Dark arts za intellijensia na utata wa kifo cha jasusi

zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,611
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,611 2,000
Wakuu habari za mchana, natumaini wote wazima. Juzi nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha kuhusu mambo ya kijasusi cha "spies against armaggedon" humo nikakutana na term inaitwa DARK ARTS na katika kusaka maana zaidi mitandaoni nikakutana na case moja ya jasusi Gareth williams ambaye kifo chake kilihitimishwa kwa kusema aliuawa na mtu ambaye ni mtaalamu wa "dark arts" sasa kupitia case hii nategemea wajuzi wa hizi mambo mtusaidie je dark arts ni nini hasa kwenye tasnia ya ujasusi.

article-2122792-0d3205b9000005dc-252_306x491-jpg.854874

Tarehe 23 august polisi wa nchini uingereza walikuta mwili wa kijana kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ndani ya bafu ambaye baadae mwili huo ulitambulika kuwa ni wa Gareth williams ambaye alikuwa anafanya kazi katika shirika la ujasusi la uingereza SIS (MI-6) katika kitengo cha mawasiliano. Kifo hichi kiliacha utata na maswali mengi kwa polisi kwa jinsi tukio hili lilivyotokea hadi kupelekea kifo cha jasusi huyu.

WILLIAMS NI NANI?
Gareth Williams alizaliwa
mwaka 1978 nchini wales iliyomo ndani ya United kingdom, na alikuwa "kipanga" wa hesabu ambapo aliisoma kwenye chuo kikuu cha Bangor na kuhitimu kwa mean GPA ya 1st class akiwa na miaka 17 tu!! Na aliendelea na masomo hayo hadi ngazi ya PhD na baadae kuajirwa katika taasisi ya kijasusi ya mawasiliano (GCHQ) ambapo baadae aliongezewa na majukumu ya ujasusi kupitia shirika la SIS maarufu kama Mi-6 ambalo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za kiintelijensia nje ya uingereza.Kazi kubwa ya bwana williams ilikuwa kulinda mifumo ya mawasiliano ya shirika la ujasusi na serikali ya uingereza huku pia akifuatilia mitandao ya watakatishaji pesa duniani

KIFO CHAKE
Baada ya kutoonekana kwa masiku kadhaa, marafiki waliwajulisha police kuhusu hofu yao hivyo mchana wa 23, august 2010 police walienda kukagua nyumba aliyopanga bwana williams. Walipofika walikuta mlango umerudishiwa vizuri, vitu vipo organized, ila hawakumuona na walipofika bafuni wakakutana na kibegi cha aina hii
article-2122792-0b22502b000005dc-531_306x385-jpg.854827


Walipofungua wakakutana na mwili wa Bwana williamson ambao ulikwisha anza kuoza na katika uchunguzi huo wa awali hawakukuta alama yeyote ya kuumia,kupigwa au kunyweshwa sumu ambayo ingeweza pelekea kifo chake.
Pia wakiwa hapo bafuni hawakuona alama ya vidole vyake au vya mwingine yeyote kwenye kitu chochote ndani ya bafu au apartment hiyo hapo ndipo utata ulipoanza.

UTATA KWENYE UCHUNGUZI
1.Mwili wa williamson ulikutwa kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ajabu ni kwamba funguo ilikutwa ndani ya begi kwenye mgongo wa william na pia zipu ilifungwa vizuri na kufuli na ushahidi wote unaonyesha zipu ilifungiwa kwa ndani ila bado hakukuwa na alama ya vidole ya williams na wala hakuwa amevaa gloves je iliwezaje kufungwa kwa ndani ilihali kufuli ipo nje na funguo ipo ndani??

2. Nyumba waliikuta haijachezewa kokote sio dirisha sio mlango sio bafu yaani kilakitu kilikuwa kwenye mpangilio wake hivyo kama kuna muuaji basi mlango ungevunjwa au dirisha ila baada ya uchunguzi ikaonekana hakuna sehemu yoyote ya kuingia "iliyochezewa"

3. Pia CCTV camera zilizokuwepo hapo hazikuonyesha mtu akiingia wala akitoka katika makazi hayo ikimaanisha alijiua mwenyewe.

LAKINI.....

4. Baada ya kuanza uchunguzi kama alijiua walishangaa kukuta mwili wake haukuwa na dalili ya sumu yeyote kwenye mwili wake au damu wala jasusi huyo kuishiwa hewa kabla ya kifo hivyo swali likaibuka je alijiuaje??

5. Wachunguzi wakahisi itakuwa alipoingia kwenye begi alishindwa kujitoa hivyo aliishiwa hewa au alipata "ajali" nyingine akafariki lakini walipojaribu kuingia kwenye begi kwa kutafuta ''mtaalam'' wa gymnastics ambaye ana asili ya mwili kama wa williams bado ilikuwa ngumu kufunga begi kutokea ndani hivyo lazima alikuwepo mtu wa pili ambaye alilifunga!!

ILA......

Kama mtu wa pili alimuingiza akiwa hai polisi hawakuona dalili ya williams kupambana kuokoa uhai wake kabla ya kufariki ndani ya begi na wala hawakuona alama ya mikono kwenye zipu upande wa ndani wa begi!!

