Dark arts za intellijensia na utata wa kifo cha jasusi

zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,611
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,611 2,000
Wakuu habari za mchana, natumaini wote wazima. Juzi nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha kuhusu mambo ya kijasusi cha "spies against armaggedon" humo nikakutana na term inaitwa DARK ARTS na katika kusaka maana zaidi mitandaoni nikakutana na case moja ya jasusi Gareth williams ambaye kifo chake kilihitimishwa kwa kusema aliuawa na mtu ambaye ni mtaalamu wa "dark arts" sasa kupitia case hii nategemea wajuzi wa hizi mambo mtusaidie je dark arts ni nini hasa kwenye tasnia ya ujasusi.

article-2122792-0d3205b9000005dc-252_306x491-jpg.854874

Tarehe 23 august polisi wa nchini uingereza walikuta mwili wa kijana kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ndani ya bafu ambaye baadae mwili huo ulitambulika kuwa ni wa Gareth williams ambaye alikuwa anafanya kazi katika shirika la ujasusi la uingereza SIS (MI-6) katika kitengo cha mawasiliano. Kifo hichi kiliacha utata na maswali mengi kwa polisi kwa jinsi tukio hili lilivyotokea hadi kupelekea kifo cha jasusi huyu.

WILLIAMS NI NANI?
Gareth Williams alizaliwa
mwaka 1978 nchini wales iliyomo ndani ya United kingdom, na alikuwa "kipanga" wa hesabu ambapo aliisoma kwenye chuo kikuu cha Bangor na kuhitimu kwa mean GPA ya 1st class akiwa na miaka 17 tu!! Na aliendelea na masomo hayo hadi ngazi ya PhD na baadae kuajirwa katika taasisi ya kijasusi ya mawasiliano (GCHQ) ambapo baadae aliongezewa na majukumu ya ujasusi kupitia shirika la SIS maarufu kama Mi-6 ambalo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za kiintelijensia nje ya uingereza.Kazi kubwa ya bwana williams ilikuwa kulinda mifumo ya mawasiliano ya shirika la ujasusi na serikali ya uingereza huku pia akifuatilia mitandao ya watakatishaji pesa duniani

KIFO CHAKE
Baada ya kutoonekana kwa masiku kadhaa, marafiki waliwajulisha police kuhusu hofu yao hivyo mchana wa 23, august 2010 police walienda kukagua nyumba aliyopanga bwana williams. Walipofika walikuta mlango umerudishiwa vizuri, vitu vipo organized, ila hawakumuona na walipofika bafuni wakakutana na kibegi cha aina hii
article-2122792-0b22502b000005dc-531_306x385-jpg.854827

Walipofungua wakakutana na mwili wa Bwana williamson ambao ulikwisha anza kuoza na katika uchunguzi huo wa awali hawakukuta alama yeyote ya kuumia,kupigwa au kunyweshwa sumu ambayo ingeweza pelekea kifo chake.
Pia wakiwa hapo bafuni hawakuona alama ya vidole vyake au vya mwingine yeyote kwenye kitu chochote ndani ya bafu au apartment hiyo hapo ndipo utata ulipoanza.

UTATA KWENYE UCHUNGUZI
1.Mwili wa williamson ulikutwa kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ajabu ni kwamba funguo ilikutwa ndani ya begi kwenye mgongo wa william na pia zipu ilifungwa vizuri na kufuli na ushahidi wote unaonyesha zipu ilifungiwa kwa ndani ila bado hakukuwa na alama ya vidole ya williams na wala hakuwa amevaa gloves je iliwezaje kufungwa kwa ndani ilihali kufuli ipo nje na funguo ipo ndani??

2. Nyumba waliikuta haijachezewa kokote sio dirisha sio mlango sio bafu yaani kilakitu kilikuwa kwenye mpangilio wake hivyo kama kuna muuaji basi mlango ungevunjwa au dirisha ila baada ya uchunguzi ikaonekana hakuna sehemu yoyote ya kuingia "iliyochezewa"

3. Pia CCTV camera zilizokuwepo hapo hazikuonyesha mtu akiingia wala akitoka katika makazi hayo ikimaanisha alijiua mwenyewe.

LAKINI.....

4. Baada ya kuanza uchunguzi kama alijiua walishangaa kukuta mwili wake haukuwa na dalili ya sumu yeyote kwenye mwili wake au damu wala jasusi huyo kuishiwa hewa kabla ya kifo hivyo swali likaibuka je alijiuaje??

