Muhtasari wa kilimo cha baadhi ya mazao jamii ya kunde

Nimefurahi kwa hamsa nzuri sana. Linalotakiwa hapa ni kumpata Mtaalamu aweze kutuelewesha kitaalamu kuwa ni udongo upi unafaa,ni hali ya hewa ipi inafaa, ni muda gani inachukua shambani, sokolake likoje ndni na nje ya nchi na namna ya kuyafikia masoko hayo pamoja na mambo mengine. Kama yupo aje atusaidie tuchangamkie fursa hii.
 
Mtaalam wa kilimo aje atujuze zaidi kuhusu ulimaji, maeneo/ aina ya aridhi inayofaa pia ni msimu gani. Maafsa ugani upo wapi?
 
Mtaalam wa kilimo aje atujuze zaidi kuhusu ulimaji, maeneo/ aina ya aridhi inayofaa pia ni msimu gani. Maafsa ugani upo wapi?
Nipo Arusha sema kilimo nataka nikifanyie huko HAI-KILMANJARO ENEO AMBALO HUWA NI KAME MKUU
 
Nadhani Geita pia linakubalika. Nataka kujua linachukua muda gani tangu kupanda hadi kuvuna, mahitaji ya zao hilo,masoko na utaalamu
 
Kwa wale wajasiriamali wanaohitaji kujiunga na group ya WhatsApp kwa masuala ya kijasiriamali nicheki 0762600100
 
wadau mm nahitaji choroko kama kg 50 nipo iringa ila sijui ntazipataje maana hapa iringa sokoni ni adimu sana kupatikana
 
ABC's ZA ZAO LA CHOROKO

Choroko ni moja ya mazao ya jamii ya mikunde hustawi eneo lenye mwanga wa kutosha pamoja na udongo wa tifutifu.pia masoko yake ni mazuri mfano kwa masasi 1300-1500@kg

Hakihitaji mvua nyingi na hakuna magonjwa yanayoathiri isipokuwa wadudu wanashambulia majani pamoja na choroko wakati za kuzaa hivyo suluhisho ni kupulizia dawa za kuu wadudu kama NINJA, KARATE, DUDU ALL e.t.c kila baaea ya siku 14 kuanzia wakati zinatoa maua.

Huchukua siku 60 hadi kuvuna japo hazizai kwa mkupuo yaani kadri unyevu ulivyo ndivyo nazo huzidi kutoa maua na kuzaa. Pia waweza mwagilia kama unavyolima kunde.

Katika kupanda tofauti ya shina na shina ni sm 35 na tofauti ya mstari na mstari sm 55.pia kila shina moja unatia punje 2-3 za choroko,halihitaji mbolea ila unahitaji kupulizia dawa ya kuuwa wadudu hasa wakati zinazaa walau mara 21.

Hivyo vijana tujishughulishe tupige kazi
 
Back
Top Bottom