Dareva wa Naibu Jaji Mkuu apigwa risasi Kenya...

Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,642
18,643
Dereva wa naibu jaji mkuu wa Kenya
Philomena Mwilu amepigwa risasi na
kujeruhiwa na watu wasiojulikana mjini Nairobi. Dereva huyo anayejulikana kama afisa wa polisi Titus Musyoka alipigwa risasi nje ya jumba la Marsabit Plaza katika barabara ya Ngong. Afisa mkuu wa polisi eneo la Dagoretti Rashid Mohammed alisema kuwa kisa hicho kilitokea mwendo wa saa kumi na nusu jioni na jaji Mwilu hakuwepo katika gari hilo. Alisema kuwa dereva aliyejeruhiwa alipigwa risasi katika bega na anapatiwa matibabu katika hospitali moja ya mjini Nairobi. Amesema kuwa maafisa wa polisi wanakichukulia kisa hicho kuwa cha ujambazi lakini uchunguzi unaendelea. Tayari maafisa wa uchunguzi wamefika katika eneo
hilo.
 
Taarifa zinaeleza kuwa gari hiyo ilishambuliwa Leo na DREVA kujeruhiwa, Naibu jaji mkuu hakuwemo kwenye gari hiyo.

Hii inakuja masaa machache kabla ya kuanza kusikilizwa kesi za kuzuia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo tarehe 27/10/2017 kutokana na kile kinachoelezwa kuwa Tume ya uchaguzi kutokujipanga vyema kuendesha na kusimamia uchaguzi huo.
 
Hili ni jambo la kawaida sana kwa Kenya, hawajakosea kuiweka Kenya katika Kundi la failed states, Juzi wamemuua Kenyama yule Pandre kule kisumu baada ya kumkosoa Kenyatta kwa kuwauwa wajaluo, na hakuna hata mtu mmoja anayeongelea kifo chake, wakenya wamezoea kuuwana kama wanyama, Kenya means;
1)Tribalism
2)Corruption
3)Insecurity

Kama njaa ikiendelea for the next 3 years, nayo itaingizwa katika orodha hii
 
Kwenye siasa kuwashwa risasi ni jambo la kawaida sana...unaziba maslah ya watu alafu wakuache mzima mzima...dhubutu
 
Kwa kweli dereve wetu arudi tu asije shambuliwa tena huko Nairobi maana kumbe nako sio salama.
 
Taarifa zinaeleza kuwa gari hiyo ilishambuliwa Leo na DREVA kujeruhiwa, Naibu jaji mkuu hakuwemo kwenye gari hiyo.

Hii inakuja masaa machache kabla ya kuanza kusikilizwa kesi za kuzuia uchaguzi mkuu wa nchi hiyo tarehe 27/10/2017 kutokana na kile kinachoelezwa kuwa Tume ya uchaguzi kutokujipanga vyema kuendesha na kusimamia uchaguzi huo.
Mgonjwa wetu Lisu atapona kweli?
 
Back
Top Bottom