Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Sabayi

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
2,310
991
bean_banner.jpg


Habari Wakuu

Nilipitia maonesho ya nane nane mwaka huu na moja ya kilimo kilichonivutia ni kilimo cha Dengu na Conflower/Brocolli.
Mazao haya yana soko kubwa sana nje ya nchi hasa India kwa Dengu na ulaya/India kwa Conflower.

Kwa wale wazee wa kanda ya kati kuanzia Dodoma, Singida, Tabora hadi Shinyanga Dengu inakubali sana maeneo hayo sina uhakika na maeneo mengine ila nadhani Morogoro inaweza kukubali (I'm not sure) ni zao la muda mfupi.

Tuchangamkie hizi fursa ndugu zangu Tunapaswa kuwa wakulima tunaowaza kuexport mazao yetu sio kila siku tunapigana vikumbo kariakoo sokoni tu kwa mfano hii Conflower/Brocolli nimeambiwa gram 25 inauzwa 30000/= TZS sasa piga hesabu kwa ekari moja unaweza kupata kilo Kilo/Tani ngapi na unamake kiasi gani?

Naomba kuwasilisha

MUHTASARI WA KILIMO CHA MAZAO JAMII YA KUNDE
KILIMO CHA NJEGERE

Mara nyingi huwa napenda kula ubwabwa na njegere, sijui kama na wewe mwenzangu unapenda kula njegere? Kama jibu ndiyo basi nakusihi uungane nami katika makala haya ili uweze kujifunza namna ya kulima kilimo hiki.

Nakusihi kulima kilimo hiki kwa kwa sababu , kilimo cha njegere ni kilimo chenye tija kwa wakulima. Njegere ni mbegu za spishi za mimea katika jamii ya kunde ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali duniani katika maeneo ya ukanda wa juu.

Spishi kadhaa za njegere ni:
1. Njegere kubwa (chickpea)
2. Njegere ya kizungu (common pea)
3. Njegere sukari (snow pea and snap pea)

Hapa nchini Tanzania njegere hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu njegere hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.
Kuna aina mbalimbali za njegere zinazopatikana Tanzania kama Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na Mbegu za kienyeji.

HALI YA HEWA:
Kwa tafiti inaonesha zao la njegere hustawi vizuri maeneo yenye hali ya ubaridi wa sentigredi 17 – 21 C, na mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari na mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama. Udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA:

Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina. Changanya mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha ardhi.

UTAYARISHAJI WA MBEGU
Chambua mbegu nzuri zinazoonekana hazina matatizo, zilizo na afya ili kupata mazao mengi. Unashauriwa kuandaa mbegu mapema ili kuweka maandalizi mazuri.

UPANDAJI
Njegere hupandwa kipindi cha mvua ama kwa umwagiliziaji, maana udongo unatakiwa uwe na unyevu ili kufanya mmea kukua vyema, nafasi za kupanda:-

i) 60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.
ii) 12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.
iii) Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.
iv) Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.

MBOLEA
Ukitumia mbolea za asili (samadi au Mboji) njegere hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari.

UPALILIAJI
Njegere zipaliliwe zikiwa changa shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya mda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu njegere hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, njegere zisipaliliwe ili kuongeza mazao.

Magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

MAGONJWA & WADUDU

MAGONJWA

Ascochyta


Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.

Root Rot na Blight disease.(kuoza kwa mizizi na Blingt)
Husababishwa na fangasiA. pinodella na mycosphaerella pinodes.

Dalili: – madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi .

Kuzuia.
1. Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.
2. Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.

Downy mildew
Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.

Dalili: Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na

kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa unyevunyevu.

Kuzuia: – Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

Fusarium wilt:– Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.

Dalili:
1. Majani kubadilika rangi kuwa manjano.
2. Mimea kudumaa.
3. Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.

Kuzuia: – Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.
Virusi
– Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.
Kuzuia: – Kutumia mbegu zisizo na maradhi.

WADUDU
Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. Baadhi ni kama American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.

Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.

UVUNAJI
Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa . Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi, Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa, Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu na ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka. Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.
Mkuu hizo ni stori za watu tu ukweli halisi haupo hivyo, hebu soma hapa labda mimi naona vibaya,

CHANGAMOTO YA KUKOSA SOKO LA UHAKIKA KWA WAKULIMA CHANZO CHA UMASIKINI​
WAKULIMA wa zao la dengu katika kijiji cha Amani kata ya Salawe halmashauri ya wilaya ya Shinyanga bado wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko la uhakika kwenye zao hilo ikiwemo miundombinu ya barabara kuwa mibovu hali ambayo inawafanya kushindwa kusafirisha mazao yao.

Wakiongea na mwandishi wa habari aliyetembelea wakulima wa kijiji hicho walisema kuwa zao hilo limekuwa mkombozi katika kunyanyua pato la familia lakini kubadilika kwa bei ikiwa wengine wanauza shilingi 45,000 mpaka 55,000 kwa gunia moja na kukosa soko la uhakika imekuwa ni tatizo, ikiwemo wadudu wahalibifu pamoja na panya.
KILIMO CHA NJEGERE

Mara nyingi huwa napenda kula ubwabwa na njegere, sijui kama na wewe mwenzangu unapenda kula njegere? Kama jibu ndiyo basi nakusihi uungane nami katika makala haya ili uweze kujifunza namna ya kulima kilimo hiki.

Nakusihi kulima kilimo hiki kwa kwa sababu , kilimo cha njegere ni kilimo chenye tija kwa wakulima. Njegere ni mbegu za spishi za mimea katika jamii ya kunde ambayo hukuzwa sehemu mbalimbali duniani katika maeneo ya ukanda wa juu.

Spishi kadhaa za njegere ni:
1. Njegere kubwa (chickpea)
2. Njegere ya kizungu (common pea)
3. Njegere sukari (snow pea and snap pea)

Hapa nchini Tanzania njegere hulimwa nyanda za juu kusini, nyanda za juu kaskazini na kwenye miinuko ya Usambara na Uluguru. Katika ulimwengu njegere hulimwa kwa wingi katika Asia ya kati, Mediterania na Afrika ya kaskazini.
Kuna aina mbalimbali za njegere zinazopatikana Tanzania kama Tanganyika yellow, Idaho white, Rondo na Mbegu za kienyeji.

HALI YA HEWA:
Kwa tafiti inaonesha zao la njegere hustawi vizuri maeneo yenye hali ya ubaridi wa sentigredi 17 – 21 C, na mwinuko zaidi ya mita 1200 usawa wa bahari na mvua, unyevu wa kutosha na maji yasiyotuama. Udongo uliowekwa mbolea, kulimwa kwa kina na wenye tindikali ya PH 5.5 – 6.5.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA:

Maandalizi yanatakiwa yaanze kabla msimu wa mvua haanza, Shamba / bustani itayarishwe kwa trekta au pawatila au jembe la mkono au jembe la ng’ombe kwa kufuata mahitaji ya udongo kama kutotuamisha maji, kulimwa kwa kina. Changanya mbolea za asili (samadi au mboji) na udongo ili kurutubisha ardhi.

UTAYARISHAJI WA MBEGU
Chambua mbegu nzuri zinazoonekana hazina matatizo, zilizo na afya ili kupata mazao mengi. Unashauriwa kuandaa mbegu mapema ili kuweka maandalizi mazuri.

UPANDAJI
Njegere hupandwa kipindi cha mvua ama kwa umwagiliziaji, maana udongo unatakiwa uwe na unyevu ili kufanya mmea kukua vyema, nafasi za kupanda:-

i) 60 sm – 90 sm x 5.7 sentimita kwa mbegu fupi.
ii) 12 sm – 15 sm x 5 – 7.5 sentimita katika safu mbili za sentimita 90 kwa mbegu inayotambaa.
iii) Njegere hustawi vizuri zikipata sehemu za kutambalia.
iv) Mbegu ya njegere huota baada ya siku 7 – 10.

MBOLEA
Ukitumia mbolea za asili (samadi au Mboji) njegere hustawi vizuri. Katika kipindi cha ukuaji ni muhimu kuweka mbolea ya chumvichumvi za nitrogen kwa kipimo cha kg 40 kwa hekari.

UPALILIAJI
Njegere zipaliliwe zikiwa changa shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya mda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu njegere hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, njegere zisipaliliwe ili kuongeza mazao.

Magugu hushindana na kunyanganyana na mimea kutumia virutubisho. Pia huongeza kivuli wakati wa utoaji maua na kusababisha upungufu mkubwa wa mazao. Palizi hufanyika kwa mkono au kutumia dawa za kuua magugu.

MAGONJWA & WADUDU

MAGONJWA

Ascochyta


Kutokea kwa mabaka makubwa ya kahawia kwenye majani na matunda. Pia hutokea hata kwenye shina. Katikati ya baka huwa rangi ya kijivu, kingo nyekundu / nyeupe husababishwa na fangasi aina ya Ascochyta pisi.

Root Rot na Blight disease.(kuoza kwa mizizi na Blingt)
Husababishwa na fangasiA. pinodella na mycosphaerella pinodes.

Dalili: – madoa madogomadogo yenye rangi ya zambarau / rangi ya kahawia iliyokaza au madoa meusi ambayo huungana na kusababisha jani na maua kuwa yenye rangi nyeusi .

Kuzuia.
1. Kutumia mbegu zisizo na magonjwa.
2. Kuzika mabaki ya mazao yaliyoadhirika kwa miaka 3 – 4.

Downy mildew
Husababishwa na fangasi Erysiphe polygoni.

Dalili: Majani kuonekana kama yamemwagiwa unga na baadae na

kufa. Ugonjwa unaathiri zaidi mimea kipindi cha uhaba wa unyevunyevu.

Kuzuia: – Kutumia sulphur ya unga kama inavyoshauriwa.

Fusarium wilt:– Husababishwa na fangasi / ukungu Fusarium oxysporum.

Dalili:
1. Majani kubadilika rangi kuwa manjano.
2. Mimea kudumaa.
3. Ugonjwa ukitokea kwenye mimea michanga huua mmea wote.

Kuzuia: – Tumia mbegu yenye uvumilivu kwa ugonjwa huu.
Virusi
– Mmea huonekana kuwa na uvimbeuvimbe kuzunguka jani. Mmea hudumaa.
Kuzuia: – Kutumia mbegu zisizo na maradhi.

WADUDU
Wapo wadudu wengi ambao hushambulia zao la njegere. Baadhi ni kama American bollworm, Bean flies, Bean Aphids, Pea Aphids huambukiza virusi na Green peach aphids.