5. Wachunguzi wakahisi itakuwa alipoingia kwenye begi alishindwa kujitoa hivyo aliishiwa hewa au alipata "ajali" nyingine akafariki lakini walipojaribu kuingia kwenye begi kwa kutafuta ''mtaalam'' wa gymnastics ambaye ana asili ya mwili kama wa williams bado ilikuwa ngumu kufunga begi kutokea ndani hivyo lazima alikuwepo mtu wa pili ambaye alilifunga!!

ILA......

Kama mtu wa pili alimuingiza akiwa hai polisi hawakuona dalili ya williams kupambana kuokoa uhai wake kabla ya kufariki ndani ya begi na wala hawakuona alama ya mikono kwenye zipu upande wa ndani wa begi!!

Hivyo kama kuna mtu alimuua je alimuua kutumia nni?? Hawakuona sumu kwenye damu wala kovu wala ushahidi kwamba alipigwa na kitu kilichopelekea kifo?? Je hapa nini kilimuua??
hoodedmanknife-1-jpg.854910

TAARIFA MPYA YAIBUKA
Ilipofika mwaka 2015 alitokea jasusi wa kirusi ambaye alidai kuna majasusi wenzake wa kirusi walimuua Bwana williams kwa kumuingizia sumu kwenye sikio, lakini taarifa za Bwana huyu zilikosa ushahidi kabisa katika uchunguzi wa polisi na wataalamu wengine wa Mi-6 ukizingatia huyu jasusi alikuwa amekimbia urusi huku uingereza ikikataa kumchukua kwenye shirika lake la kijasusi wakiamini ni pandikizi hivyo taarifa zake zilipuuzwa maana walihisi anatafuta "kiki" ya kuaminika na kuingizwa kwenye shirika lao.

HITIMISHO
Ni kweli majasusi huwa wanatumia taaluma nyingi hata nyingine za kiroho maana kuna story za jasusi mmoja wa kiyahudi huko ufaransa aliyekuwa akipita mtaani ni kma upepo yaani hakuna anayejua kuwa kuna mtu kapita dakika hiyo na wala kwenye CCTV humuoni..... Sasa cha kujiuliza je dark arts inahusisha nguvu zingine za kiroho au ni mafunzo tu ya kiakili na kimwili ya hali ya juu ili kufanya kazi hizi za ujasusi kwa weledi?

Naomba kuwasilisha

cc Prof Richard Mshana Jr Malcom Lumumba Elungata ningeomba mpite huku
 
Vi rendra

Vi rendra

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Messages
1,599
Points
2,000
Vi rendra

Vi rendra

JF-Expert Member
Joined Sep 11, 2017
1,599 2,000
Ni rahisi mno, aliyefanya yale mauaji alikuwa ni mjuzi wa
Chi power (vital force)
Telekinesis na
Telepathy
Muuaji alichofanya ni kutumia CHI POWER Kuondoa uhai bila kumgusa mhanga.. Yani anarusha mkono lakini haumfikii mhanga kinachofika ni nguvu yenye mitetemo (vibrations) ndio inayopiga
Baada ya hapo muuaji alitumia telekinesis /telepath kumnyanyua kumuingiza kwenye begi kufunga begi nk bila kugusa chochote
Telekinesis ni uwezo wa kuhamisha vitu bila kuvigusa

Jr
Mshana Chi power ni nini?
maana nimeanza kuliona hilo neno kwenye series ya Iron Fist sijaelewaga mpaka leo Chi power ni nini? Maana wanalitumia sana kUlingana na hio movie
 
Prince Mhando

Prince Mhando

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Messages
5,562
Points
2,000
Prince Mhando

Prince Mhando

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2014
5,562 2,000
Msisahau kuwa mtu anaweza kuuawa sehemu A na mwili wake ukaterekezwa sehemu B.....kumbukumbu za mauaji yake hufutwa taratibu eneo A kwa kuwa eneo B silo lililohusika wakati Wa mauaji kamwe and ever huwezi kupata chochote mwisho wa siku watu wanakuja na mambo ya kufikirika ya Asili au ulozi
 
S

said msuya

Member
Joined
Sep 22, 2016
Messages
51
Points
95
S

said msuya

Member
Joined Sep 22, 2016
51 95
Msisahau kuwa mtu anaweza kuuawa sehemu A na mwili wake ukaterekezwa sehemu B.....kumbukumbu za mauaji yake hufutwa taratibu eneo A kwa kuwa eneo B silo lililohusika wakati Wa mauaji kamwe and ever huwezi kupata chochote mwisho wa siku watu wanakuja na mambo ya kufikirika ya Asili au ulozi
Fafanua prince

Sent using Jamii Forums mobile app
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,611
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,611 2,000
Msisahau kuwa mtu anaweza kuuawa sehemu A na mwili wake ukaterekezwa sehemu B.....kumbukumbu za mauaji yake hufutwa taratibu eneo A kwa kuwa eneo B silo lililohusika wakati Wa mauaji kamwe and ever huwezi kupata chochote mwisho wa siku watu wanakuja na mambo ya kufikirika ya Asili au ulozi
Mkuu umeeleza vyema lakini issue hapa inakuja hata kama williams aliuawa eneo A na kutupwa eneo B (nyumbani kwake) bado utata unaanzia hapo kwa kuleta haya maswali.
1. Je aliingizwaje ndani ya jengo? Ilihali CCTV na uchunguzi haukuprove kuna watu waliingia kwenye jengo kwa hizo siku 3 alizokuwa haonekani ofisini. Let alone walikuta milango yote imefungwa kutokea ndani na hakukua na ushahidi kuwa milango ilichezewa wala madirisha!!

2. Je aliingizwaje ndani ya begi ilihali ushahidi wote unaonyesha begi limefungwa kutokea ndani na funguo ipo ndani ya begi ikimaanisha limefungwa na mhusika mwenyewe?

3.Hakuna jeraha lolote mwilini mwake kusuggest aliuawa ikimaanisha hakuvamiwa wala kupigwa na kitu kizito!!

4. Hakuna ushahidi kuwa aliuawa na sumu maana hata damu ilipopimwa haikuonekana kuwa na chembe zozote za kemikali inayoweza kuua.... Wala internal organ failure je alikufaje???

Haya maswali yote bila kujali aliuawa eneo A na kutupwa eneo B bado yaliacha utata ndio maana watu wakaingiza habari za "kufikirika".
 
Nanyaro Ephata

Nanyaro Ephata

Verified Member
Joined
Jan 22, 2011
Messages
1,003
Points
1,500
Nanyaro Ephata

Nanyaro Ephata

Verified Member
Joined Jan 22, 2011
1,003 1,500
Dark arts ni mafunzo ya hali ya juu ya ujasusi mara nyingi watu wenye IQ kubwa ndio wahusika
Kwenye majeshi husikia habari za makomandoo wenye weledi.Miongoni mwa mambo ambayo ni sehemu ya mafunzo ili uwe kamandoo ni pamoja na kuachwa nchi yake mbali unapewa passport tu!
Mfano unachukuliwa unaanchwa Australia unaachiwa paspoti tu na unapaswa kufika Tanzania
Ukifaulu ndio......
 
Papaa_Mobimba

Papaa_Mobimba

Senior Member
Joined
Mar 3, 2019
Messages
161
Points
500
Papaa_Mobimba

Papaa_Mobimba

Senior Member
Joined Mar 3, 2019
161 500
Nimejikuta nasisimka... Nina silika ya kuwatazama watu na kuwafahamu undani wao kabla hata hawajajitambulisha.. Sio ufahamu ule wa kuvaa la hasha.. Undani wao usiosemwa

Jr
Natamani sana Kuwa na Uwezo Huu!! Nifanyeje??

"Mopao Mokonzi"
 
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Messages
10,217
Points
2,000
Gama

Gama

JF-Expert Member
Joined Jan 9, 2010
10,217 2,000
Wakuu habari za mchana, natumaini wote wazima. Juzi nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha kuhusu mambo ya kijasusi cha "spies against armaggedon" humo nikakutana na term inaitwa DARK ARTS na katika kusaka maana zaidi mitandaoni nikakutana na case moja ya jasusi Gareth williams ambaye kifo chake kilihitimishwa kwa kusema aliuawa na mtu ambaye ni mtaalamu wa "dark arts" sasa kupitia case hii nategemea wajuzi wa hizi mambo mtusaidie je dark arts ni nini hasa kwenye tasnia ya ujasusi.

View attachment 854874
Tarehe 23 august polisi wa nchini uingereza walikuta mwili wa kijana kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ndani ya bafu ambaye baadae mwili huo ulitambulika kuwa ni wa Gareth williams ambaye alikuwa anafanya kazi katika shirika la ujasusi la uingereza SIS (MI-6) katika kitengo cha mawasiliano. Kifo hichi kiliacha utata na maswali mengi kwa polisi kwa jinsi tukio hili lilivyotokea hadi kupelekea kifo cha jasusi huyu.

WILLIAMS NI NANI?
Gareth Williams alizaliwa
mwaka 1978 nchini wales iliyomo ndani ya United kingdom, na alikuwa "kipanga" wa hesabu ambapo aliisoma kwenye chuo kikuu cha Bangor na kuhitimu kwa mean GPA ya 1st class akiwa na miaka 17 tu!! Na aliendelea na masomo hayo hadi ngazi ya PhD na baadae kuajirwa katika taasisi ya kijasusi ya mawasiliano (GCHQ) ambapo baadae aliongezewa na majukumu ya ujasusi kupitia shirika la SIS maarufu kama Mi-6 ambalo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za kiintelijensia nje ya uingereza.Kazi kubwa ya bwana williams ilikuwa kulinda mifumo ya mawasiliano ya shirika la ujasusi na serikali ya uingereza huku pia akifuatilia mitandao ya watakatishaji pesa duniani

KIFO CHAKE
Baada ya kutoonekana kwa masiku kadhaa, marafiki waliwajulisha police kuhusu hofu yao hivyo mchana wa 23, august 2010 police walienda kukagua nyumba aliyopanga bwana williams. Walipofika walikuta mlango umerudishiwa vizuri, vitu vipo organized, ila hawakumuona na walipofika bafuni wakakutana na kibegi cha aina hii
View attachment 854827

Walipofungua wakakutana na mwili wa Bwana williamson ambao ulikwisha anza kuoza na katika uchunguzi huo wa awali hawakukuta alama yeyote ya kuumia,kupigwa au kunyweshwa sumu ambayo ingeweza pelekea kifo chake.
Pia wakiwa hapo bafuni hawakuona alama ya vidole vyake au vya mwingine yeyote kwenye kitu chochote ndani ya bafu au apartment hiyo hapo ndipo utata ulipoanza.

UTATA KWENYE UCHUNGUZI
1.Mwili wa williamson ulikutwa kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ajabu ni kwamba funguo ilikutwa ndani ya begi kwenye mgongo wa william na pia zipu ilifungwa vizuri na kufuli na ushahidi wote unaonyesha zipu ilifungiwa kwa ndani ila bado hakukuwa na alama ya vidole ya williams na wala hakuwa amevaa gloves je iliwezaje kufungwa kwa ndani ilihali kufuli ipo nje na funguo ipo ndani??

2. Nyumba waliikuta haijachezewa kokote sio dirisha sio mlango sio bafu yaani kilakitu kilikuwa kwenye mpangilio wake hivyo kama kuna muuaji basi mlango ungevunjwa au dirisha ila baada ya uchunguzi ikaonekana hakuna sehemu yoyote ya kuingia "iliyochezewa"

3. Pia CCTV camera zilizokuwepo hapo hazikuonyesha mtu akiingia wala akitoka katika makazi hayo ikimaanisha alijiua mwenyewe.

LAKINI.....

4. Baada ya kuanza uchunguzi kama alijiua walishangaa kukuta mwili wake haukuwa na dalili ya sumu yeyote kwenye mwili wake au damu wala jasusi huyo kuishiwa hewa kabla ya kifo hivyo swali likaibuka je alijiuaje??

5. Wachunguzi wakahisi itakuwa alipoingia kwenye begi alishindwa kujitoa hivyo aliishiwa hewa au alipata "ajali" nyingine akafariki lakini walipojaribu kuingia kwenye begi kwa kutafuta ''mtaalam'' wa gymnastics ambaye ana asili ya mwili kama wa williams bado ilikuwa ngumu kufunga begi kutokea ndani hivyo lazima alikuwepo mtu wa pili ambaye alilifunga!!

ILA......

Kama mtu wa pili alimuingiza akiwa hai polisi hawakuona dalili ya williams kupambana kuokoa uhai wake kabla ya kufariki ndani ya begi na wala hawakuona alama ya mikono kwenye zipu upande wa ndani wa begi!!