Hivyo kama kuna mtu alimuua je alimuua kutumia nni?? Hawakuona sumu kwenye damu wala kovu wala ushahidi kwamba alipigwa na kitu kilichopelekea kifo?? Je hapa nini kilimuua??
hoodedmanknife-1-jpg.854910


TAARIFA MPYA YAIBUKA
Ilipofika mwaka 2015 alitokea jasusi wa kirusi ambaye alidai kuna majasusi wenzake wa kirusi walimuua Bwana williams kwa kumuingizia sumu kwenye sikio, lakini taarifa za Bwana huyu zilikosa ushahidi kabisa katika uchunguzi wa polisi na wataalamu wengine wa Mi-6 ukizingatia huyu jasusi alikuwa amekimbia urusi huku uingereza ikikataa kumchukua kwenye shirika lake la kijasusi wakiamini ni pandikizi hivyo taarifa zake zilipuuzwa maana walihisi anatafuta "kiki" ya kuaminika na kuingizwa kwenye shirika lao.

HITIMISHO
Ni kweli majasusi huwa wanatumia taaluma nyingi hata nyingine za kiroho maana kuna story za jasusi mmoja wa kiyahudi huko ufaransa aliyekuwa akipita mtaani ni kma upepo yaani hakuna anayejua kuwa kuna mtu kapita dakika hiyo na wala kwenye CCTV humuoni..... Sasa cha kujiuliza je dark arts inahusisha nguvu zingine za kiroho au ni mafunzo tu ya kiakili na kimwili ya hali ya juu ili kufanya kazi hizi za ujasusi kwa weledi?

Naomba kuwasilisha

cc Prof Richard Mshana Jr Malcom Lumumba Elungata ningeomba mpite huku
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,611
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,611 2,000
Mkuu zitto junior mada yako ni fikirishi sana

na nimepitia kila comment humu na nimejiunza mengi

yapo yaliyoniingia na nimeyaunga mkono na yapo yaliyoniacha njiapanda na yapo ambayo hayaingii akilini hata kidogo

all in all nimeenjoy kusoma mada hii na comments husika

next time naomba unitag kwa thread kama hizi

Thanks mkuu
Hii umeipitia mkuu?
 
Blue G

Blue G

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
5,037
Points
2,000
Blue G

Blue G

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
5,037 2,000
Hii umeipitia mkuu?
yeah mkuu hii ndio iliyonipeleka mpaka huko
 
Omary Ndama

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2017
Messages
3,092
Points
2,000
Omary Ndama

Omary Ndama

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2017
3,092 2,000
Na wakati akiyafanya hayo vp CCTV camera kutomuona mkuu..
Ni rahisi mno, aliyefanya yale mauaji alikuwa ni mjuzi wa
Chi power (vital force)
Telekinesis na
Telepathy
Muuaji alichofanya ni kutumia CHI POWER Kuondoa uhai bila kumgusa mhanga.. Yani anarusha mkono lakini haumfikii mhanga kinachofika ni nguvu yenye mitetemo (vibrations) ndio inayopiga
Baada ya hapo muuaji alitumia telekinesis /telepath kumnyanyua kumuingiza kwenye begi kufunga begi nk bila kugusa chochote
Telekinesis ni uwezo wa kuhamisha vitu bila kuvigusa

Jr
 
Old - Hand

Old - Hand

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Messages
1,342
Points
2,000
Old - Hand

Old - Hand

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2017
1,342 2,000
Aaah aaah aah msee mjanja mjanja wewe..

Una kamba saaana dah
Mh ok
Ni wachache wamewahi kusoma aina hii ya ujuzi na wakatoka salama na ndio maana hadi leo sio sayansi pana miongini mwa jamii nyingi za kijasusi....

Lakini mkuu zitto junior ili walau uelewe kwa mbali inabidi usome kuhusu huo uchawi mweusi na huyo jasusi inaonekana aliuwawa kwa CURSES HEXES ambapo nia ni kukufanya uwe mhanga wa kifo katika uwezo wako mwenyew na aina hii ya mauaji hufanyika eneo tulivu sana huku muuaji akiwa katika angle ya Brevity na mlengwa akiwa angle ya curation.....

Hii inakuwa ni kama zoezi la kuhamisha kivuli chako mwenyewe na alipakiwa kwenye begi kwa njia ya SPELL ambapo unaweza kuamua kufanya kitendo ukiwa nyuma ya kitu yani mfano unaweza kuhamisha kitu ndani nakukiweka sehemu nyingin ukiwa nje na umefunga mlango ila lazima uwe karibu na mlango.....

Dah huyo jamaa alikufa kifo kibaya sana na chenye mateso mengi japo hakina ushahidi...

Lakini pia alieuwa naamini alikuwa katika mazoezi ya vitendo....

