Darasa la saba Dar kufanya mitihani 16 Jan 2020, Necta watoa ufafanuzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetoa ufafanuzi kuhusu mitihani itakayofanyika kesho Alhamisi Januari 16, 2020 jijini Dar es Salaam kwa wanafunzi wa darasa la saba.

Mtihani huo utahusisha shule zote za umma na binafsi na utafanyika kwa siku moja ya kesho.

Limesema mitihani hiyo ni mazoezi ya ndani ya wanafunzi katika shule za Mkoa huo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Januari 15, 2020 katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kinachofanyika kesho si mitihani ya Necta, ni jaribio kwa walimu wa Mkoa huo baada ya kupewa mafunzo ya namna bora ya kutunga mitihani.

“Hawana mtihani kama watu wanavyotaka kupotosha, usahihi ni kwamba watakuwa na mazoezi ya ndani ya shule zao ambayo yatasimamiwa na Necta.”

“Tuliwapa walimu mafunzo ya namna bora ya kuwapa mitihani na mazoezi wanapokuwa shuleni kuhakikisha ufaulu unakuwa vizuri zaidi na wanafunzi wanaizoea mitihani ya Taifa na kuwa tayari watakapokutana nayo,” amesema Msonde.

Amesema lengo la mazoezi hayo ni kuhakikisha walimu wa shule zote za msingi wanakuwa na umahiri wa kutunga mtihani.

“Tunaamini shule zikiimarika Taifa linaimarika, tunataka ubora wa maswali uongezeke ili wanapofika kwenye mtihani wa mwisho wawe wamebobea. Tunataka tuone kama kuna chochote wamekipata kwenye mafunzo yetu na kama kuna shida tuone ni namna gani tunaweza kuweka sawa,” amesisitiza Msonde

Chanzo: Mwananchi
 
Kwahiyo wanaotunga mitihani ya NECTA ni walimu wa Dar tu?

Sent using Jamii Forum's by simcard
 
Wanagunzi wamefungua shule tarehe 6 january, kesho ni tarehe 16
Hivi ndani ya huo muda, walimu na wanafunzi wanaweza kuwa wamesoma kiasi cha kucover mada zote za darasa la saba?
“Tuliwapa walimu mafunzo ya namna bora ya kuwapa mitihani na mazoezi wanapokuwa shuleni kuhakikisha ufaulu unakuwa vizuri zaidi na wanafunzi wanaizoea mitihani ya Taifa na kuwa tayari watakapokutana nayo,”
 
NARUDIA KWA SAUTI TUBADILISHE MITAALA juzi tu wanafunzi wa kidato cha pili kanda ya ziwa wameulizwa na Afisa Elimu wao kwanini hamjui kusoma na kuandika lakini mmefika Sekondari?Wanafunzi wakajibu TUMEFANYIWA MITIHANI NA WALIMU sasa huyu msonde anamfurahisha Nani ?Yaani nchi nzima upuuzi wa walimu kuwafanyia wanafunzi mitihani umekuwa kawaida ,Ndalichako yupo,Msonde yupo,Rais yupo,Ndumbaro yupo,Wadau wa Elimu wapo
 
Ninapokujibu hivyo hiyo yote naifahamu
Semina ilitolewa siku ya jumamos, zaidi walitoa maagizo na kuonya juu ya wizi wa mitihani unaofanywa na shule za hapa jijini pia waliwaagiza walimu wakajipange kwa kujiandaa na mtihani huo
Ajabu ni kesho mtihani utafanyika, je hayo maandalizi yatafanyika lini?
“Tuliwapa walimu mafunzo ya namna bora ya kuwapa mitihani na mazoezi wanapokuwa shuleni kuhakikisha ufaulu unakuwa vizuri zaidi na wanafunzi wanaizoea mitihani ya Taifa na kuwa tayari watakapokutana nayo,”
 
Back
Top Bottom