Dare to use Your own Mind

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Elimu yetu ya sasa ni kama chupa tatu kubwa; Moja ya nusu lita, nyingine ya lita moja na nyingine ya lita mbili. Zote hizi baada ya kujazwa maji kiwandani zilifungwa vizibo.

Chupa hizi ni maarifa tunayowapa watoto wetu kuanzia shule ya msingi, sekondari na chuo kikuu. Ili tuendelee kama taifa ni lazima tufungue vizibo hivi.

Ni lazima elimu yetu ielekezwe kukuza ufikiri watoto wetu na sio kumwingizia maarifa kama maji yanavyojazwa kwenye chupa na kufungwa. Ni lazima ielekezwe kwenye kukuza ufahamu wao.

Kwa njia hii pekee watu wetu watakuwa wabunifu na wagunduzi. Ni muhimu kutokutengeneza watu wa kulishwa maarifa bali watu wanaofikiri.

Hatuwezi kuendelea katika misingi ya elimu ya namna hii. Kuendelea kwa binadamu ni kukua kwa akili zake. Watu wanaofikiri ndio wanaounda mifumo na kugundua na kutengeneza dunia tunayoona kwa sasa.

Fikiri Fikiri Fikiri, tumia ubongo wako mwenyewe... Usikubali mtu afikiri kwa niaba yako... Shule zilijengwa na watu wanaofikiri wakawa wana wafuasi waliyatafuta maarifa kwa nguvu na jasho na nidhamu ya hali ya juu.

"Dare to use your own mind" Be a master and not a disciple.

Elimu yetu lazima ifundishe watu wetu watumie akili yao wenyewe....And that is true freedom.

Ni muhimu kufahamu hata mbwa anaweza kufundishwa lakini binadamu ni lazima afikiri na aendelee kukua katika fikra. Ni kwa kukuza fikra za watu wetu tu ndipo watu wetu watakuwa wenye maarifa na wazalishaji.

Kwa njia hii pekee tutajenga jamii yenye busara na maarifa.

Popote ulipo tumia uwezo wako wa kufikiri kuna nguvu katika uwezo wa kufikiri, kumtegemea mtu mwingine kwa fikra ni utumwa ambao hautatufanya tupige hatua kama mtu na kama taifa. Tutajitegemea kama taifa tutakapo jitegemea kifikra.

Shaabany@yahoo.com: Note from the book ''KIU YA UZALENDO''
 
Mkuu, Ulaya iliendelea baada ya kukua kwa elimu ya falsafa ya uwezo wa kufikiri (Epistemology).
Bila kufikiri hakuna ugunduzi (innovation) wa mambo mapya.
Ninapendekeza somo la falsafa lianze kufundishwa toka shule za msingi, sekondari hadi vyuoni na liwe somo la lazima (compulsory),
Hii itasaidia sana kukuza uwezo wa kufikiri.
 
Ni vyema! Kwa kuongezea pia, nje ya somo darasani bado tunahitaji kuwa-condition watoto wetu katika mazingira ya kila siku kufikia huko tunakotaka! Wasikie kipi na kipi marufuku! Watake kipi na kipi marufuku! Waone nini na kipi marufuku! Watamke kipi na kipi marufuku! Wacheze nini na nini marufuku! Wavaaje! Kiujumla, how should they behave-ni lazima KUSUKWE hasa, kufika ukomavu wa fikra zao!
Leo hii mashuleni na mavyuoni mwenye akili ni yule anayeweza kukariri majina mengi ya theory za watu na kuzielezea! Ndio wasomi hao! Leo, mtoto kila akifungua redio anachosikia ni matangazo ya Show za muziki, dansi, mpira, na udaku. Akifungulia TV, anachoona ni Utupu wa wasanii wetu, mambo ya faragha, umagharibi, n.k. Akisoma gazeti ni udaku udaku kila kona! Akiwa anaenda shule, tangu ndani mwao mama yake kava kimini na dada zake viguo vya kulalia, njiani mtaani nusu uchi wamejaa kibao, had shulen mwalimu wake ameacha mpasuo! Hakuna kanuni wala sheria kuhoji hayo, eti UTANDAWAZI-UHURU! Pumbavu! Ni AJE TUTAPATA FIKARA BORA HAPO!? TUNAHITAJI KUKAA CHINI HASA! Hizi ni HESABU! Mkuu wangu Shayu nakupata!
Mungu wetu anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:

Be blessed.
 
Mkuu JingalaFalsafa,

Umenena vyema na natumai kuwa maoni yako hayo ni katika kutaka kujenga taifa linalofikiri.

Katika maoni yako umejikita sana katika suala la maadili kulingana na mila na tamaduni zetu, na umeziweka katika mfumo wa "DO's and DONT's", kwamba kuwe kuna makatazo katika mienendo ambayo inakwenda kinyume na mila na tamaduni zetu.

Nakuunga mkono kwa asilimia zote katika suala zima la kulinda maadili kutokana na desturi zetu.

Lakini kama ni kweli tumedhamiria kujenga jamii inayofikiri ni vyema sisi kwanza tukaanza kufikiri. Kwa mfano kutokana na mchango wako huu tunaweza kujiuliza yafuatayo;

Je, namna ya mavazi, kuongea, udaku n,k n,k vinaweza kusababisha watu wasiweze kufikia ukomavu wa fikra?

Ni kweli kuna baadhi ya mila na desturi huwa zinaashiria ufinyu wa fikra katika jamii husika,

Je, umagharibi kama ulivyouita ni kikwazo katika kufikia ukomavu wa kifikra?

