Dark arts za intellijensia na utata wa kifo cha jasusi

zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,611
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,611 2,000
Wakuu habari za mchana, natumaini wote wazima. Juzi nilikuwa nasoma kitabu kimoja cha kuhusu mambo ya kijasusi cha "spies against armaggedon" humo nikakutana na term inaitwa DARK ARTS na katika kusaka maana zaidi mitandaoni nikakutana na case moja ya jasusi Gareth williams ambaye kifo chake kilihitimishwa kwa kusema aliuawa na mtu ambaye ni mtaalamu wa "dark arts" sasa kupitia case hii nategemea wajuzi wa hizi mambo mtusaidie je dark arts ni nini hasa kwenye tasnia ya ujasusi.

article-2122792-0d3205b9000005dc-252_306x491-jpg.854874

Tarehe 23 august polisi wa nchini uingereza walikuta mwili wa kijana kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ndani ya bafu ambaye baadae mwili huo ulitambulika kuwa ni wa Gareth williams ambaye alikuwa anafanya kazi katika shirika la ujasusi la uingereza SIS (MI-6) katika kitengo cha mawasiliano. Kifo hichi kiliacha utata na maswali mengi kwa polisi kwa jinsi tukio hili lilivyotokea hadi kupelekea kifo cha jasusi huyu.

WILLIAMS NI NANI?
Gareth Williams alizaliwa
mwaka 1978 nchini wales iliyomo ndani ya United kingdom, na alikuwa "kipanga" wa hesabu ambapo aliisoma kwenye chuo kikuu cha Bangor na kuhitimu kwa mean GPA ya 1st class akiwa na miaka 17 tu!! Na aliendelea na masomo hayo hadi ngazi ya PhD na baadae kuajirwa katika taasisi ya kijasusi ya mawasiliano (GCHQ) ambapo baadae aliongezewa na majukumu ya ujasusi kupitia shirika la SIS maarufu kama Mi-6 ambalo jukumu lake kubwa ni kukusanya taarifa za kiintelijensia nje ya uingereza.Kazi kubwa ya bwana williams ilikuwa kulinda mifumo ya mawasiliano ya shirika la ujasusi na serikali ya uingereza huku pia akifuatilia mitandao ya watakatishaji pesa duniani

KIFO CHAKE
Baada ya kutoonekana kwa masiku kadhaa, marafiki waliwajulisha police kuhusu hofu yao hivyo mchana wa 23, august 2010 police walienda kukagua nyumba aliyopanga bwana williams. Walipofika walikuta mlango umerudishiwa vizuri, vitu vipo organized, ila hawakumuona na walipofika bafuni wakakutana na kibegi cha aina hii
article-2122792-0b22502b000005dc-531_306x385-jpg.854827


Walipofungua wakakutana na mwili wa Bwana williamson ambao ulikwisha anza kuoza na katika uchunguzi huo wa awali hawakukuta alama yeyote ya kuumia,kupigwa au kunyweshwa sumu ambayo ingeweza pelekea kifo chake.
Pia wakiwa hapo bafuni hawakuona alama ya vidole vyake au vya mwingine yeyote kwenye kitu chochote ndani ya bafu au apartment hiyo hapo ndipo utata ulipoanza.

UTATA KWENYE UCHUNGUZI
1.Mwili wa williamson ulikutwa kwenye kibegi kidogo cha kubebea nguo ajabu ni kwamba funguo ilikutwa ndani ya begi kwenye mgongo wa william na pia zipu ilifungwa vizuri na kufuli na ushahidi wote unaonyesha zipu ilifungiwa kwa ndani ila bado hakukuwa na alama ya vidole ya williams na wala hakuwa amevaa gloves je iliwezaje kufungwa kwa ndani ilihali kufuli ipo nje na funguo ipo ndani??

2. Nyumba waliikuta haijachezewa kokote sio dirisha sio mlango sio bafu yaani kilakitu kilikuwa kwenye mpangilio wake hivyo kama kuna muuaji basi mlango ungevunjwa au dirisha ila baada ya uchunguzi ikaonekana hakuna sehemu yoyote ya kuingia "iliyochezewa"

3. Pia CCTV camera zilizokuwepo hapo hazikuonyesha mtu akiingia wala akitoka katika makazi hayo ikimaanisha alijiua mwenyewe.

LAKINI.....

4. Baada ya kuanza uchunguzi kama alijiua walishangaa kukuta mwili wake haukuwa na dalili ya sumu yeyote kwenye mwili wake au damu wala jasusi huyo kuishiwa hewa kabla ya kifo hivyo swali likaibuka je alijiuaje??

