zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 18,919
- 28,535
Wakuu habari za mchana, natumaini wote wazima. Juzi nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha kuhusu mambo ya kijasusi cha "spies against armaggedon" humo nikakutana na term inaitwa DARK ARTS na katika kusaka maana zaidi mitandaoni nikakutana na case moja ya jasusi Gareth williams ambaye kifo chake kilihitimishwa kwa kusema aliuawa na mtu ambaye ni mtaalamu wa "dark arts" sasa kupitia case hii nategemea wajuzi wa hizi mambo mtusaidie je dark arts ni nini hasa kwenye tasnia ya ujasusi.
Tarehe 23 august polisi wa nchini uingereza walikuta mwili wa kijana kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ndani ya bafu ambaye baadae mwili huo ulitambulika kuwa ni wa Gareth williams ambaye alikuwa anafanya kazi katika shirika la ujasusi la uingereza SIS (MI-6) katika kitengo cha mawasiliano. Kifo hichi kiliacha utata na maswali mengi kwa polisi kwa jinsi tukio hili lilivyotokea hadi kupelekea kifo cha jasusi huyu.
WILLIAMS NI NANI?
Gareth Williams alizaliwa
mwaka 1978 nchini wales iliyomo ndani ya United kingdom, na alikuwa "kipanga" wa hesabu ambapo aliisoma kwenye chuo kikuu cha Bangor na kuhitimu kwa mean GPA ya 1st class akiwa na miaka 17 tu!! Na aliendelea na masomo hayo hadi ngazi ya PhD na baadae kuajirwa katika taasisi ya kijasusi ya mawasiliano (GCHQ) ambapo baadae aliongezewa na majukumu ya ujasusi kupitia shirika la SIS maarufu kama Mi-6 ambalo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za kiintelijensia nje ya uingereza.Kazi kubwa ya bwana williams ilikuwa kulinda mifumo ya mawasiliano ya shirika la ujasusi na serikali ya uingereza huku pia akifuatilia mitandao ya watakatishaji pesa duniani
KIFO CHAKE
Baada ya kutoonekana kwa masiku kadhaa, marafiki waliwajulisha police kuhusu hofu yao hivyo mchana wa 23, august 2010 police walienda kukagua nyumba aliyopanga bwana williams. Walipofika walikuta mlango umerudishiwa vizuri, vitu vipo organized, ila hawakumuona na walipofika bafuni wakakutana na kibegi cha aina hii
Walipofungua wakakutana na mwili wa Bwana williamson ambao ulikwisha anza kuoza na katika uchunguzi huo wa awali hawakukuta alama yeyote ya kuumia,kupigwa au kunyweshwa sumu ambayo ingeweza pelekea kifo chake.
Pia wakiwa hapo bafuni hawakuona alama ya vidole vyake au vya mwingine yeyote kwenye kitu chochote ndani ya bafu au apartment hiyo hapo ndipo utata ulipoanza.
UTATA KWENYE UCHUNGUZI
1.Mwili wa williamson ulikutwa kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ajabu ni kwamba funguo ilikutwa ndani ya begi kwenye mgongo wa william na pia zipu ilifungwa vizuri na kufuli na ushahidi wote unaonyesha zipu ilifungiwa kwa ndani ila bado hakukuwa na alama ya vidole ya williams na wala hakuwa amevaa gloves je iliwezaje kufungwa kwa ndani ilihali kufuli ipo nje na funguo ipo ndani??
2. Nyumba waliikuta haijachezewa kokote sio dirisha sio mlango sio bafu yaani kilakitu kilikuwa kwenye mpangilio wake hivyo kama kuna muuaji basi mlango ungevunjwa au dirisha ila baada ya uchunguzi ikaonekana hakuna sehemu yoyote ya kuingia "iliyochezewa"
3. Pia CCTV camera zilizokuwepo hapo hazikuonyesha mtu akiingia wala akitoka katika makazi hayo ikimaanisha alijiua mwenyewe.
LAKINI.....
4. Baada ya kuanza uchunguzi kama alijiua walishangaa kukuta mwili wake haukuwa na dalili ya sumu yeyote kwenye mwili wake au damu wala jasusi huyo kuishiwa hewa kabla ya kifo hivyo swali likaibuka je alijiuaje??
5. Wachunguzi wakahisi itakuwa alipoingia kwenye begi alishindwa kujitoa hivyo aliishiwa hewa au alipata "ajali" nyingine akafariki lakini walipojaribu kuingia kwenye begi kwa kutafuta ''mtaalam'' wa gymnastics ambaye ana asili ya mwili kama wa williams bado ilikuwa ngumu kufunga begi kutokea ndani hivyo lazima alikuwepo mtu wa pili ambaye alilifunga!!
ILA......
Kama mtu wa pili alimuingiza akiwa hai polisi hawakuona dalili ya williams kupambana kuokoa uhai wake kabla ya kufariki ndani ya begi na wala hawakuona alama ya mikono kwenye zipu upande wa ndani wa begi!!
Hivyo kama kuna mtu alimuua je alimuua kutumia nni?? Hawakuona sumu kwenye damu wala kovu wala ushahidi kwamba alipigwa na kitu kilichopelekea kifo?? Je hapa nini kilimuua??
TAARIFA MPYA YAIBUKA
Ilipofika mwaka 2015 alitokea jasusi wa kirusi ambaye alidai kuna majasusi wenzake wa kirusi walimuua Bwana williams kwa kumuingizia sumu kwenye sikio, lakini taarifa za Bwana huyu zilikosa ushahidi kabisa katika uchunguzi wa polisi na wataalamu wengine wa Mi-6 ukizingatia huyu jasusi alikuwa amekimbia urusi huku uingereza ikikataa kumchukua kwenye shirika lake la kijasusi wakiamini ni pandikizi hivyo taarifa zake zilipuuzwa maana walihisi anatafuta "kiki" ya kuaminika na kuingizwa kwenye shirika lao.
HITIMISHO
Ni kweli majasusi huwa wanatumia taaluma nyingi hata nyingine za kiroho maana kuna story za jasusi mmoja wa kiyahudi huko ufaransa aliyekuwa akipita mtaani ni kma upepo yaani hakuna anayejua kuwa kuna mtu kapita dakika hiyo na wala kwenye CCTV humuoni..... Sasa cha kujiuliza je dark arts inahusisha nguvu zingine za kiroho au ni mafunzo tu ya kiakili na kimwili ya hali ya juu ili kufanya kazi hizi za ujasusi kwa weledi?
Naomba kuwasilisha
cc Prof Richard Mshana Jr Malcom Lumumba Elungata ningeomba mpite huku