Dario: Mfalme mwenye haki aliyetawala huko Persia na kuwaruhusu Wayahudi kurudi makwao

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
KUHUSU miradi ya ujenzi aliyokuwa ameanzisha, mfalme mwenye kujulikana sana alijisifu hivi wakati mmoja: “Kwenye ukigo wa Babiloni nilifanyiza ukuta wenye nguvu katika sehemu ya mashariki. Nilichimba handaki la maji . . . nilijenga kwa lami na matofali ukuta mkubwa ambao, kama mlima, haungeweza kuondoshwa.” Ndiyo, Mfalme Nebukadneza wa Babiloni alikuwa amejihusisha katika mpango mkubwa wa ujenzi, na alikuwa amefanya kazi ngumu kulitia nguvu jiji kuu la milki yake. Lakini jiji la Babiloni halikuthibitika kuwa lisiloweza kushambuliwa, sawa na alivyodhania.

Ithibati ya jambo hili ilitokea Oktoba 5, 539 K.W.K. Akiungwa mkono na jeshi la Wamedi, mtawala Mwajemi Sairasi wa Pili alivamia Babiloni na kumwua mtawala wake Mkaldayo, Belshaza. Ni nani sasa angekuja kuwa mtawala wa kwanza wa jiji hili lililoshindwa? Nabii wa Mungu Danieli, ambaye alikuwa ndani ya mji huo ulipoanguka, aliandika hivi: “Dario, Mmedi, akaupokea ufalme, naye umri wake alikuwa na miaka sitini na miwili.”—Danieli 5:30, 31.

Dario alikuwa nani? Yeye alithibitika kuwa mtawala wa aina gani? Yeye alimtendeaje nabii Danieli, ambaye alikuwa katika utekwa katika Babiloni kwa zaidi ya miaka 70?

MFALME MWENYE HISTORIA HABA SANA

Habari za kihistoria juu ya Dario Mmedi ni haba sana. Yaelekea Wamedi hawakuacha rekodi zozote zilizoandikwa. Isitoshe, yale mamia ya maelfu ya mabamba ya kikabari yaliyofukuliwa Mashariki ya Kati, hutoa historia isiyo kamili yenye mapengo mengi. Maandishi mengine ya kale ambayo yamesalia ni machache, na yametenganishwa na matukio yanayohusianisha Dario kwa karne moja hivi au zaidi.

Hata hivyo, ushuhuda waonyesha kwamba baada ya kuuteka Hamadan, jiji kuu la Umedi, Wamedi walikuwa waaminifu-washikamanifu kwa mtawala Mwajemi, Sairasi wa Pili. Baadaye, Wamedi na Waajemi walipigana kwa umoja chini ya uongozi wake. Kwa habari ya uhusiano wao, mwandishi Robert Collins aandika hivi katika kitabu chake kiitwacho The Medes and Persians: “Katika amani Wamedi walikuwa katika kiwango sawa na Waajemi. Mara nyingi wao walikuwa wakichaguliwa kushikilia nyadhifa za juu katika serikali ya umma na vyeo vya uongozi katika jeshi la Waajemi. Wageni waliwaita Wamedi na Waajemi, bila kutofautisha washinde na washindi.” Hivyo Wamedi wakaungana na Waajemi kufanyiza Milki ya Umedi na Uajemi. —Danieli 5:28; 8:3, 4, 20.

Wamedi kwa wazi walitimiza sehemu kubwa katika kupinduliwa kwa Babiloni. Maandiko humtokeza “Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi” kuwa mfalme wa kwanza wa Milki ya Umedi na Uajemi kutawala Babiloni. (Danieli 9:1) Uwezo wake wa kifalme ulihusisha kuidhinisha amri ‘kulingana na sheria za Wamedi na Waajemi ambazo hazingebatilika.’ (Danieli 6:8) Yale ambayo Biblia husema kuhusu Dario pia hutuonyesha kifupi utu wake, kutia ndani na sababu yenye kusadikisha ya kukosekana kwa habari za ziada zinazomhusu.

Daniel alipendelewa sana na utawala wa mfalme Dario

Mara tu baada ya kuchukua utawala katika Babiloni, Dario aliweka “maliwali mia na ishirini, wawe juu ya ufalme wote,” Biblia yasema, “na juu yao akaweka wakubwa watatu, na Danieli alikuwa mmoja wao.” (Danieli 6:1, 2) Hata hivyo, cheo cha juu cha Danieli kiliwachukiza sana maofisa wale wengine. Uaminifu-maadili wake kwa wazi, ulielekea kuzuia ufisadi, ukielekea kutokeza uchungu wa moyo. Lazima maofisa hao wa cheo cha juu wawe walikuwa na wivu pia, kwa kuwa mfalme alimpendelea Danieli na aliazimia kumweka juu ya ufalme wote.