5. Wachunguzi wakahisi itakuwa alipoingia kwenye begi alishindwa kujitoa hivyo aliishiwa hewa au alipata "ajali" nyingine akafariki lakini walipojaribu kuingia kwenye begi kwa kutafuta ''mtaalam'' wa gymnastics ambaye ana asili ya mwili kama wa williams bado ilikuwa ngumu kufunga begi kutokea ndani hivyo lazima alikuwepo mtu wa pili ambaye alilifunga!!

ILA......

Kama mtu wa pili alimuingiza akiwa hai polisi hawakuona dalili ya williams kupambana kuokoa uhai wake kabla ya kufariki ndani ya begi na wala hawakuona alama ya mikono kwenye zipu upande wa ndani wa begi!!

Hivyo kama kuna mtu alimuua je alimuua kutumia nni?? Hawakuona sumu kwenye damu wala kovu wala ushahidi kwamba alipigwa na kitu kilichopelekea kifo?? Je hapa nini kilimuua??
hoodedmanknife-1-jpg.854910


TAARIFA MPYA YAIBUKA
Ilipofika mwaka 2015 alitokea jasusi wa kirusi ambaye alidai kuna majasusi wenzake wa kirusi walimuua Bwana williams kwa kumuingizia sumu kwenye sikio, lakini taarifa za Bwana huyu zilikosa ushahidi kabisa katika uchunguzi wa polisi na wataalamu wengine wa Mi-6 ukizingatia huyu jasusi alikuwa amekimbia urusi huku uingereza ikikataa kumchukua kwenye shirika lake la kijasusi wakiamini ni pandikizi hivyo taarifa zake zilipuuzwa maana walihisi anatafuta "kiki" ya kuaminika na kuingizwa kwenye shirika lao.

HITIMISHO
Ni kweli majasusi huwa wanatumia taaluma nyingi hata nyingine za kiroho maana kuna story za jasusi mmoja wa kiyahudi huko ufaransa aliyekuwa akipita mtaani ni kma upepo yaani hakuna anayejua kuwa kuna mtu kapita dakika hiyo na wala kwenye CCTV humuoni..... Sasa cha kujiuliza je dark arts inahusisha nguvu zingine za kiroho au ni mafunzo tu ya kiakili na kimwili ya hali ya juu ili kufanya kazi hizi za ujasusi kwa weledi?

Naomba kuwasilisha

cc Prof Richard Mshana Jr Malcom Lumumba Elungata ningeomba mpite huku
 
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Messages
31,833
Points
2,000
Elungata

Elungata

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2011
31,833 2,000
The Dark Arts of Espionage:
Typical training for an intelligence agent
includes but is not limited to: covert
surveillance, slight of hand, con-artistry,
manipulation tactics, personality-type
identification, lying, cheating, stealing,
trickery, camouflage, evasion, escape,
improvised weaponry, improvised self
defense, analytical combat, and espionage.
Part of intelligence training is instruction in
something called the "Dark Arts". The Dark
Arts are the espionage, trickery, con artistry
type stuff.
The Dark Arts are a social science that has
been developed through the detailed study
of proven experiments. Quite basically, a
study of what works, has worked in the
past, and is likely to work on a given mark.
The CIA undertook a detailed study of Con
Artists and their scams in order to derive
these methods. Top 10 Con-Men of Recent
History
Not everyone has what it takes to effectively
pull this off. It takes confidence and a good
amount of acting. It takes an artist who is
quick, versatile, and creative. But if studied,
practised, and perfected these methods can
and do work.
 
Samandarojk

Samandarojk

Member
Joined
Sep 25, 2016
Messages
54
Points
95
Samandarojk

Samandarojk

Member
Joined Sep 25, 2016
54 95
Utamu wa ngoma unaujua ukicheza.

Nimeangalia kwa makini hilo begi na kuangalia hao Northern face ni akina nani na wanafanya nini na wana bidhaa gani ?
Moja wapo ya bidhaa ambayo northern face wanaiuza ni sleeping bag( begi la kulalia)

Mabegi ya kulalia yapo ya aina nyingi kutegemeana na matumizi, na ni mabegi ambayo binadamu mwenye ukubwa wowote anaweza akaingia ndani akajifungia zipu na akajikinga na baridi(hali ya hewa mbaya) n.k. Haya mabegi yanatumika sana kwenye ma kempu, pia watu wanaolala kwenye tent lakini pia yanaweza yakatumika indoor ( ndani ya nyumba) kutegemeana na hitaji la mtumiaji.