Mimi sio mtetezi wa umagharibi hata kidogo ila huwa ninajiuliza ni kwa nini hao wamagharibi wamepiga hatua kubwa kimaendeleo kutokana na ukomavu wa kifikra walionao, pamoja na umagharibi wao ambao sisi huku tunaupiga vita, sina nia ya kukukwaza mkuu ila tu ni katika hali ya kujaribu kufikiria.

Tunatakiwa tutafute kizingiti hasa cha ni kwa nini tunashindwa kujenga jamii inayofikiria, Migogoro ya udini kwa mfano,
ni miongoni tu mwa dalili za kuashiria jamii isiyofikiria.
Ninakubaliana na wewe kwamba kuweza kukariri majina mengi ya theory za watu na kuzielezea sio usomi, ila ni hatua moja muhimu ya kuelekea usomi.

Mtu anahitaji kuelewa mawazo ya mwingine ili kufahamu alipoanzia na alipoishia ili na wewe uendeleze pale alipoishia.

Kuna mfano wa wanafalsafa wa ugiriki ya kale( ancient Greece) waliokuwa wanaendeleza fikra za kila mmoja kila pale anapoishia(advancement of thoughts).

Their names were Thales, Anaximander and Anaximenes.
Thales who lived between 624 and 546 BC distinguished that all living things, although they differ they all have a basic similarity for each and everyone and that resemblance unites them despite of their difference.

Thales thought that what unites everything despite the difference upon them is WATER.

According to these thoughts there was a general believe in Greece that water was a source of everything.

Thales's student known as Anaximander agreed with his teacher that there must be something which is a source of everything but this thing must have no boundaries ie, it should be limitless.

Anaximander commented that, the source of everything must be limitless and he said it should not be WATER, and he just ended up like that without mentioning what is that " Limitless''.

Another philosopher, who is a student of Anaximander, Anaximenes agreed with his teacher that the source of everything must be limitless, and mentioned AIR, due to the fact that air is the fundamental unit of life in everyliving thing, and if a living thing lacks air, it dies.

Other philosophers like Democritus, Leccippus etc, discovered the source of all things to an ATOM.
 
Nimekupata Mkuu wangu Mjuni Lwambo. Nakupata vyema, na ninashukuru!

Tatizo si watu kutofikiri, WATU WETU WANAFIKIRI TENA SANA! Swali, je WANAFIKIRI NINI? Je, FIKRA ZAO NI SAHIHI AMA MFU! Hadi kufikia hatua ya kulalamikia Fikra zetu, ni wazi zi MFU hazitusaidii chochote, vijana huwa tunasema HAZITUTOI! Je, zipi ni FIKRA ENDELEVU KWA TAIFA HILI? Je, zinakuja 'automatically' vichwani mwetu, au zinawezeshwa?

Binafsi ninaamini wazi kabisa kuwa FIKRA BORA hujengwa na mazingira kwa watoto wetu! Ndipo hapo ninaposema kuwa ni lazima TUIFUNGE milango yao yote ya fahamu kuingiza kile tu kitakachomuwezesha kuwa na fikra bora na si mfu! Kwa bahati mbaya hapo nilitoa mifano ya kitamaduni mingi, lakini suala la KUJENGA FIKRA BORA kwa watoto wetu haliishi hapo tu! Ni pamoja wakishuhudiacho katika Siasa, Uchumi na Mazingira katika jamii zao!

Chukulia mfano wa tukionacho leo, tofauti iliyopo kwa wanasiasa na raia wa kawaida, mtoto atakua akiamini kabisa siasa ni ulaji, na atajikita huko kufanikisha hilo tu, FIKRA MFU! Ona leo mtaani wenye nazo na sie wakina baba kabwela, jamii inaona ni sawa! Watoto nao wanajenga fikra kuwa kumbe ni halali kuwa na matabaka, na hawezi kuwakumbuka wa chini yake pale anapopata kanafasi nae!

Laiti kama kungekuwa na walau taratibu za kukemea taratibu kama hizo, vichwani mwao nao wangewaza na fikra kuwa KILA MTU ANA WAJIBU JUU YA USTAWI WA MWENZAKE-ndizo FIKRA tulizokosa!

Kama anashuhudia mkandarasi wa nje akithaminiwa kuliko yeye, kwanini asifikiri kuwa chochote bora ni kutoka nje? Kama anashuhudia aliyesoma nje ndio anayepewa kipaumbele, ataiwaziaje elimu yake ya St. Kayumba? Kama anashuhudia, wagonjwa sawa wa malaria wakilazwa wodi mbili tofauti mwingne Grade A na yeye kule kwa 'Kina kajamba nani', tena kwenye hospitali ya umma, kwanini nae asitamani hata kuibia nchi apate ukuu huo? Je, tunafahamu ni kwa kiwango gani ni kikwazo kwa ustawi wetu(FIKRA BORA)?

Mkuu wangu, fikra bora ni zile zenye kusadifu mazingira na nyakati za eneo husika, ni kwa kiwango kidogo tena sana chini ya 3% tunafanana na wa magharibi si tamaduni, sura ya nchi, watu, historia, (ikumbukwe pia science and technological advancement haitofautishi umagharibi na uafrika wetu, bali ni the way tunavyoyachukulia hayo mabadiliko ni LAZIMA TUTOFAUTIANE), movements zetu leo hazijali hilo.