Wakitumainia kukomesha hali hii, maofisa hao wawili na maliwali walipanga njama za mtego wa kisheria. Walimwendea mfalme wakiomba sahihi yake juu ya amri ambayo ingezuia ‘kuomba dua kwa mungu awaye yote’ ila kwa Dario kwa siku 30. Walipendekeza kwamba yeyote ambaye angehalifu sheria hiyo angetupwa kwenye tundu la simba. Dario alifanywa aamini kwamba amri kama hiyo ingewapendeza maofisa wote wa cheo cha juu wa serikali, na pendekezo hilo lilionekana kuwa wonyesho wao wa uaminifu-mshikamanifu kwa mfalme.—Danieli 6:1-3, 6-8.

Dario alitia sahihi amri hiyo, na punde akaja kuyakabili matokeo yake. Danieli alikuja kuwa mhalifu wa kwanza wa sheria hiyo, kwa kuwa yeye aliendelea kusali kwa Yehova Mungu. (Linganisha Matendo 5:29.) Danieli mwaminifu alitupwa ndani ya tundu la simba, zijapokuwa jitihada nyingi za moyo mweupe za mfalme kutafuta namna ya kugeuza amri hiyo isiyobadilika. Dario alielezea usadikisho wake kwamba Mungu wa Danieli alikuwa na nguvu za kumponya nabii huyo.—Danieli 6:9-17.

Baada ya kukesha usiku kucha, Dario aliharakisha kwenda kwenye tundu la simba. Jinsi alivyofurahi kumpata Danieli akiwa hai na bila dhara lolote! Akitoa adhabu ya haki, mfalme aliamuru mara moja washtaki wa Danieli pamoja na familia zao watupwe ndani ya tundu la simba. Pia alitoa amri kwamba ‘katika mamlaka yote ya ufalme wake, watu watetemeke na kuogopa mbele za Mungu wa Danieli.’ —Danieli 6:18-27.

Kwa wazi, Dario aliheshimu Mungu wa Danieli na dini yake, na alitamani kusahihisha kosa. Hata hivyo, kuwaadhibu washtaki wa Danieli lazima kuwe kuliwafanya maofisa waliobaki kuwa wenye uhasama. Isitoshe, tangazo la Dario la kuagiza watu wote katika ufalme wawe wenye “kuogopa mbele za Mungu wa Danieli,” lazima liwe liliwasababishia viongozi wenye nguvu wa Babiloni uchungu mkubwa wa moyo. Kwa kuwa mambo haya bila shaka yalikuwa yenye uvutano kwa waandishi, haingeshangaza ikiwa maandishi yangebadilishwa kufuta habari inayohusu Dario. Hata hivyo, simulizi fupi kwenye kitabu cha Danieli humfanya Dario aonekane kuwa mtawala asiyependelea na mwenye haki.
 
Changamoto ya historia hii n kwamba inapingana na historia iliyopo ya uamed na uajem,

historia haimtambui kabsa mfalme dario badala yake inamtambulisha mfalme koreshi kama ndie alieingusha babeli na kutawala badala ya bltesheza sawasaw na utabr wa nabii isaya 44:22, 45:1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Changamoto ya historia hii n kwamba inapingana na historia iliyopo ya uamed na uajem,

historia haimtambui kabsa mfalme dario badala yake inamtambulisha mfalme koreshi kama ndie alieingusha babeli na kutawala badala ya bltesheza sawasaw na utabr wa nabii isaya 44:22, 45:1

Sent using Jamii Forums mobile app

Koreshi ndiye huyohuyo ambaye OP alimwita Sairusi.
 
Changamoto ya historia hii n kwamba inapingana na historia iliyopo ya uamed na uajem,

historia haimtambui kabsa mfalme dario badala yake inamtambulisha mfalme koreshi kama ndie alieingusha babeli na kutawala badala ya bltesheza sawasaw na utabr wa nabii isaya 44:22, 45:1

Sent using Jamii Forums mobile app
There was King Darius and then there was Darius the Mede, two different people. And then Belteshazzar was not a King of Babylon but a regent, ruling on behalf of his father Nebonidas who was the real last king of Babylon.
 
Back
Top Bottom