Inashauriwa kumwona mtaalam wa kilimo aliye karibu yako kwa ufafanuzi wa kuwazuia wadudu waharibifu.

UVUNAJI
Kwa njegere teke / mbichi hukomaa siku 60 – 90 na kwa njegere kavu huchukua siku 80 -150 kukomaa . Njegere teke huvunwa punje zikiwa bado mbichi, Uvunaji hufanyika mara 2 – 3 kwa wiki wakati wa kipindi cha ukuaji. Zaidi ya kilo 3000 kwa hekta za njegere teke huvunwa, Njegere kavu huvunwa wakati punje zimekauka na kuwa ngumu na ni muhimu kuwahi kuvuna njegere kavu ili kutopoteza mavuno zikipasuka. Mavuno ya punje kavu na kilo 1500 kwa hekta.
ABC's ZA ZAO LA CHOROKO

Choroko ni moja ya mazao ya jamii ya mikunde hustawi eneo lenye mwanga wa kutosha pamoja na udongo wa tifutifu.pia masoko yake ni mazuri mfano kwa masasi 1300-1500@kg

Hakihitaji mvua nyingi na hakuna magonjwa yanayoathiri isipokuwa wadudu wanashambulia majani pamoja na choroko wakati za kuzaa hivyo suluhisho ni kupulizia dawa za kuu wadudu kama NINJA, KARATE, DUDU ALL e.t.c kila baaea ya siku 14 kuanzia wakati zinatoa maua.

Huchukua siku 60 hadi kuvuna japo hazizai kwa mkupuo yaani kadri unyevu ulivyo ndivyo nazo huzidi kutoa maua na kuzaa. Pia waweza mwagilia kama unavyolima kunde.

Katika kupanda tofauti ya shina na shina ni sm 35 na tofauti ya mstari na mstari sm 55.pia kila shina moja unatia punje 2-3 za choroko,halihitaji mbolea ila unahitaji kupulizia dawa ya kuuwa wadudu hasa wakati zinazaa walau mara 21.

Hivyo vijana tujishughulishe tupige kazi
MUHTASARI WA KILIMO CHA MBAAZI

Mbaazi ni zao jamii ya mikunde inayostawi katika nchi za kitropiki zenye mvua chache. Zao hili ni muhimu sana kwa nchi za Asia ambako ni mojawapo ya chakula kikuu hasa katika nchi ya India.

Kwa miaka ya hivi karibuni, zao la mbaazi limekuwa moja ya mazao muhimu ya biashara katika maeneo mengi ulimwenguni. Hii ni kutokana na ongezeko la walaji na uwezo wake wa kustahimili ukame na mvua chache ambao unaendana na mabadiliko ya hali ya hewa ulimwenguni kote. Nchini Tanzania, zao hili hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Manyara (Hanang na Mbulu), Arusha (Arusha vijijini na Meru), Dodoma (Kondoa), Kilimanjaro (Same, Mwanga, Rombo, Hai na Moshi vijijini) Mbaazi kwa kawaida hupandwa kwa msimu mmoja lakini aina za kienyeji zinaweza kulimwa kama zao la kudumu ambapo huweza kukaa shambani miaka mitatu hadi mitano ingawa uzalishaji wa mazao hupungua msimu hadi msimu.

Matumizi ya Mbaazi
Chakula/mboga hasa zikiwa mbichi. Mbaazi mbichi huwa na protini zaidi ya asilimia 21%, wanga asilimia 44.8%, mafuta asilimia 2.3% pamoja na baadhi ya virutubisho vya madini kama chokaa na chuma.

Zao la biashara. Kutokana na kuwepo kwa aina bora za mbaazi zinazohitajika kwa wingi katika soko la ndani na nje pamoja na kuwepo kwa aina zinazokomaa mapema na kuwahi soko la dunia, zao hili limekuwa likilimwa kwa ajili ya biashara hasa katika wilaya za Babati, Karatu, Arumeru pamoja na Kondoa

Chanzo cha nishati (kuni). Miti ya mbaazi hutumiwa kwa ajili ya kuni katika maeneo ya ukanda wa chini ambayo haina miti. Matumizi haya pia husaidia kupunguza uharibifu wa mazingira kutokana na watu kutokukata miti ovyo.
Kirutubisho cha udongo. Mbaazi ni jamii ya mikunde ambayo huongeza mbolea aina ya Naitrojeni kwenye udongo. Majani yake yanapopukutika na kudondoka ardhini huoza na kubadilika kuwa mbolea ambayo pia huboresha muundo wa udongo. Chakula cha mifugo. Maganda na majani ya mbaazi hutumika kama chakula kwa ajili ya kulishia mifugo.

Hali ya hewa
Mbaazi hustawi vizuri katika nyuzi joto 29 hadi 38, na hupandwa kuanzia usawa wa bahari hadi mita 1900 kutegemeana na aina ya mbegu. Kuna mbegu zinazostawi katika ukanda wa chini, wa kati na wa juu. Aidha kuna aina zinazostawi zaidi ya mita 2000 kutoka usawa wa bahari Zao hili huhitaji kiasi cha milimita 600 hadi 1000 cha mvua kwa mwaka. Aina za mbaazi za muda mfupi hutosha kustawi katika mvua kiasi cha milimita 250 hadi 370 kwa mwaka.