(dharura kidogo, nitarudi Mkuu wangu)
 
Last edited by a moderator:
Nakubaliana na wewe JINGA LA FALSAFA ni muhimu kuangalia fikra za watu wetu wanalishwa nini kutoka kwenye media. Ni muhimu ili kujenga fikra zao.

Udaku hauwezi kujenga fikra za watoto wetu au jamii yetu.
 
Mkuu wangu Mjuni Lwambo, kama nilivyoanza kusema hapo juu kuwa, tunaposema umagharibi ni mifumo, mifumo ya uchumi wao, mifumo ya siasa zao na mifumo ya tamaduni zao!

Mifumo yao ni sahihi kuwafikisha walipo KWASABABU NI YA KWAO! Imezaliwa kutokana na Mazingira na Nyakati zao wenyewe! Hivyo umagharibi uko suitable hukohuko kwao magharibi, kamwe usitarajie kuuleta huku kwetu na kuzaa matunda yaleyale, HAIWEZEKANI MILELE! Umagharibi kwetu ni UTEGEMEZI kwani hakusadifu chochote kwetu, kwa namna yoyote ukitaka uendelee kuwepo ni lazima UWATEGEMEE WAO! Na hicho ndicho kinachotugharimu leo! Na hizo ndizo FIKRA MFU!

Watoto wetu wanajengwa katika ku-copy and paste umagharibi huo katika maisha yetu huku! Hayo yanafanyika katika harakati zetu za kila siku, serikali, mitaani, mashulen, kanisani, misikitini, sokoni, n.k. Mazingira na Nyakati zetu ni tofauti kabisa na hiyo mifumo pandikizi, ndio maana haiishi kupandikiza UNYONGE WETU! Vile vile, ukitaka kuona kwamba mifumo hii ya kimagharibi si lolote si chochote, embu jaribu kuwaza na IFUTE AFRIKA KUTOKA USO WA DUNIA, TAZAMA ULAYA NA MAREKANI, JE ZITASIMAMA KATIKA UTULIVU ULIOPO LEO CHINI YA MIFUMO YAO HII HII? THUBUTU YAO! Wataanza na vita vya wenyewe kwa wenyewe mwishowe taifa kwa taifa, wakimbizi, magonjwa, umasikini, watoto wa mtaani watajaa vile isivyo kwetu leo!

TUSIDANYWE NA HILA ZAO LEO, UWEPO WA MAGHARIBI VILE ILIVYO LEO UNATEGEMEA SANA UNYONGE WETU! Fikra mfu ni kufikiri kuna cha mzungu chochote kututakia mema!

Mavazi, Maongezi na Udaku katika kuathiri Fikra zake mtu, fikiria mapaja nje, vipindi vya mahaba, aje mtoto asitumie muda wake mwingi kuwaza ngono? TATIZO SI KUFIKIRI BALI TUNAFIKIRI NINI! Atapata muda gani kufikiri changomoto katika maendeleo yetu wakati kila siku anawaza show za muziki atapataje kiingilio! Chunguza japo kidogo, wangapi nguo zao zina japo picha ya ramani yetu ama waasisi, linganisha na wangapi wamevaa akina Ronaldo, Obama, NYC, n.k kaa nao karibu chunguza maongezi yao! Mtu hutumia muda mwingi zaidi kuwaza na kuathiriwa na kile kinachomzunguka kila siku, akizungukwa na upuuzi (umagharibi) atawaza kimagharibimagharibi, HAKUTUTOI.

Angalizo:
Kamwe tusipotoshe, maendeleo ya sayansi na teknolojia si umagharibi, tunaweza kutumia nyenzo hizo kwa namna yetu wenyewe, si vile tu watakavyo wao! Na FIKRA BORA ni zile zitakazohusisha kwanza maendeleo hayo na Mazingira na Nyakati zetu kwanza, na kuona namna bora ya kutumia kabla ya kuyafakamia.

TUNATAKA KIZAZI KIPYA CHA FIKRA! Kile kitachobuni Mifumo na taratibu mahususi kwa uendelevu wa taifa letu Afrika! Si kazi rahisi, lakini TUNAWEZA! Ubunifu haujawahi kufika mwisho! Nguvu yetu ni Umoja na Kuthubutu!

Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Last edited by a moderator:
Nimepata fursa ya kukusoma vizuri hii leo. Na hiyo ndio inayoitwa Mind revolution.
 
Naomba niongezee hili!
Fikra za kwamba MTU MWEUSI ni MTU DUNI, anayestahili kunyonywa, kutumikishwa, kuburuzwa, kutawaliwa, kunyanyaswa, kufanyiwa maamuzi, n.k kama vile tuwaonavyo kuku wetu nyumbani kwa kitoweo, ndizo zilizo zilizojikita vichwani mwa ngozi nyeupe, "YOYOTE". Fikra hizo kwa kuhusianisha na mazingira yao, ndizo zilizozaa mifumo ya kuendesha maisha yao! Ndio maana tunapaswa kulaani hii copy and paste style! Stori tulizonazo kuwa, watoto wa kizungu huwasugua weusi ngozi wakijua tumejipaka rangi(ndio mafundisho wanayopata tangu utoto) au majukwaani wachezaji kuitwa manyani, ni sehemu ya TAMADUNI zao sio kwa bahati mbaya, na hawajawahi kuwaza tofauti na hivyo!
AFRIKA! Ina MAZINGIRA na NYAKATI zake, mahususi kwa eneo lake na vilivyomo! Iwe sheria, sera ama mfumo zaliwa kwetu, ni LAZIMA ISADIFU NYAKATI NA MAZINGIRA YA AFRIKA! Nje ya hapo ni UNYONGE UNYONGE KILA KONA! Mzungu kumnyonya mwanawa-afrika, ni sehemu ya imani yao juu ya hata Mungu wao!

Umenena vyema mkuu swali tufanyaje ili tuondokane na hii hali na kuleta kujiamini kwetu kama waafrika na kama watanzania?

And though the philosopher may live remote from business, the genius of philosophy, if carefully cultivated by several, must gradually diffuse itself throughout the whole society, and bestow a similar correctness on every art and calling. (David Hume, 1737)
 
...
Udaku hauwezi kujenga fikra za watoto wetu au jamii yetu.

kuna waandishi, nadhani wa gazeti la mwananchi, walidai kupitia gazeti lao kuwa udaku una boresha afya.....nilisikitika sana.

NIKIRUDI KWENYE MADA

Mazingira ya kumuandaa mtoto/mwanafunzi kuwa na uwezo wa kufikiri lazima yaandaliwe vema na nyenzo za kumuwezesha kufanikisha kile anachokifikiri kilicho chema kwake na kwa taifa zina takiwa kuwepo. Kwa mashuleni hata vyuo vikuu lazima viwepo vifaa bora na husika, walimu wenye utaalamu na weledi uliotukuka kumuwezesha mwanafunzi kutimiza malengo yake na taifa kwa ujumla na mengine kama haya.

kwenye walimu...hapo ni pa muhimu kweli.....nakumbuka wakati nina soma nilikuwa na wazo langu la mradi ambalo lilikuwa la kibunifu. Kipindi hicho,nadhani mpaka sasa, suala la mradi ilikuwa sehemu ya kukamilisha masomo yako kwa mujibu wa silabasi/mtaala husika. Hivyo ilikulazimu ufanye/ukamilishe mradi ndipo utakapotunukiwa cheti cha kuhitimu masoma. Basi, nilimshirikisha mwalimu wangu juu wazo langu hilo la mradi. Nashukuru alinisikiliza vizuri wakati nampa maelezo ya mradi huo. Baada ya kumpa maelezo yale,kwa kifupi , alinieleza kuwa kama wazo hilo/mradi huo haujawahi kufanywa popote... basi niachane nao maana nitakosa sehemu ya kuangalizia/nukuu taarifa/maandishi juu ya wazo la mradi huo.Sikuwa na namna niliachana na wazo hilo. Mpaka hapo unaweza kuona namna baadhi ya walimu wanavyofifisha nia ya wanafunzi kufikiri.

Binafsi suala la kujenga fikra za watoto wetu au jamii yetu naliona kama suala mtambuka, hivyo lina hitaji ushirikiano na ushirikishwaji wa wadau wote katika jamii.
 
Kuendelea kwa taifa lolote hutegemea sana nguvu kazi iliyo nayo, nidhamu na elimu mahsusi kuleta maendeleo jamii inayo yahitaji kwa ujumla, ili kufanya taifa liendelee.
Misingi ya elimu hii lazima ijengwe katika kuendeleza taifa na si vinginevyo. Ni lazima ijengwe katika misingi ya uzalendo, nidhamu na wajibu.

Taifa linapofundisha mtu si kwaajili yake tu, bali ni kwaajili ya taifa, ni kwaajili ya maendeleo ya wote. Ni kwaajili ya watu wote wapate uelewa utakaosaidia katika ujenzi wa taifa imara. Kuendelea kwa taifa lolote hutegemea sana nguvu kazi iliyo nayo na elimu mahsusi kuleta maendeleo jamii inayo yahitaji kwa ujumla, ili kufanya taifa liendelee.

Watu wote watakapopata uelewa ndipo ukombozi wa kweli utakapopatikana. Uelewa huu ni muhimu kwa ukuaji wa taifa. Kuishi katika ujinga ni sawasawa na kuishi katika kiza kinene, ni elimu pekee itakayotutoa katika kiza hiki.

Na elimu hii ni lazima iende kwa watu wengi zaidi ili wapate kujielewa. Kwakuwa pasipo kujielewa huku hatutaweza kujenga taifa hili. Ni kwa kujitambua huku pekee tutaweza kujenga jamii iliyobora, pasipo kujitambua huku hatutaweza kuondoa ujinga.

Lakini misingi ya elimu yetu ya sasa haisaidii kujitambua huku kwa watu wetu kwa taifa lao ndio maana watu wanapata maarifa ya kazi lakini ujinga wanaendelea kuwa nao NA UFAHAMU WAO kwa taifa lao unakuwa finyu. Hawajui kwanini sisi ni taifa na wala hawana uzalendo wa kulijenga.

Kujitambua huku ni kufanya mambo ambayo ni yenye faida kwa jamii na kwa mtu husika. Kujitambua huku ni kutumia uwezo wa kiakili kujizuia na kuongozwa na fikra. Ni kujua asili ya binadamu ni fikra na nje ya fikra huwezi kumtofautisha na mnyama. Pasipo kuongozwa na fikra na kuchagua kilicho bora kwa faida yetu kama taifa tutasemaje tumeelimika?

Elimu hii ni lazima iwe na uwezo wa kujenga mahusiano yetu na kufanya taifa liwe na dira moja.

Ni nini faida ya elimu kama sio kutengeneza mwenendo wa binadamu kadiri inavyowezekana kuwa bora na wenye faida kwa umma?