Kwa muktadha huu, nimepata picha kuwa inawezekana muhusika aliingia kwenye sleeping bag peke yake bila kushurutishwa na mtu na ajali ikatokea, ingawa pia tujiulize hali ya hewa ilikuwaje wakati huo?

Pia inawezekana katika hilo begi kulikuwa na sumu au kuliwekwa aina ya sumu ambayo inaua kwa haraka sana na inapotea hewani kwa haraka sana bila kuja kugundulika kiurahisi.
Inawezekana pia hapo aliponunua begi au kama halikuwa jipya basi pale wanapoliosha wamehusika na wanajua mchezo mzima.

Nimewaza kingombaro ngombaro tu, sina ufahamu wa hayo mambo ila nipo tayari kukosolewa na kujifunza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko deep.
Lakini inasemekana jamaa alifungiwa na kufuli kwa nje na funguo zikiwa mgongoni ndani yake, na hakuna alama za vidole...
 
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Messages
10,590
Points
2,000
Richard

Richard

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2006
10,590 2,000
hapo kwa Sergio Ramos umetudanganya
Kwa vipi nimedanganya?

Mimi nimetoa maelezo yangu kuhusu Sergio Ramos kwamba anasifika barani Ulaya kwa kutumia dark arts.

Tafuta hizo facts zipo usiseme tu kiholela na kiujumla kwamba mimi ni mwongo .
 
Hum boy

Hum boy

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2014
Messages
445
Points
500
Hum boy

Hum boy

JF-Expert Member
Joined Sep 17, 2014
445 500
Kwenye martial arts dark art ipo ila mimi nitadadavua kidogo karate,kwa aliye advance karate kuna kitu tunaita msawazo wa AKILI,ROHO na MWILI una vicombine kua kitu kimoja ndio inazaa hiyo kitu inaitwa dark art ila kwenye karate tunaita CHI au INNER POWER kwenye GOJURYU KARATE hii unaipata vizuri ktk SANCHIN KATA na TENSHO KATA uki practice vizuri na MOKUSO/MEDITATION za mara kwa mara
 
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2011
Messages
7,148
Points
2,000
Ciril

Ciril

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2011
7,148 2,000
Kila Mtu alie bobea kwenye Anga zake ni lazima tumchukulie tofauti ,wengine watasema ni Miujiza wengine watasema ni Mchawi nk.

Nionavyo mimi Kazi ya Ujasusi ina kanuni zake ngumu sana kuzifuata kwa baadhi ya walio zichagua hizo Kazi.Wakati mwingine ni Michezo ya wao kwa wao ndani humo kwa maslahi mapana ya Nchi zao.Mbuzi amefia kwa Bwana Kheri hamna Kosa hapo.

Inawezekana tukasema na kutafsiri vyovyote vile kutokana na Mauaji yalivyo tekelezwa na Majibu ya Serikali ,Ukweli wanaujua wenyewe ndani ya Sistim huko.Binafsi nna aamini tumesha lishwa Uongo mwingi sana kuliko Ukweli ktk hii Dunia ..
 
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,664
Points
2,000
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,664 2,000
Hivi uchawi sio sayansi?

Juzi nilisikia BBC wakimuongelea jamaa mmoja huko njombe ambaye anatumia mbuzi kujilinda. Anasema kuna kitu (hirizi) alimmezesha huyo mbuzi. Hata namna mbuzi anavyolia ipo tofauti.

Kuna nyakati huwa nafikiria kuwa kile tunachoita "uchawi" pengine ni sayansi kabisa ila tu kwa sababu "hatujui" knavyofanya kazi.
 
Mwanambugulu

Mwanambugulu

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2017
Messages
512
Points
1,000
Mwanambugulu

Mwanambugulu

JF-Expert Member
Joined May 26, 2017
512 1,000
Kwa maoni yangu nadhani dark art ni sayansi inayohitaji umakini wa hali ya juuu sana na pia hufundisha au hutumiwa na watu maalumu katika vitengo maalumu tena kwa kazi maalumu kwa maslahi ya taifa au mtu flani