Udongo
Kwa kilimo chenye tija, ni vizuri kuotesha mbaazi kwenye udongo unaoruhusu maji, wenye mbolea kiasi na wenye tindikali kiasi cha pH kuanzia 5 hadi 7.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba la mbaazi litayarishwe mapema kwa kung’oa mabaki yote ya mimea pamoja visiki kabla ya kulilima.
Lima shamba kiasi kisichopungua sentimeta 30.
Lainisha udongo kwa kupitisha haro.
Tayarisha matuta au makinga maji kama shamba liko kwenye mteremko.
Kuandaa mbegu
Mbegu bora iliyochaguliwa vizuri na kuhakikiwa kiwango cha uotaji ziandaliwe.
Mbegu ziwekewe dawa ya kuzuia kuvu (fungus) kabla ya kupanda ili kuzuia magonjwa yatokanayo na mbegu na udongo.
Mbegu bora
Mbegu za mbaazi zimegawanyika katika makundi makubwa matatu nazo ni, mbegu za muda mfupi, mbegu za muda wa kati, mbegu za muda mrefu.

KUPANDA
1. Mbaazi za muda mfupi, zipandwe peke yake bila kuchanganya na mazao mengine. Nafasi: Kuwe na nafasi ya sentimeta 75 toka mstari na mstari, sentimita 20 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Kilo 5 hadi 6 zaweza kutumika kwa ekari moja.

2. Mbaazi za muda wa kati, zipandwe peke yake na katika mwinuko kutoka usawa wa bahari wa mita 1000 hadi 1880 Nafasi: Kuwe na nafasi ya sentimita 120 toka mstari hadi mstari na sentimita 30 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Waweza kutumia kilo 5 kwa ekari moja.

3. Mbaazi za muda mrefu, zipandwe peke yake katika mwinuko toka usawa wa bahari wa mita 1000 hadi 1880. Nafasi: Kuwe na sentimita 150 toka mstari hadi mstari na sentimita 50 toka shimo hadi shimo. Kiasi cha mbegu: Waweza kutumia kilo 5 kwa ekari moja

PALIZI NA KUPUNGUZIA MIMEA
Ni muhimu kupalilia mapema (angalau mara mbili kulingana na kiasi cha unyevu au mvua) na kuondoa magugu ambayo hushindana na mimea michanga. Miche ikiwa mingi kwenye shina husababisha mazao kuoza. Kwa hivyo ni muhimu kupunguza miche na kubaki miwili au kutegemeana na nafasi.

WADUDU
Kuna wadudu wa aina mbalimbali ambao kushambulia mbaazi, wakati zikiwa shambani au zikiwa galani.
1. Vidukari
Vidukari weusi wanaotembea kwa makundi na ambao huonekana zaidi katika sehemu changa za mimea kama vichomozo, matawi na majani. Wadudu hawa husambaa kwa wingi wakati wa majira ya ukame. Wadudu hawa hufyonza majimaji au utomvu ulio kwenye maeneo hayo na kusababisha mbaazi kubadilika rangi na kukauka. Udhibiti….Wadudu hawa hudhibitiwa kwa kutumia njia bora za kilimo na kufanya kilimo cha mzunguko.

2. Kunguni wa mifuko ya mbaazi
Kuna aina nne za wadudu hawa ambao ni Kunguni wa kahawia (Claiigralla spp), Kunguni wakubwa (Anoploenemies spp), Riptutasi (Riptortus dentipes), Kunguni wa kijani (Nezara viridula). Wadudu hawa hufyonza mbegu inayokuwa kupitia kuta za mifuko na kufanya mbegu kuoza na kukosa thamani ya kuwa mbegu na chakula cha binadamu. Udhibiti….Wadudu wanaofyonza mifuko ni vigumu kuwadhibiti kwani huruka kutoka sehemu moja na kwenda nyingine hivyo wanaweza kukusanywa kwa chandarua na kuangamizwa.

3. Mbawakavu wa maua na chavua (Blister beetles)
Wadudu hawa wenye rangi ya njano hula maua na kupunguza uzalishaji wa mifuko ya mbaazi. Katika eneo ambalo uzalishaji wa mbaazi ni mkubwa, wadudu hawa hufanya uharibifu mdogo kuliko katika eneo ambalo mbaazi huzalishwa kwa kiasi kidogo. Udhibiti….Wadudu hawa wanaweza kudhibitiwa kwa kuwaondoa kwa mikono na kuwauwa isipokuwa wakati wa kuwashika kuwepo na uangalifu kwani wakisumbuliwa huweza kutoa kemikali ambayo inaweza kuunguza mikono au mwili.

4. Funza wa vitumba (Maruca vitrata)
Wadudu hawa hutaga mayai kwenye vikonyo vya mbaazi kabla ya kuchanua au juu ya mifuko hula vikonyo vya maua na mbegu iliyoko ndani ya mifuko ya mbaazi. Udhibiti. Mkulima anaweza kuwadhibiti wadudu hawa kwa kufanya ukaguzi wa shamba mara kwa mara ili kufahamu uwepo wa wadudu hawa, pamoja na kutumia viuatilifu kulingana na maelekezo ya mtaalamu wa kilimo. Ni vyema ukaguzi ukafanyika wiki moja kabla ya mbaazi kuchanua na baada.

5. Inzi wa mifuko (Melanagromyza chacosoma)
Hawa ni wadudu wadogo weusi warukao na wanaotaga mayai katika kuta za mifuko za mbaazi inavyokua. Funza wake ni weupe na wana urefu wa sentimeta 3. Wadudu hawa hufanya uharibifu mkubwa kwa kula mbegu changa iliyopo kwenye mifuko. Udhibiti. Katika maeneo ambayo wadudu warukao ni tatizo, jamii ya mikunde inayokomaa kwa muda tofauti isipandwe kwenye shamba moja ili kuzuia mwendelezo wa kuzaliwa kwa inzi hawa hasa kila aina ya mikunde inapotoa maua. Pia mwarobaini waweza kunyunyiziwa mara 4 kila baada ya wiki kwa kiwango cha gramu 50.

6. Vithiripi (Megalurothrips spp. And Frankliniella schultzei)
Wadudu hawa wadogo na wenye rangi ya kahawia na mabawa ya njano huathiri mbaazi hasa kwa kufyonza utomvu kwenye majani na maua.Husababisha maua na vikonyo kusinyaa, kufifia rangi na kudondoka kabla ya kukomaa. Udhibiti. Kagua shamba kila mara ili kufahamu uwepo wa wadudu hao kabla ya mimea kuchanua ili kudhibiti mapema.

7. Vipekeche
Hawa ni wadudu wanaoshambulia mbaazi ikiwa ghalani. Wadudu hawa hutoboa mbegu na kutengeneza mashimo ya kutokea wadudu kamili.
KILIMO CHA DENGU: MAZINGATIO, CHANGAMOTO NA MASOKO

Dengu ni nafaka kama zilivyo nafaka zingine, ni zao la jamii ya mikunde pia ni zao la biashara, ni miogoni Mwa zao muhimu sana la biashara ukanda wa ziwa kwa sababu ya thamani yake Kuwa juu sana, zao hili hutumika pia kama zao la chakula kama mbonga , mchaganyo wa wali mseto , makande , kutegeneza Bagia , chiichiri na mengineyo mengi.

Kanda ya ziwa hili ndiyo Zao llinalotegenewa zaidi likiogozwa na zao la choroko kwa kuwa na thamani kubwa, hivyo zao hili ni zao muhimu kwa uchumi wa wa kanda ya ziwa.

Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma. Zao hili likilimwa vizuri linaweza kutoa mavuno ya kilogram 200 hadi 500 kwa ekari. Zao hili huchukua wastani wa siku135 kupandwa hadi kuvunwa.

HATUA MUHIMU KATIKA KILIMO CHAKE
Kilimo cha ndegu ni kilimo rahisi sana hakina usubufu sana kama yalivyo mazao mengine hasa ukifata utaratibu wa hatua za mwanzo.

Mambo ya kuzingatia
1. Kuwa makini na hali ya hewa ya mwaka husika kwa kuangalia ukame katika mbuga utaaisha lini pia hali ya mvua ikoje kwa maana kuwa msimu wa kulima huwa mwezi wa tatu mwishoni kwenye maeneo ambayo mbuga huwahi kukauka mapema yaani muda huo ndiyo watu huanza kuandaa shamba kwa kulilima mara ya kwanza kama hatua ya kuliandaa shamba pia hatua hii hufanyika mwenzi nne lakini iwe kwenye kumbukumbu sahihi kuwa ndegu kwa hali ya uzuri kabisa hulimwa mwezi nne na mwanzoni kabisa mwa mwezi wa tano kabla mbuga hazickauka .

2. Uchaguzi wa Mbengu, mbengu bora za dengu ni muhimu kuzifahamu na kuzitumia katika kilimo hiki, Ziko mbengu ambazo hazihimili magonjwa lakini zipo zinazohimili magonjwa na zinakuwa na uzito hii husaidia katika swala la uuzaji kwa maana ya kuwa mara nyungi dengu kwa sasa huuzwa kwa kilo ili mkulima apate faida zaidi

3. Baada ya kulima mara ya kwanza kama kuliandaa shamba unapaswa kulima mara ya pili na kupanda mbengu kwa kufata misitari au kufata tumba au vitalu au misingi itakayokuwa imeadaliwa.

4. Hakikisha dengu unapanda katika mbunga isiyo na maji yaliyotuama , unyevunyevu wa udogo wa shambani ndiyo hitaji muhimu la uoteshaji dengu hairuhusiwi kabisa kupanda dengu kwenye shamba lenye maji.

5. Ardhi inayofaa kwenye kilimo cha dengu ni shamba nyeusi au udongo mweusi ambao hutumika pia katika kilimo cha mpunga, mahidi, choroko na mengineyo .

6. Baada ya dengu kuota hakijisha hakuna maji yaliyotwama katika shamba lako.

7. katika ulimaji wa dengu palizi haina ulazima mara nyingi dengu haina palizi kabisa ukizigatia hatua za mwanzo za uandaaji wa shamba.

8. Dengu hutumia miezi mitatu mpaka kuvuna hivyo inajulazimu kusubiri ikauke mpaka hali ujano itokee kwenye mmea, mavuno ya dengu mara zato hufanyika kwa kung’oa mmea wote na kukusanya sample dogodogo ili kumaliza mapema mavuno yake baada ya hatua hiyo unaleta mkokoteni shambani unakusanya kwa mkokoteni nakupeleka sehemu kavu iliyosafi kwa ajili ya kutoa maganda ya zao la dengu, hatua ya kutoa maganda ya dengu inaweza fanyika kwa kienyeji kwa kupiga na miti au ikatumika kwa kitaalamu kwa kupiga .

na Tractor yaani tractor inapita kwa mzuguko kwenye navuno ya dengu yaliyosambazwa mpaka kuputua maganda ya juu ya dengu na kubaki dengu yenyewe tayari kwa biashara au kukoborewa tena kwa chakula.

9. Uhifadhi wa zao la dengu hauna chagamoto sana japo hushambuliwa na wadudu baada ya miezi mitatu bila kuweka dawa unapaswa kuhifadhi kwenye eneo la wazi yaani kama ni chumba kiwe na uwazi wa hewa ya kutosha.

CHAGAMOTO KATIKA KILIMO CHA DENGU
Zipo chagamoto kadhaa katika kilimo cha dengu kama ifatavyo;

1. Wakati wa kupanda huwa kunachagamoto ya mvua ambazo hujitokeza na kuharibu zao la dengu kwa kisukuma tunaita SHIBOJA yaani mvua za kuozesha dengu chagamoto hiyo ikijitokeza subiri maji yakauke katia mbengu upya kama zao limeathiriwa kidogo kama limeathiriwa sana unarudia shamba lote.

2 Chagamoto ya funza baada ya mmea kutoa maua . mmea ukitoa maua funza hushambulia kwa kasi kama eneo hilo liko na funza tiba ya funza hao nikupulizia dawa unaenda duka la kilimo watakupatia.

3. Chagamoto ya wadudu wakati wakati mmea unatoa zao lenyewe Wakati huu pia unapulizizia dawa kama wakijitokeza Jambo la funza na wadudu hujitokeza mara chache sana hivyo ni vyema kuwa na tahadhaRi hiyo.

4. Chagamoto ya panya Panya hujitokeza kwenye shamba wakati zao Linaanza kukomaa. wao hutafuna dengu kamili hivyo unaweza jikuta unapata hasara wakati dengu zilisitawi vyema, Utatuzi wa chagamoto hiyo ni kuwatega panya kwa sumu kwa ukanda wa mkoa wa shinyanga serikali hutoa dawa nasi huchaganya na mahidi nakusambaza pembezoni mwa shamba maana panya hutokea kwenye nyasi hivyo watakutana na mahidi nakuyala.

Chagamoto nyingine ni za masika unaweza lima mwishoni sana kwenye mavuno ukakutana na mvua.

5 Chagamoto ya uhifadhI Hapo kunachagamoto ya kushambuliwa na wadudu ndani ya miezi mitatu ya mwanzo unashauriwa kuhifadhi kwenye magunia nasiyo mifuko ya plastic.

Unashauriwa kutia dawa inaitwa AKTERIA mapema kabisa unapohifadhi kama unahifadhi kwa muda mrefu baada ya miezi mitatu unatia tena Au unaweza hifadhi kwenye mifuko maalumu ambayo imetiwa dawa kabisa na dani inakuwa kama mfuko wa sukari na upaswa kuifuga kitaalamu kama maeelekezo yalivyo .

Chagamoto nyingine ni ya soko naieleza hapa chini na utatuzi wake

HALI YA HEWA NA UDONGO
Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto kali na ukame sana huathiri mavuno yake, hupunguza wingi wa mavuno. Ni zao linalostahimili ukame, linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu.

Kama utakuwa unamwagilia basi epusha unyevu mwingi ikifikia kipindi cha maua hadi kuvuna. Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina tofauti tofauti wenye Ph 6-8. Udongo wenye asidi na base kidogo.

Kwa Tanzania zao hili linaweza kulimwa katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Singida, Morogoro, Shinyanga N.K. Lakini kwa sasa mikoa yaShinyanga na Mwanza ndio wazalishaji wakubwa wa Dengu.

UPANDAJI NA NAFASI
Zao hili huitaji mbegu kiasi cha kilogram15 hadi 40 kutegemea ukubwa wa mbegu husika. Zao hili hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua,unaweza kupanda baada ya kuvuna mazao mengine uliyopanda mapema.

Mbegu za dengu hufukiwa katika kina cha sentimeta 5 hadi 6 ili kufanya mazingira rafiki kwa bacteria wa rhizobia kufanya kazi. Zao hili usipande pamoja na vitunguu na tangawizi. Panda kwa kutumia drilling method-njia ya vifereji kwa nafasi ya mistari miwili ya sentimeta 15 na sentimeta 30 hadi 50 kwa mstari hadi mstari.

MBOLEA ZA VIWANDANI NA SAMADI
Mbegu unaweza kuzipanda baada ya kuziongeza inoculam kundi F na Pia Mbolea ya DAP kilogram 25 hadi 50 kwa ekari katika shamba lisilo na rutuba ya kutosha.

PALIZI
Palilia mapema shamba lako.

WADUDU WAHARIBIFU KWA DENGU
Dengu hushambuliwa na Mchwa wakubwa weusi, aphid wa njegere, funza wa vitumba, Inzi wa lucina n.k. wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu uonapo dalili za mashambulizi ya wadudu.

MAGONJWA YA DENGU
Dengu hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu. Hivyo kama eneo lako hushambuliwa na ukungu mara kwa mara basi puliza dawa za ukungu (FUNGICIDES ).

UVUNAJI WA DENGU
Zinavunwa mara tuu pindi vitumba vya chini vibadilikapo rangi kuwa kahawia angavu na vitumba vikiguswa hutoa sauti Mavuno ya dengu kwa heka yanaweza kuwa gunia 6,5,4 Inategemeana na eneo ulilolima linarutuba kiasi ngani na umefata taratibu zote.

Soko la dengu.
Soko la dengu ni la uhakika sana kwa maana ya uhitaji wa dengu katika soko la ndani na nje.

Kilimo cha zao la Choroko​

Choroko ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini na madini ya phosphorus na calicium.Zao hili likilimwa vizuri hutoa mavuno kati ya Kg 400 hadi 900 kwa ekari.

Udongo na hali ya hewa
Choroko hustawi katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji. Hulimwa kutoka mita 0 hadi 1500 kutoka usawa wa bahari japokuwa kuna mbegu nyingine zinaweza kukubali zaidi ya ukanda huu.Hili ni zao linalostahimili ukame.

Aina za Choroko
Kuna aina kuu mbili za choroko ambazo pia zimegawanyika katika makundi mawili,choroko nyeusi na choroko za kijani.
A) Choroko zinazotambaa , hizi ni choroko ambazo zinarefuka sana na hutambaa sehemu mbalimbali.
B) Choroko zinazosimama, hizi ni choroko ambazo zinakuwa kwa kusimama kwenda juu.

Kipindi kizuri cha upandaji wa choroko
Choroko hazihitaji maji mengi hivyo ni budi zipandwe mwishoni mwa msimu wa mvua,Pia zinaweza kupandwa katika shamba lililolimwa mpunga.

Nafasi cha upandaji wa choroko na kiasi cha mbegu
Choroko huitaji mbegu kiasi cha kilogram 8 hadi kumi kwa ekari moja.
Panda choroko zako kwa nafasi ya sentimeta 30 mastari na mstari na sentimeta 10 shina hadi shina (30 x10 )sentimeta au (40 x 8)sentimeta

Samadi na mbolea ya viwanda
Kama shmba lako halina rutuba ya kutosha unaweza kuongeza samadi kiasi cha tani tano kwa ekari na pia unaweza kupanda kwa kutumia mbolea ya NPK kg 50 kwa ekari.weka mbolea zote kabla ya kupanda.

Umwagiliaji
Kama umepanda kipindi cha ukame sana au unalima kilimo cha umwagiliaji basi mwagilia shamba lako upate unyevu wa kuotesha mbegu, kisha baada ya mbegu kuota kaa siku 6 hadi 10 na umawgilie tena. Mara tatu za kumwagilia zinatosha kwa choroko. Na palilia shamba lako mapema kuzuia magugu kuota ndani ya shamba lako na kwa palizi moja inaweza kutosha.

Magonjwa ya Choroko
1-yellow mosaic virus ( Ugonjwa wa manjano)
Dalili- mmea unakuwa wa njano na madoa ya njano katika majani.
Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili magonjwa.

2-Powdery Mildew (Ukungu)
Dalili-Majani yanakuwa na vidoti vya njano ambavyo vinabadilika kuwa vya kahawia au kijivu haraka na ambapo kunakuwa na unga unga katika majani.

Kinga na tiba-Panda mbegu zinazostahimili ukungu,Pulizia dawa za ukungu (Fungicide).
anza kupuliza wiki tatu baada ya mimea kuota na kuendelea kulingana na hali halisi.

3-Leaf spot (Vidoti katika majani)
Dalili-majani yanakuwa na vidoti vya mviringo na visivyo na umbo maalum ambapo katikati yanakuwa na rangi rangi ya kijivu na weupe na mistari ya rangi ya wekundu-kahawia au nyeusi-kahawia.ugonjwa huu husababisha hasara hadi ya asilimia 58 ya mapato.
Kinga na Tiba-Panda mbegu inayostahimili ugonjwa huu,Choma mabaki ya mimea hii na ile ya jamii moja baada ya kuvuna.Pulizia dawa za ukungu (Fungicide) Katika nafasi ya wiki mbili mbili kama eneo hilom linashambuliwa mara kwa mara na ukungu.

Wadudu
Kuna wadudu mbalimbali wanaoshambulia choroko kama vile aphidi,funza wa vitumba,nzi wa maharage.Wazui wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu baada ya mimea kuota, dawa kama karate, twigathoate, dimethote na nyinginezo zinaweza kutumika.

Uvunaji
Mara tuu choroko zinapofikia asilimia 85 ya ukaukaji zinabidi zivunwe ukichelewa zitapukutikia shambani.
 
Mkuu hii bei ya hi conflower imenishitua, yani gram25 ni ths30,000?au typing error? So inamaana gram 250 ambayo ni robo kilo in ths 300,000 right?so kilo 1 ni ths 1,200,000. Ikiwa utalima heka1 na ukapata 100hks inamaana una 120million right?

Ebu fafanua mkuu juu ya bei.
 
Dengu ni zao potential sana, linatumika ktk kutengeneza biskuti na chokoleti nadhani. Ni kweli nami nina taarifa lina soko zuri sana hasa katika viwanda vya kutengeneza biskuti sio India tu hata hapa Nchini na nchi jirani katika Afrika Mashariki.

Mkuu na mimi nimefikiria kulima hili zao, na hapa nipo katika mchakato wa kupata eneo huko wilaya ya Chemba, Dodoma.
Tuendelee kutumia thread hii kuelimishana juu ya kilimo cha zao hili na masoko yake.
 
Habari zenu wana jamii, nimejitokeza kutaka kupata msaa kwa undani kwa mtu anafahamu kilimo cha Dengu,

1. Mbegu za dengu zinapatikana wapi?
2. Matayarisho yake yaweje.
3. Namna za kuzipanda ikiwemo nasafi kutoka shins moja mpaka jingine, na umbali kutoka mstari mpaka. Matunzo yake zikiwa shambani.
4. Zinachukua muda gani tangu kupandwa mpaka kuvunwa.
5. Soko lake likoje.
 
Sabayi,

Kwenye hiyo Mikoa ongeza mkoa wa Mwanza na hasa Wilaya ya Missungwi. Ni kilimo kinachomuokoa Mkulima Mdogo baada ya zao la Pamba kuuawa. Ni zao linalilimwa baada ya Wakulima kuwa wamevuna Mazao mengine kama Mahindi, Maharage na Mpunga. Ni zao lisilohitaji Mvua nyingi (kwa uzoefu, sio utaalamu). Hivi sasa kuna Mbegu bora kabisa zilozotolewa na Taasisi zetu hapa hapa kama Ukiriguru, n.k.

Dengu ina Soko kubwa sana hapa Nchini ukiachilia Nje ya Nchi. Ukulima Oyee!:smiling:
 
Kwenye hiyo Mikoa ongeza mkoa wa Mwanza na hasa Wilaya ya Missungwi. Ni kilimo kinachomuokoa Mkulima Mdogo baada ya zao la Pamba kuuawa. Ni zao linalilimwa baada ya Wakulima kuwa wamevuna Mazao mengine kama Mahindi, Maharage na Mpunga. Ni zao lisilohitaji Mvua nyingi (kwa uzoefu, sio utaalamu). Hivi sasa kuna Mbegu bora kabisa zilozotolewa na Taasisi zetu hapa hapa kama Ukiriguru, n.k.

Dengu ina Soko kubwa sana hapa Nchini ukiachilia Nje ya Nchi. Ukulima Oyee!:smiling:

Juzi nimepita kutoka Shinyanga kwenda Mwanza hapo kupitia Old Shinyanga nimeona wakulima wengi sana wamepanda Dengu.
 
Juzi nimepita kutoka Shinyanga kwenda Mwanza hapo kupitia Old Shinyanga nimeona wakulima wengi sana wamepanda Dengu.

Ni ukweli usiopingika. Mwezi uliopita nilikwenda Kwimba na Missungwi, Wilaya za Mkoa wa Mwanza zinazopakana na Shinyanga. Nilipata nafasi ya kuongea na Wakulima kadhaa. Ninadiriki kusema kuwa huenda Dengu ndilo Zao la Biashara linalioongoza na linalowapa Wakulima matumaini kizidi mengine katika Wilaya hizo mbili.

Kwenye Nane-Nane ya Mwaka jana hapo Nyamhongolo, Mwanza nilioneshwa Mbegu mpya (hybrid) iliyotafitiwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru ambayo ni bora kuliko mbegu za kienyeji. Kwa ufupi Dengu, kama ilivyo Choroko, Mbaazi, Ufuta, n.k., ni fursa nyingine katika Kilimo!
 
Ni ukweli usiopingika. Mwezi uliopita nilikwenda Kwimba na Missungwi, Wilaya za Mkoa wa Mwanza zinazopakana na Shinyanga. Nilipata nafasi ya kuongea na Wakulima kadhaa. Ninadiriki kusema kuwa huenda Dengu ndilo Zao la Biashara linalioongoza na linalowapa Wakulima matumaini kizidi mengine katika Wilaya hizo mbili. Kwenye Nane-Nane ya Mwaka jana hapo Nyamhongolo, Mwanza nilioneshwa Mbegu mpya (hybrid) iliyotafitiwa na Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru ambayo ni bora kuliko mbegu za kienyeji. Kwa ufupi Dengu, kama ilivyo Choroko, Mbaazi, Ufuta, n.k., ni fursa nyingine katika Kilimo!

Uzuri ni kwamba wanapanda dengu wakishavuna mahindi/mpunga na haitaki mvua au maji mengi.
 
Wadau napenda kufahamu soko la mbaazi,kunde na choroko daresalamu maana ninampango nianze biashara hiyo kwa kununua choroko kutoka mtwara na kusafirisha dar naitaji mwenye ufahamu wa soko na hata changamoto zake
 
Hey guys, mimi ni mgeni lkn ni mwenyeji Sana kwa kupita humu ndani nimekuwa nafuatilia michango ya akina Malila na wenzie Muda mrefu, Sasa safari hii nimelima mihogo na choroko Tanga maeneo ya Marungu natarajia kuvuna mwezi wa 6 mwishoni mkae mkao wa kula Insha Allah
 
Mkuu mambo hayakuwa mazuri Sana ndege walizishambulia sana mlinzi wangu hakuwa makini kwenye ulinzi, hata hivyo choroko ilikuwa ni nyongenza tu kilimo kikuu kilikuwa ilikuwa ni zao la mihogo limekubali sana January natarajia mavuno mazuri tu mlio tayari nawakaribisha marungu Tanga
 
Back
Top Bottom