Tuangalie elimu yetu ya sasa ilivyoundwa je ina mjengea mwanafunzi nidhamu na wajibu katika jamii na taifa lake? Je inamjengea uzalendo? Je inatengeneza mienendo ya namna gani kwa wanafunzi? Je inampatia maarifa ya kazi ya kutosha ambayo yameambatanishwa na mapenzi na uzalendo kwa taifa?

Je inaonyesha ubora wetu katika kuzalisha na katika tabia zetu na mienendo yetu?

Elimu yetu lazima ifundishe watu kutumia akili yao wenyewe. Tutafanya mapinduzi makubwa kama watu wetu watakuwa na uwezo huu, elimu yetu ni lazima iwe katika kukuza akili na sio kumwingizia maarifa mtoto kama maji yanavyojazwa kwenye chupa na kufungwa, kwa kufanya hivyo tunafunga ufahamu wao. Ukuzaji wa akili za watoto wetu ndio lengo kuu ya elimu. Tukikuza ufahamu huu ni hatua moja kubwa kwetu kuendelea. Ni lazima iunde watu wetu katika uzalendo,nidhamu na maadili...Ni lazima tutengeneze akili za watoto wetu katika mkondo fulani, akili zilizotawanyika kamwe hazitojenga kitu.

Kutengeneza akili za watoto wetu katika mkondo fulani ndio nidhamu yenyewe ambayo ni muhimu sana kwa ukuaji wa taifa lolote na kujitambua kwake. Watu wetu ni lazima wawe na mwelekeo na taifa lao.

Ni lazima tujielewe sisi ni watu wamoja na elimu yetu tunayotoa kwa watu wetu ni maalum kwaajili ya ujenzi wa taifa hili na ni kwaajili ya ukombozi kwa watu wetu dhidi ya ujinga.

Je ujinga tutautoaje? Ujinga ni kufanya mambo yasiyo sahihi. Kupata maarifa ya kazi tu sio tiketi ya kukufanya wewe uwe umeelimika. Ili tuseme tumeelimika ni lazima tuwe na watu wanaofanya mambo yaliyo sahihi kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla ndio maana nasema ni lazima iunde tabia zao pia. Ili uwe ume elimika ni lazima utumie akili zako vizuri na uwe mwenye manufaa kwa umma. Namaanisha uwe mwenye msaada kwa taifa. Utumike ipasavyo kuleta manufaa katika taifa sio kulibomoa.

Hivi ndivyo tutakavyo jenga taifa kwa kujitolea. Tukitaka kujenga jamii yenye furaha ni lazima tufanye mambo haya. Bila ukombozi huu dhidi ya ujinga kwa watu wetu wengi zaidi, hatutaweza kuendelea wala kuondoa uhalifu nchini. Kwahiyo ni lazima tuwe na watu walioelimika na waliotayari kujitolea kulijenga taifa hili ndio maana mataifa yanawapa elimu watu wao. Lakini wale wanaoitumia vizuri katika uzalendo, wajibu na kujitolea kuona taifa lao likiendelea ndio waliopiga hatua. Sisi elimu yetu imejengwa katika ubinafsi.

''Ni katika kujitolea huku sisi kama taifa tutapiga hatua za kimaendeleo. Kwahiyo ni lazima elimu yetu ibadilike ilenge katika kujenga taifa badala ya kuelimisha watu kwa manufaa binafsi. ''

Suala la ajira kwa watu wetu litamalizwa ikiwa watu wetu watapata maarifa ya kutosha yatakayo -wafanya kujitegemea. Ni katika msingi huu wa kutoa maarifa yatakayomfanya raia kujitegemea nchi yetu itapiga hatua kimaendeleo.Ni lazima elimu yetu ijengwe katika misingi hiyo. Ni lazima tutoe elimu bora itakayowafanya watu wetu kujitegemea na kuwa wazalendo na wawajibikaji kwa taifa.

Pamoja na kuwapa elimu ya stadi za kazi tabia pia ni muhimu kujengwa kwakuwa bila tabia bora hatutakuwa na nguvu kazi nzuri katika taifa letu. Ni lazima tujiulize ni tabia gani tujenge kwa watoto wetu ambazo zitakuwa chachu ya maendeleo yetu kama taifa?

Ni mambo gani watoto wetu wajiepushe nayo na ni yapi wayafuate ni lazima tuangalie hapa kwakuwa pasipo kujenga tabia bora za watoto wetu baadae ya taifa hili itakuwa gizani.

Kuwaachia vijana wetu kujiingiza katika starehe za kupindukia sio jambo jema kwa ukuaji wa taifa letu. Jambo hili huondoa uwajibikaji na utiifu wa vijana na huondoa uwezo wao wa kufikiri sawa sawa. Kwahiyo maadili ni jambo la msingi kwa ukuaji wa taifa na hatutaweza kujenga maadili hayo kwa kuwaacha vijana kutopea katika starehe.

Tunahitaji kujenga raia wawajibikaji kwa taifa lao, wazalendo na shupavu. Kwa njia hii pekee tutapata mwelekeo kama taifa. Kujitolea huku kwa vijana kwa taifa lao kutaka kuona likinyanyuka na kupata heshima katika mataifa ni roho ya kweli ya ukombozi. Tunahitajika kujenga roho hii kwa kila raia. Watoto wetu lazima wakue wakitambua wanawajibu huu muhimu ni lazima wawe na mahaba kwa taifa lao. Mwanamke asiyejipenda hawezi kujipamba, Taifa ambalo watu wake hawajawekeza hisia zao kwake litavutiaje?