Dark art hutumiwa na aina tofauti za watu takupa mfano

Katika pita pita zangu siku moja nilijikuta niko mkoa wa tabora wilayani sikonge katika kata ya kitunda kuna sehemu wanapaita lukula kuna mambo mengi sana lakini kule ni polini na kuna Hifadhi za wanyama na pia kuna ujangili sana na wizi wa kutumia silaha pia katika vijiwe kupata story za hapa na pale nikakutana n.a. story ya jamaa mmoja ambaye aliwasumbua sana polisi unaambiwa huyo polisi walikua wanamtafuta hata kama mmekaa sehemu mnapiga story dakika tano kabla ya polisi kuja anaweza kusema aah mi nimechoka jamani naondoka pale anaondoka tu basi polisi hawa hapa tena wanataKA vibaya mno na wakimfatilia hawampati wakati wote mlijua jamaa leo ameisha

Katika kutaka kujua zaidi niliambiwa huyu jamaa ni kawaida yake sometimes anaweza kubeba silaha za hatari kama bunduki za hatari na akakutana na polisi lakini wakamuachia na wala wasione kama ni muhalifu lakini baada ta dakika kadhaa wanakuja kushituka kumbe wamemuachia waliekua wanamtafuta

Kwa kule ilisemekana jamaa no mchawi wa hatari that's why nakubaliana na wachangiaji pale juu kwamba dark art ina uhusiano wa karibu sana na ushirikina ingawa siwezi kua na majibu ya moja kwa moja

Serikali zetu hizi zote haya mambo nazani ndio kipaumbele cha kwanza kabla hata ya ulinzi wa kawaida

Hapo zamani kidogo kuna uzi uluongelea maswala ya ulinzi kidogo wa nchi na pia kulikua na mtaaaluamu wa maswala ya giza aliekua anatambuliwa na kiongozi wa nchi kuanzia nyerere paka mkwele ila jiwe sijapata data zake

So I think dark art ni neno smart tu la kutumia kuhalalisha upande wa pili
 
lauzi96

lauzi96

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2014
Messages
398
Points
1,000
lauzi96

lauzi96

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2014
398 1,000
Kuna vitu vingine huku uswahilini vinafanyika tunaona kawaida tu km hyo dark art kuna mshikaji mtaani akiwa hana kitu anaweza kuingia duka lolote akachukua vitu anavyotaka na akatoka bila kulipa hata 100 hila anasema mashart yake wanaouza wasimuone macho yake yaani macho yake na ya wenye duka yasikutane wakati anaingia hila Akishafika kwenye za kutundikia nguo anatia kwenye begi hata pair 20 na anaondoka bila kuwaangalia usoni na maduka yana camera.
 
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Messages
10,611
Points
2,000
zitto junior

zitto junior

JF-Expert Member
Joined Oct 7, 2013
10,611 2,000
Kuna vitu vingine huku uswahilini vinafanyika tunaona kawaida tu km hyo dark art kuna mshikaji mtaani akiwa hana kitu anaweza kuingia duka lolote akachukua vitu anavyotaka na akatoka bila kulipa hata 100 hila anasema mashart yake wanaouza wasimuone macho yake yaani macho yake na ya wenye duka yasikutane wakati anaingia hila Akishafika kwenye za kutundikia nguo anatia kwenye begi hata pair 20 na anaondoka bila kuwaangalia usoni na maduka yana camera.
Duuuh hii mpya hii
 
adden

adden

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Messages
4,836
Points
2,000
adden

adden

JF-Expert Member
Joined Dec 27, 2015
4,836 2,000
Write your reply...wanaposema jasusi anapita kama upepo haonekani kwenye cctv,haina maana kuwa kweli hupita pale kimazingara,hawa watu kabla ya kwenda kufanya tukio sehemu,wanastudy eneo na kuangalia camera ziko angle gani,kwahiyo anapopita anapita angle ambayo camera haitamnasa,na kama coverage ni ngumu kuikwepa wanahack mfumo wa cctv usiweze kunasa matukio kwa mda atakaoukua anaingia hadi kutoka mahali
Angalia hiyoView attachment VID-20181007-WA0009.mp4
 
Mbulajee

Mbulajee

Member
Joined
Jun 2, 2017
Messages
94
Points
125
Mbulajee

Mbulajee

Member
Joined Jun 2, 2017
94 125
KWA SISIS TULIOLELEWA KWENYE DINI ZOTE: uisilamu na ukiristo...PIA TUKAPELEKWA SHULE NJE YA NCHI...pia tukaishi maisha ya chini na tabu...halafu TUKAIBUKA UTADHANI TULIKUWA TUMEFICHWA KWENYE TANULU LA MOTO...tunayo majibu ya mnachozungumzia ILA HATUWEZI KUSEMA...by force by fire.
Duuuh hyo kali
 

Forum statistics

Threads 1,326,257
Members 509,458
Posts 32,215,955
Top