Darasa la uongozi: Sababu ya Wagombea wengi kushindwa ni matokeo ya kukosa mipango na mikakati ya ‘kuwekeza kwenye uongozi’

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Watu wanapenda matokeo ya haraka, ila ni wavivu kuyatafuta. Wahenga walivyosema ‘Mtaka cha uvunguni, sharti ainame’, walikuwa na maana ya kwamba, unavyokuwa na ndoto za kupata kitu chochote kwenye maisha, ni lazima uweke mipango na mikakati ya kufanikisha azma yako.

Mtu unataka kuwa kiongozi, mathalani mbunge 2025, usisubiri ifike hiyo 2025 ndo uanze harakati za kuwa mbunge. ‘Anza kuwekeza mapema kupata huo ubunge. Ukisubiri ifike hiyo 2025 ndo ukurupuke uchukue fomu angali kuku nyuma hukuwekeza, hapo ni sawa na kucheza Kamari, na wananzengo lazima wakupige na kitu chenye ncha kali, kama tulivyoshuhudia kwenye hizi kura za maoni.

Unawekeza vipi kuwa mbunge/kiongozi?

Kwa tasiri yangu, uongozi ni kugusa maisha na hisia za watu, ni kujitoa kuhakikisha unakuwa sehemu ya maisha ya watu angalau kwenye furaha zao, huzuni, na shughuli za kijamii.

Uongozi sio kugawa mahela kwa watu, ndo maana tumesikia kuna mahali watu wamekula mahela ya watu na hawajampa kura mtoaji mahela, unadhani ni kitu gani kinamfanya mpinzani wako apate kura pasipo kutoa hela, na wewe ukose kura angali umehonga ‘mahela’?

Jibu la hilo swali litategemea, ni namna gani uliwekeza vizuri kuwa kiongozi wakati unaishi kwenye jamii. Namna gani ulikuwa unajaribu kuwa sehemu ya maisha ya watu / wanachama wenzako ndani ya chama.

Mbinu za kimkakati za kuwekeza kwenye uongozi

Kwa mfano umetafiti kwamba asilimia 35% ya wajumbe wa jimbo lako ni wakina mama ambao itakuwa muhimu kupata kura zao. Tengeneza utaratibu wa kugusa maisha ya hawa wamama miaka mitano kabla.
  • Tumia ujuzi wako wa kielimu, tengeneza vikundi vidogo vidogo kuwakutanisha hawa wakina mama, wasaidie kusajili vikundi vyao na uhakikishe unakuwa mstari wa mbele kutoa mawazo ya hapa na pale ya kupiga hatua.
  • Tenga muda wako walau mara moja kwa mwezi, uandae darasa la kiujasiriamali kwa hawa wakina mama.
Matokeo ya haya ni kwamba, utatengeneza Imani fulani kwa hawa wakina mama, kwamba umekuwa mtu muhumu kwenye maisha yao kama raia na mwanachama mwenzao wa chama cha kisiasa.

Hata ikitokea siku inafika unasimama kuomba ridhaa, itakuwa ni ngumu kukosa kura za hawa wakina mama.

Tekeleza mbinu hizi hizi kwa makundi mengine ya wajumbe wa chama chako (vijana na wazee) mfano
  • Kuwa mtu mwenye kutoa maneno ya busara na mtu mwenye uwezo wa kutoa ushauri wenye manufaa kwa watu. Onyesha hizi mbinu kwenye vikao vya ndani vya chama, onyesha kwamba unakitu cha tofauti ndani yako pale unaposimama kuongea.
  • Usiwe mtu wakujitenga na daraja la chini, kwa mfano, haigharimu kitu kila weekend moja kwenda kwenye kijiwe cha kucheza bao pale kwenye ofisi ya chama kuzogoza na wajumbe wazee.
  • Kuwa mbunifu, andaa hata mashindano ya bao kwa wazee wa chama chako, kwenye kila tarafa ya jimbo.
  • Appearance ni muhimu sana hapa itabidi ujifunze kuvaa na kupendeza, kuwa mtu smart kila siku ya maisha yako, hii inajenga nguvu ya kupendwa na watu na kuheshimika.
  • Pia kwenye dini, hakikisha unapata nafasi kwenye uzee wa kanisa,
  • Kwenye shule, wanazosoma watoto wako, tafuta namna ya kuwa kwenye kamati za shule.
Lengo la haya yote, ni kwamba yatakupatia platform kwenye jamii na kukupa kitu muhimu sana kinachohitajika kwenye uongozi ambacho ni ‘VISIBILITY’. Hakuna mtu duniani atakuwa na nguvu na uwezo wa kupambana na wewe, ukishakuwana VISIBILITY.

Ni VISIBILITY ambayo mara nyingine itafanya hata vikao visianze bila wewe kufika, sio kwamba kwa sababu wewe ni mwenyekiti wa mkutani, la hasha, ni kwasababu tu kuna kitu kisichoonekana umekiwekeza kwa watu, kiasi kwamba wanafikia hatua ya kuhisi mkutano haujakamilika bila wewe kuwepo.

Ukiyafanya haya mambo yote, ambayo mimi nayaita ‘uwekezaji kwenye uongozi’ hakika, itakuwa ni ngumu sana kwa wewe kukosa aina yoyote ile ya uongozi wa kuchaguliwa na watu katika dunia hii.

Huyu mama alikuwa hana kazi, lakini kupitia vikundi ulivyovianzisha wewe, sasahiv anapata hata 10,000 kwenye ujasiriamali wake wa kila siku, anakunyimaje kura yake kwa mfano?

Hawa wazee kwa miaka mingi, umekuwa sehemu ya maisha yao kwenye kubadilishana mawazo na kupiga zogozi kwenye vikundi vyao vya bao, unadhani wanaposikia umetia nia, wanaanzaje kukunyima kura?

Ndo mana nilivoona, watu wameangukia pua kwenye hizi kura za maoni, nimepata tafsiri moja tu kwamba, watu wengi wanapenda uongozi lakini hawapendi kuwekeza kwenye uongozi, n ahata ukiangalia wengi walioshindwa ni watu ambao kuna ushahidi usio na shaka kwamba walishindwa kuwekeza kuwa viongozi.

Uongozi ni uwekezaji na sio kubahatisha

N.Mushi
 
Wameshindwa pia kuna walioshinda sasa unataka wote washinde inawezekana vipi?
Nawafundisha walioshindwa ikiwa nao watataka kushinda.

Na nini kitatokea ikiwa kila mtu ataishi ili mshindi?

Maana yake ni kwamba watu wengi sana watajitoa kwa jamii zao ili kuzitendea mambi mema ili baadae waje kuziongoza, iki maanisha hata jamii yenyewe itakuwa bora zaidi na zaidi.

Kama mfano hawa watia nia wa CCM zaidi ya 10,000 kila mmoja angeamua kipindi cha miaka mitano iliyopita afanye kitu kwenye jamii yake, unadhani impact yake ingekuwa ni ndogo?

Kungekuwa na mabadiliko makubwa sana, na hii ndio haswa msingi wa siasa na maendeleo unavopaswa kuwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom