back
Top Bottom