Fredinho
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 971
- 1,137
Hatua aliyofikia msanii Darasa imenikumbusha miaka kama 6 iliyopita wakati msanii 20% alipofikia kiwango chake cha juu mno kimuziki,pamoja na kuwa 20 pa alikuwa na nyimbo nzuri kama maisha ya bongo na mama neema lakini kilele chake cha mafanikio kimuziki kilifika rasmi mwaka 2010 baada ya kutoa nyimbo tatu kali: Ya nini malumbano,Ningekusamehe na 'wimbo wa taifa' TAMAA MBAYA.
Kila mtu alimjua 20 pa, kama zawadi kwa kazi yake nzuri watanzania walimpa tuzo 5 katika usiku ule wa kukumbukwa sana (ambao baada ya hapo uigizaji umekuwa mwingi kwa baadhi ya wasanii kupewa tuzo 6 au 7 ili tu ionekane nao wamevunja rekodi,ingawa mpaka leo mimi naamini ni 20% na nyimbo zake zilizogusa sana ndie msanii pekee ambae wingi wa tuzo zake ulimstahili).Kilichomtokea baada ya hapo hatujui lakini 20 amepotea sababu kuu inaweza kuwa menejimenti mbovu au kutokuwa na nidhamu ya kazi,kwani wengi tulijuwa kuwa lile lilikuwa jukwaa la 20 kupaa zaidi......
Darasa anapita njia ya 20% ila natamani kumuoana akifika juu juu na mbali zaidi.Licha ya kuwa Darasa amekuwa na nyimbo nzuri huko nyuma kama sikati tamaa na nishike mkono lakini ni kweli kuwa mwaka huu ndio umemtambulisha na kumpa darasa jukwaa kubwa zaidi kwa nyimbo zake tatu: Kama utanipenda,Too much na "wimbo wa taifa" MUZIKI (ni kama 20% mwaka 2010),Naimani kama Kili awards ikifanyika mwanzoni mwa mwaka ujao basi Darasa anaweza kuvunja rekodi ya tuzo kama 20% 2010 na hakuna atakaebisha.
Nategemea Darasa atapita njia tofauti na 20% na kama anavyosema mwenyewe ataendelea kutoa bampa to bampa,nategemea atatumia jukwaa hili na kilele hiki alichofikia kulipeleka gemu to the top top kama anavyodhamiria,kufika kileleni ni rahisi ila kudumu kileleni kumewashinda wengi.
KILA LA HERI DARASA