Kwahiyo ni lazima tujenge upya fikra za watoto wetu katika mwelekeo fulani na katika tabia fulani. Hizi tabia tunaweza kuzijenga kwa kuwapa elimu itakayo wajenga hivyo. Kwakuwa Siamini kama kuachia taasisi kama polisi na mahakama kushinikiza tabia na mienendo ya watu wetu katika tabia tunayotaka inatosha. Ni lazima watu wetu wajielewe wenyewe na kujua wanajenga taifa lao wenyewe. Kwahiyo hii roho ya kutaka taifa lao livutie na kupendeza ni lazima iwe katika kila moyo wa mwananchi.

Uzuri wa taifa hili utatutegemea sisi kutokana na maarifa na stadi zetu za kazi. Kutokana na busara na hekima. Kila mwananchi ni lazima ajitahidi kufanikisha hili kwakuwa hili taifa ni la kila mmoja wetu, kila mtu ana umiliki nalo ndio maana mtu aliyezaliwa hapa tunamwita mwananchi na mtu yeyote mwenye asili ya hapa kwa vizazi vingi. Ni muhimu kutambua kwa vizazi vingi tumeendelea kuishi katika taifa hili tukipitia katika mambo kadhaa mpaka tulipofikia sasa. Utumwa na ukoloni, na mambo yote magumu ni wakati sasa wa kutafakuri na kulileta taifa hili pamoja. Wakati sasa umefika kwa sisi kuwa wamoja. Ni wakati sasa umefika wa kujifunza kutokana na historia. Ni lazima tuungane tuwe kitu kimoja. Kwa kutopendana kwetu na kwa kutokuwa wamoja tulijikuta katika utumwa na katika ukoloni.

Ukurasa wa umoja na mwelekeo lazima ufunguliwe. Umoja katika malengo ya kujenga jamii bora na endelevu.
Kitabu lazima kifunguliwe sasa, kitabu chenye hadithi nzuri ya kuvutia ya taifa lilinyanyukia kutoka katika utumwa na kutawaliwa, na kujenga jamii bora na zinazovutia dunia haijapata kuona. Kwa ushupavu na matumaini tutafika huko. Mbegu hii lazima ikue, tumaini hili lazima linyanyuke katika kila moyo wa mwananchi. Kwahiyo ni lazima tujenge tabia za wananchi wetu kuelekea huko.

Tungehitaji raia wanaojiongoza wenyewe kutenda yanayostahili kutokana na ufahamu wao na mapenzi yao kwa taifa .
Hapa ndipo umuhimu wa elimu bora unapokuja na ndio maana nasema; elimu ya stadi za kazi peke yake haitoshi pasipo kujenga tabia na nidhamu za watu wetu. Tukifanya hivi taifa letu litakuwa na mwelekeo ni lazima tujenge taifa letu katika uzuri na sio katika ubaya.

Kwahiyo polisi na mahakama havitoshi kujenga jamii bora bila ya kuwepo elimu bora.
Ingawaje vyombo hivi ni muhimu katika kurekebisha tabia za watu wetu na kushinikiza taratibu na sera, ili kujenga jamii bora na zenye amani.

Vyombo hivi vingetumika kidogo kwenye jamii iliyoelimika ili kufanya jamii bora zaidi.
Kwahiyo mtazamo uliokuwepo ya kuwa watu wetu wanapata elimu ili iwafaidishe wao na kuwapatia ajira ni lazima ufutwe ili tuwe na mtazamo wa kuwapa maarifa yatakayowafanya kujikomboa kifikra ili waweze kujenga taifa lao wenyewe na kujitegemea.

Elimu yetu ni lazima iwapatie stadi za kazi zitakazowafanya wajitegemee. Ni ubora wa stadi za za kazi pekee utakaowafanya wahitajike na kuwa wenye manufaa. Ni lazima pia tuwajengee moyo wa kupenda kufanya kazi kwa bidii na bila kukata tamaa.

Habari ya kupasi na kufeli ni lazima tuiangalie upya na kwa umakini. Lengo hapa ni kumuingizia maarifa mtoto na maarifa haya inabidi tuangalie tangia wakiwa watoto katika makuzi yao, tutawajengeaje ufikiri wao. Je tutawasaidiaje watoto wenye ufikiri mdogo kama wakiwepo darasani? Kuwaacha waliofeli ni kutotimiza wajibu wetu. Ni lazima tujenge nidhamu yao na mwelekeo wa akili zao. Pengine walimu wawe na muda wa ziada kwaajili ya wale wenye ufikiri mdogo. Ni lazima vijana na watoto wetu wajue wanaenda shule kutafuta maarifa na akili yao iwe katika maarifa na sio ajira. Wakienda shule katika mtazamo wa kutafuta maarifa watakuwa wabunifu zaidi na watatia juhudi zaidi kupata ufahamu. Vijana wetu wakienda shule kwa mtazamo wa ajira na sio maarifa tutakuwa hatujafanya jambo la msingi. Hawatopata uelewa wa kutosha na hawatotumia nguvu nyingi na akili kuitafuta. Watatumia njia zozote ili wapasi hata kwa kudanganya ili waje wapate ajira na pesa hawatothamini maarifa kama maarifa. Kwa mtazamo huu hatutaweza kukuza ufahamu wao.
Vijana wetu wakiwa na mtazamo huu hawatapenda elimu, itakuwa ngumu na mzigo kwao, na watatumia nguvu nyingi katika kuelewa, elimu yetu itajawa na uwoga na hofu ya kufeli na ya maisha. Ni muhimu kuwaondolea hofu hii vijana kwa kuangalia upya misingi na mazingira ya elimu yetu.