Hivyo kama kuna mtu alimuua je alimuua kutumia nni?? Hawakuona sumu kwenye damu wala kovu wala ushahidi kwamba alipigwa na kitu kilichopelekea kifo?? Je hapa nini kilimuua??
View attachment 854910

TAARIFA MPYA YAIBUKA
Ilipofika mwaka 2015 alitokea jasusi wa kirusi ambaye alidai kuna majasusi wenzake wa kirusi walimuua Bwana williams kwa kumuingizia sumu kwenye sikio, lakini taarifa za Bwana huyu zilikosa ushahidi kabisa katika uchunguzi wa polisi na wataalamu wengine wa Mi-6 ukizingatia huyu jasusi alikuwa amekimbia urusi huku uingereza ikikataa kumchukua kwenye shirika lake la kijasusi wakiamini ni pandikizi hivyo taarifa zake zilipuuzwa maana walihisi anatafuta "kiki" ya kuaminika na kuingizwa kwenye shirika lao.

HITIMISHO
Ni kweli majasusi huwa wanatumia taaluma nyingi hata nyingine za kiroho maana kuna story za jasusi mmoja wa kiyahudi huko ufaransa aliyekuwa akipita mtaani ni kma upepo yaani hakuna anayejua kuwa kuna mtu kapita dakika hiyo na wala kwenye CCTV humuoni..... Sasa cha kujiuliza je dark arts inahusisha nguvu zingine za kiroho au ni mafunzo tu ya kiakili na kimwili ya hali ya juu ili kufanya kazi hizi za ujasusi kwa weledi?

Naomba kuwasilisha

cc Prof Richard Mshana Jr Malcom Lumumba Elungata ningeomba mpite huku
Nimebofya "like" usiache kunitag
 
Tychob

Tychob

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2013
Messages
1,450
Points
2,000
Tychob

Tychob

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2013
1,450 2,000
Mi ninachojua hata Marekani wanatumia nguvu za giza...Kipindi cha vita Afghanistan drones zilikuwa hazilipuki hata Al Jazeera walizionyesha sana.....Yaani midege ya kivita ya America ikirusha bomu halilipuki linatua hivyo hivyo kama lichuma tu watoto mitaani walikuwa wanayachezea.. Hata Osama alikuwa na hizo nguvu na zilimsaidia asikamatwe...Osama hakuuwawa na majeshi ya Marekani, bali alikufa kifo cha kawaida kwa ugonjwa wa homa ya matumbo...Ile ya Marekani ilikuwa movie tu ya kuihadaa Dunia
Hahahaha aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ChoiceVariable

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Messages
3,508
Points
2,000
ChoiceVariable

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined May 23, 2017
3,508 2,000
Ni rahisi mno, aliyefanya yale mauaji alikuwa ni mjuzi wa
Chi power (vital force)
Telekinesis na
Telepathy
Muuaji alichofanya ni kutumia CHI POWER Kuondoa uhai bila kumgusa mhanga.. Yani anarusha mkono lakini haumfikii mhanga kinachofika ni nguvu yenye mitetemo (vibrations) ndio inayopiga
Baada ya hapo muuaji alitumia telekinesis /telepath kumnyanyua kumuingiza kwenye begi kufunga begi nk bila kugusa chochote
Telekinesis ni uwezo wa kuhamisha vitu bila kuvigusa

Jr
Possible kwa sababu hata hao wanaojiita mitume na manabii wa kilokole wanawazubaisha waumini kwa nguvu hizi,wakilusha mikono yao watu wanaanguka huko
 
Blue G

Blue G

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
5,037
Points
2,000
Blue G

Blue G

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
5,037 2,000
Nasoma "Hitler and the secrete Alliance" jinsi gani Argentina walimsaidia or inawezekana alitorokea kwao!. Kuna kipindi majenerali wa UK na Germany walikuwa wanarequest kubadilishiwa tarehe za Navy attack kwa ajili ya kitu wanaterm 'superstitious belief'.
Nitaleta mrejesho wa hii mada mkuu, kuna kitabu flani cha Hitler's quest on Magical artifacts nadhani ndani yake ntapata hizi Dark Arts!. I will be back :).
mkuu Wick tag me please ukiileta kama tayari please kanitag kwa hiyo thread
 
Blue G

Blue G

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Messages
5,037
Points
2,000
Blue G

Blue G

JF-Expert Member
Joined Jun 20, 2012
5,037 2,000
Mkuu zitto junior mada yako ni fikirishi sana

na nimepitia kila comment humu na nimejiunza mengi

yapo yaliyoniingia na nimeyaunga mkono na yapo yaliyoniacha njiapanda na yapo ambayo hayaingii akilini hata kidogo

all in all nimeenjoy kusoma mada hii na comments husika

next time naomba unitag kwa thread kama hizi

Thanks mkuu
 
Forum statistics

Threads 1,326,268
Members 509,458
Posts 32,216,640
Top