Naomba niishie hapa ila ni hatar kujifunza Dark Magic/art View attachment 855182View attachment 855182View attachment 855183View attachment 855182View attachment 855183
 
Old - Hand

Old - Hand

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Messages
1,342
Points
2,000
Old - Hand

Old - Hand

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2017
1,342 2,000
Unataka kumtapeli huyo jamaa, acha hzo tabia za utapeli
Braza kwan nimemuambia alete pesa.. Mi ninemuambia anichek pm.... We haujui pm kuna nini?

Utamchuuza mwenzako kizeeembe
 
T

The Wakanda Panth3r

Senior Member
Joined
May 22, 2018
Messages
145
Points
225
T

The Wakanda Panth3r

Senior Member
Joined May 22, 2018
145 225
Salaam Wakuu!Kiongozi zitto jr. mada ya leo ni ngumu kuifafanua kwa kweli!
Dark Arts/Dark Magic na Mashirika ya Kijasusi au Ujasusi ni Jambo tata kulithibitisha - Ubishi ni Mwingi sana- Lakini wasomi wa mambo ya espionage wanakiri kuwepo kwa Mafunzo hayo katika Kambi za Ujasusi kote ulimwenguni - Ni Mafunzo kimsingi ambayo Jasusi huwezeshwa ili aweze kumudu kazi zake vyema na kwa ustadi mkuu - Wanadai ni pamoja na Kufungua Makufuri ya milango bila funguo,Kujificha sehemu iliyowazi bila mtu kukuona(Camouflage).
Kupotea mbele ya Macho ya watu - Sio Kimazingaombwe bali ni kwa kukalukuleti umakini wa watu na kuwaacha wanazubaa,hii mimi nishahidi kabisa nadhani hii inafundishika kirahisi - Wakati wa Kampeni za Urais 2006 - Wale wajamaa wa kitengo walikuwa wanne wamepanda pembeni ya Vx ya Mgombea wa CCM JK;Jamaa waliluka toka kwenye gari wakapotolea kwenye Umati wa Watu;Sikuweza kuwaona walipoelekea.
Kuua mtu bila kuacha alama - Hapa sasa inahusisha mafunzo ya kuimprovise sumu rahisi kwenye mazingira uliyopo,au kutumia mikono au kitu chochote ambacho kinamfanya adui apoteze uhai kwa haraka.
Inasemekana Kuna Sumu inatengenezwa Saudia Arabia - Sumu hii (Jina nimelisahau) inatumiwa sana na Majasusi na watu waliopania kulipa kisasi;Ukimwekea mtu kwenye Chakula hata umpeleke wapi? watasema ni Shinikizo la Damu tu.

Lakini nadharia nyingine inadai Black arts inahusishwa na mambo ya Kimshana Jr (Occultism). Hii inahusisha Ushirikina kabisa wa kutazama Nyota na Nguvu za Asili. Na baadhi ya watu walifanikiwa sana kwenye Ujasusi wakati wa Vita vya Pili vya Dunia walikuhishwa na matumizi ya Black art akiwemo Hitler na genge lake.
wengine wanadai inahusisha mpaka Magical Spells;ABRACADABRA.
Lakini shida inakuja hakuna anayeweza kuthibitisha kuwa Watu wa vitengo vya Ujasusi hutumia mambo ya namna hii.

Miaka 1980's Ndugu Ludovick Mwijage akiwa katika nchi ya Swaziland akiendelea kusaka haki ya Ukimbizi wa kisiasa,akiwa katoroka Tanzania akijaribu kutafuta namna yakutorokea Ulaya anakutana na Sheikh Yahya Hussein naye akiwa katika shughuli zake za kutibu watu hapo swaziland,ghafla anapata ushawishi wakukutana na Sheikh yahya na kumwelezea shida yake ya kukosana na Utawala wa Nyerere,Sheikh anaonesha huruma na kusikitishwa sana na kumpa apointment amtafute waongee zaidi;akamwambia afike hotel aliyofikia pale swaziland.
Siku aliyofika alikwenda na Documents zake muhimu kwa Sheikh;Lakini alipotaka kuondoka akazikosa kabisa zile documents zikapotea katika mazingira ya kutatanisha - Sheikh akaonesha kushangaa kweli eti documents zimepotea poteaje pale!
Jamaa akaamua kuondoka bila documents zake akiamini kuwa labda kazisahau mahala pengine; lakini kila akikumbuka anashangaa kwamba wakati anakwenda kwa Sheikh Alikwenda nazo!

Bahati mbaya akajichanganya akadakwa na Frelimo wakampakia mpaka Msumbiji,baadae akakabidhiwa kwa TISS Mtwara; wakamsafirisha mpaka Dar; Akafikishiwa Black site moja kwa ajili ya Mahojiano mazito na Mateso;Ni wakati wa mahojiano ndipo alipobaki Mdomo wazi ; Jamaa wakaja na zile Documents alizopoteza Swaziland akiwa chumbani kwa Sheikh! Je ? Hiyo ndio Black Arts?

Asante Zitto Jr! Kwa Kunitag! Be Blessed Man.
Kupotea mbele ya macho ya watu. Ni sahihi kabisa
 

Forum statistics

Threads 1,326,248
Members 509,448
Posts 32,215,758
Top