Iwe watu wanaenda shule kutafuta maarifa yatakayokuja kuwasaidia jinsi ya kuishi, na ufundi stadi wa kuzalisha mali.
Katika mwelekeo huu taifa letu litakuwa na tija. Watu wetu wataweza kutawala familia zao na kuwa na mahusiano mazuri miongoni mwao lakini watakuwa na dira ya pamoja kama taifa.

Tunapenda watu wetu wawe na ufahamu na wawe huru. Waweze kujua yaliyo sahihi kwao. Waweze kujenga familia zao katika ubora, na wawe wenye manufaa kwa jamii na kwa taifa.
Wakiwa na elimu hii wataweza kutumia rasilimali za taifa kwa faida ya umma kwasababu elimu yetu itakuwa imeelekezwa kwenye ujenzi wa taifa na jamii na sio manufaa binafsi.
Watatengeneza sheria na kuzitii kwasababu watajua ni mali yao na ni kwa faida yao. Ni katika mtazamo huu tutaweza kulikabidhi taifa hili kwa kizazi kingine likiwa bora na lenye utaratibu na ustaarabu.

Tunapenda watu wetu wawe kwa asilia wenye kupenda maarifa ni lazima tujenge tabia hii na ni lazima tuondoe fikra hizi zilizojengeka kwa miaka mingi mongoni mwetu. Tukifanikiwa tutajenga jamii bora na yenye uwajibikaji.
Ni lazima wafundishwe kulithamini na kulipenda taifa lao na ya kwamba wanapewa elimu ili waweze kuliendesha taifa hili katika ubora.

Ni muhimu kutambua ya kwamba binadamu anapata faida kubwa anapoishi na jamii, nje ya jamii maisha ya binadamu yasingekuwa kama yalivyo sasa.
Tuna wajibu wa kujenga jamii zetu na familia zetu lakini pasipo elimu bora hatutaweza vyote hivi. Ni lazima tujenge familia zetu na jamii zetu katika nidhamu na katika utaratibu.

Elimu yetu pia lazima ilenge kukuza fikra na uelewa wa watu wetu. Na sio tu kumwingizia maarifa kichwani, imfanye aweze kufikiri na kufanya maamuzi sahihi kwa kutumia ubongo wake na sio kuelekeza tu bali kukuza ufahamu na wala sio kukariri. Aweze kufikiri mwenyewe na kuamua yaliyo sahihi.

Elimu hii itamfanya kuwa huru zaidi na bila elimu ya namna hii hatutaweza kujenga nchi ya kidemokrasia. Kwasababu demokrasia inahitaji uelewa wa watu katika kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya nchi.
Kwasababu demokrasia inawataka wananchi kujiamulia mambo yao wenyewe kwa faida yao wenyewe na hii inahitaji elimu. Bila elimu na hatutaweza kujenga demokrasia.

Demokrasia hii inahitaji nidhamu na jamii yenye utaratibu na mpango. Demokrasia katika jamii isiyokuwa na utaratibu mzuri ni fujo. Ni lazima jamii iwe inajielewa ili demokrasia ifanye kazi vizuri. Ni lazima iwe jamii inayojitambua na inayojua mwelekeo wao. Ni lazima iwe jamii iliyopangwa na kupangika ndipo demokrasia itakapofanya kazi vyema. Jamii hii ni lazima iwe ambayo imeelimika. Bila kuelimika huku demokrasia haiwezi kufanya kazi.

Ni baba anayejua kilicho bora kwa mtoto wake lakini mtoto atakapokua na kupata uelewa hujua anachohitaji. Ni lazima elimu yetu iwafanye watu wetu wapate uelewa huu. Na demokarsia yetu itafanya kazi mpaka pale watu wetu watakapoelimika na kujitambua, kwasasa ni mpaka tumpate kiongozi mzuri atakayesimamia ukuaji huu. Mpaka hapo itakapoonekana watu wetu wanajitambua na wanaweza kujiongoza wenyewe kwa njia za kidemokrasia bila kuathiri mpangilio wa jamii na amani ya nchi.

Ni muhimu sana kama tunataka kujenga taifa la kidemokrasia ambalo pia huhitaji nidhamu ya hali ya juu. Ni lazima tujenge watu wetu katika fikra sahihi.

'' Kama madhumuni ya elimu ni kumuongezea uelewa na binadamu na kumfanya kujitambua, kutambua mazingira yake, kutengeneza tabia yake na mahusiano yake na jamii, kumfanya awe na nidhamu na awe mwenye faida kwa umma na kwa jamii, bado kwa kiwango kikubwa, hatujafanikiwa katika dhamira hii kwakuwa dhumuni la kuwa na taifa sio tu ni kupata faida za kimali bali pia kujenga mahusiano yetu na mashirikiano yetu kama binadamu. Na huu ndio msingi wa jamii yenye furaha.
Jamii ambayo inahangaika kwenye kutafuta mali tu bila pia kujenga misingi ya mahusiano yao kamwe haitoweza kuwa na furaha. Kwasababu pesa itakuwa ndio msingi wa maisha yao. Uhusiano wao utakuwa duni na tunaweza kupima mwisho wa jamii hii kwa matendo yake na kuujua. Ni dhahiri sio mwisho mzuri''
 
Umenena vyema mkuu swali tufanyaje ili tuondokane na hii hali na kuleta kujiamini kwetu kama waafrika na kama watanzania?

And though the philosopher may live remote from business, the genius of philosophy, if carefully cultivated by several, must gradually diffuse itself throughout the whole society, and bestow a similar correctness on every art and calling. (David Hume, 1737)

Na tufanye fikra zetu kuwa HAI. Si muda wa porojo sasa pasi na VITENDO. Ni sisi wenyewe wa kuzifanya hai. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU, hakuna kinachoshindikana. Naamini sana kichwa cha MTU MWEUSI, HATUWEZI KUSHINDWA. Tujikatae kwanza, katika Umoja tuthubutu, lets reason, TUSUKE HESABU ZETU WENYEWE. Anayejitambua ni anayetekeleza wajibu wake katika jamii yake! TUJITAMBUE LEO.
Time Will Tell! WE ARE THE TIME!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!
 
Na tufanye fikra zetu kuwa HAI. Si muda wa porojo sasa pasi na VITENDO. Ni sisi wenyewe wa kuzifanya hai. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU, hakuna kinachoshindikana. Naamini sana kichwa cha MTU MWEUSI, HATUWEZI KUSHINDWA. Tujikatae kwanza, katika Umoja tuthubutu, lets reason, TUSUKE HESABU ZETU WENYEWE. Anayejitambua ni anayetekeleza wajibu wake katika jamii yake! TUJITAMBUE LEO.
Time Will Tell! WE ARE THE TIME!
Mungu wetu yu tayari kutushindia vitani. Anaita sasa!

Sure mkuu.
 
you people i love your ideas.

But kiongozi Shayu nafikiri kama vile uliisoma signature yangu ulipokuwa unaandika huu uzi.

Binafsi nakubaliana na hoja juu ya kufikiri sana kwa kina na hii ndiyo itakayotuletea ukombozi wa kimaisha na kimaendeleo.

Lakini sasa nirudi kidogo kwenye elimu yetu tunayopenda sana kuinanga kwamba haikidhi vigezo. Kwanza kabisa naomba niseme wazi kwamba siku zote tusiwe watu tusiopenda kusifia tulicho nacho (sina maana kwamba umenanga elimu yetu la hasha) ila pia tusiwe watu tunaopenda kuwa wanyonge mbele za wageni wetu.

nayasema haya nikichukulia mfano mdogo sana kwenye maisha yetu ya kila siku, wanafunzi wentu wengi tu wa vyuo vikuu ni wazuri na wanafanya mambo mazuri ajabu ishu inakuja tu kwamba wao hawajiamini kwenye karibu kila kitu wanachokifanya na wamebaki na ule utegemezi ya kwmba lazima awepo mtu atakayetenda hili jambo.

leo hii Kenyan sio kamba wana elimu ya kutisha ama wanamaarifa ya kutisha kuliko sisi ila tu kenyans are so aggressive ukilinganisha na sisi, kwa wao kuwa aggressive unajikuta kwamba wana confidence kubwa sana ukilinganisha na sisi. sasa kumbe ishu kwetu sio tu kufikiri peke yake bali pia kuwa na na confidence and this is very serious inapokuja kwenye mambo ya kudeliver ama hata kujiuza kimataifa.

leo hii kijana wa kitanzania mathalan mwenye ngazi ya shahada ya kwanza yuko so diversified kwenye mambo mengi sana, manake utamkuta kwenye mngnt, kwenye law, business na bado ile professional discipline yuko tena vizuri tu. sasa anapokwenda kwenye kufanya kazi ndipo tatizo linapotokea kwanza anakata tamaa manake hataki kuanza kutoka chini( ikumbukwe kwamba maisha lazima yaanze chini kupanda juu), halafu kutokana na kwamba hajameet malengo yake anaanza kuwa mjanja mjanja ili atoke kimaisha na katika hili uvivu na utegevu unakuwepo na hata wizi na rushwa.

lakini kijana huyu akikumbushwa maisha lazima graph yake i grow gradually akaelewa nafikiri angeyaepuka haya na angekuja kuyafurahia maisha vizuri sana baadae.
 
'' Kama madhumuni ya elimu ni kumuongezea uelewa binadamu na kumfanya kujitambua, kutambua mazingira yake, kutengeneza tabia yake na mahusiano yake na jamii, kumfanya awe na nidhamu na awe mwenye faida kwa umma na kwa jamii, bado kwa kiwango kikubwa, hatujafanikiwa katika dhamira hii kwakuwa dhumuni la kuwa na taifa sio tu ni kupata faida za kimali bali pia kujenga mahusiano yetu na mashirikiano yetu kama binadamu. Na huu ndio msingi wa jamii yenye furaha.
Jamii ambayo inahangaika kwenye kutafuta mali tu bila pia kujenga misingi ya mahusiano yao kamwe haitoweza kuwa na furaha. Kwasababu pesa itakuwa ndio msingi wa maisha yao. Uhusiano wao utakuwa duni na tunaweza kupima mwisho wa jamii hii kwa matendo yake na kuujua. Ni dhahiri sio mwisho mzuri''

Nadhani ukisoma hii sentence utatambua kitu ninachoongelea Elimu yetu imepungukiwa hasa katika hila jambo la uzalendo na fikra za kujenga taifa. Elimu yetu imejengwa katika ubinafsi lakini sio fikra pana za ujenzi wa taifa.
 
Similar Discussions

18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom