Darasa Huru: Ufundi Laptop (Beginners To Advanced) PART 2 EP01: Tuijue Laptop Na Tuifungue Kisha Tuifunge

Mtwara Smart

JF-Expert Member
Jun 6, 2019
666
1,480
PART 2 EP01
Tuijue Laptop Na Tuifungue Kisha Tuifunge.

684727a43933f40a3ea594f1f1a08fb5.jpg


Wasalaam Wanandugu:

Tumekutana Tena Katika Darasa Letu Huru La Laptop Repair, Na Part 2 Hii Tutakuwa Tunaangalia Matatizo Ya Hardware Tu.

Tuanze Kwanza Na Utangulizi Wa Laptop Kwa Siku Ya Leo, Tujifunze Kuhusu Basic Concept Ya Laptop Hardware, Tujifunze Kufunga Na Kuifungua Laptop Yenyewe Na Elimu Kidogo Ya Laptop Charger.

Laptop ni aina ya Computer ambayo ni portable ina maana mtu anaweza kuibeba na kuhama nayo kutokuwa nzito sana na rahisi kubeba.

Laptop kiutaalamu ina part 2, hardware na software, hardware part tunayoangalia hapa ni Kitu Chochote Unachoweza Kukishika Katika Laptop Kwa Lugha Rahisi.

Laptop inapewa nguvu ya umeme kutoka kwenye charger na battery lake kama charger haitakuwepo.

Charger Nyingi Za laptop zina range Voltage Kuanzia 18V, 19.5V Mpaka 20V DC.

Swali: Nitajuaje Kiasi Cha Umeme Kinachotoka Kwenye Charger?
Je Laptop Yangu Inatakiwa Kupokea Umeme Kiasi Gani?

Jibu: Nyuma Ya Charger Zote Za Laptop Kuna Indications Ya Umeme Unaotakiwa Kuingia Na Kutoka, OUTPUT na INPUT, Na Pia Nyuma ya Laptop Zote Kuna Indication Ya Moto Sahihi Unaotakiwa Kuingia Kwenye Laptop Yako. ANGALIA PICHA CHINI

Altenative: Unaweza Kuangalia Voltage Range Google Kwa Kutumia System Model Na Brand Name Hii Utaiona Nyuma Ya Case Y a Laptop Yako Na Pia Imeandikwa Kwenye Motherboard.

Mfano: TOSHIBA C850-PSCBWE-OHFOONEN ( Unapofanya Kutafuta Details Au Kitu Cha Laptop Mtandaoni Hakikisha, Unamalizia Hizo Model Item Numbers, Watu Wengi Huwa Wanafanya Search Kwa Kuandika Tu Herufi Za Mwanzo Mfano TOSHIBA C850 Basi, Ukifanya Hivi Kuna Posibility Kubwa Ya Wewe Kupata Details Zisizo Sahihi)

Kipi Cha Kuangalia Kwenye Charger Ya Laptop Kama Fundi Au Wakati Unanunua Charger?

1. Voltage SAHIHI
2. Watts
(What Ndogo Hazitachaji Laptop Yako Au Zitaifanya Iwe Slowly Mfano: Kuna Watu Wakichomeka Charger Laptop Zao Touchpad Inakuwa Nzito)
3. Power Series (Laptop Nyingi Zina Power Series Moja, Means Kwenye Cord (Kile Kichuma Cha Charger Kinashabihiana Utoaji Wa Umeme Mfano: Pini Ya Kati Ni Ve+ Na Mzunguko Wa Duara Pembeni Ni Ve-, Lakini Laptop Nyingine Ni Tofauti)
4. Amps: (Kama utatumia charger yenye amps ndogo kuliko zinazotakiwa kwenye laptop, sio vizuri maana unaweza ukawa unachaji laptop kwa muda mrefu, au charger ikawa ina overheat sana au isicharge kabisa laptop yako.)
5. Case: (Kama Kuna Leakage Yoyote Kwenye Case Ya Charger Basi Achana Nayo, Kwa Maana Inaweza Kusababisha Jeraha La Short Kwa Mtumiaji)
6. Brand: Kama Wewe Ni Mtumiaji Wa HP Basi Tafuta charger ya Hp Maana Kuna Watu wengi huwa wanafoji charger za Dell Kwenye HP ambapo sio sahihi kwa maana charger nying za dell ni Njia 3 na HP ni Mbili Viceversa)

MATATIZO YA CHARGER

Kwa Fundi Wowote Wa Laptop Kituo cha kwanza cha kukimbilia ni charger ya laptop kwa upande wa hardware mfano: Laptop Haiwaki, Laptop Ina Blink, Laptop Haicharge, Laptop Inawaka Then Inazima Kabla Ya Booting.

Bahati mbaya sana laptop charger nyingi zimetengenezwa kiroho mbaya, huwezi kuifungua kwa screwdriver kwa maaana haina Screws, So Hawataki Uifungue Na Kuifanyia Repair Nadhani Sababu Ya Hatari Ya Short Ya Umeme. So Kuifungua Mara Zote Ni Kwa Kuivunja Mimi Huwa Natumia Hummering Method, Nagonga Nyundo Kwa Kutumia Screw Drive.

TATIZO LA 1
Power Cable (Flower), Imekufa Au Inamiss Njia Moja Hili Ni Tatizo Kubwa Kwa Maana Mara Nyingi Adapter Hawezi Kufa Kwa Sababu Ina Switching Power Supply Yenye Short Protection, ikitokea Fault Basi Inakata Moto Na Kuizima Kabisa (Utaona Adapter LED inazima Kama Vile Haina Moto)

UTAJUAJE
Kama Huna Multmeter Basi Tafuta Flower Cable Nyingine, Au Kwa Multmeter Tumia Diode Mode Ambapo utaangalia Continuity Ya Nyaya Zote Ambapo Kama Kuna Connection Basi Utasikia Beep Sound.

UTATUZI
Hizi Cable Ni Cheap Sana Kariakoo Huwa Wanauza 2500 Hadi 10000, So nashauri nunua tu nyingine, usiiunge, maana umeme unaopita hapa unaweza kusababisha majeraha kwako.

TATIZO LA 2
Charger Cord Imeharibika: (Inagusa Njia Nyingine Au Chuma Kimekatika Au Chuma Kimekosa Umeme Baada Ya Wire Kuachia, Hii Ni Common Sana kwa charger za DELL Especially za njia tatu, ambapo utaona charger inawasha laptop lakin haichaji, pin ya kati ambayo ni ya signal inakuwaga na 4V ndiyo inakuwaga imemis hivyo ukifanya Test kwa Multimeter utaona una Njia Mbili Zenye 19V Lakin Charger Haichaji.

UTAJUAJE
Pima kwa kutumia Multimeter All Three Pins Kwenye Chager Cord lazima Ziwe Na Umeme, Au Ukichomeka Charger Halafu Ile LED Kweny Adapter Ikizima, au Ukiona Cheche Kwenye Charging Port Wakati Ukichomeka Charger.

SULUHISHO
Kama Kuna Uwezekano Wa Kuzi Arrange Tena Hizo Charger Basi Fanya Hizo Then Rudishia Na Hot Glue, Ikishindikana Basi Badili Adapter Nzima.

TATIZO LA 3
Adapter Kuungua: Hii sasa ni tatizo kubwa ila sio sana kwa maana ni mara chache sana kutokea kama charger adapter imeungua, suluhisho ya hili ni kufanya manunuzi ya adapter mpya kama huna skills advanced za electonics kwa maana utakuwa una deal na live AC Current, hivyo upo katika hali kubwa ya kupata madhara yatokanayo na umeme.
Kwa advanced learner unaweza kuipasua na kuangalia shida na mara nyingi inakuwaga ni Shorted Cap.

TUTAIANDALIA SESSION YAKE ADVANCED LAPTOP CHARGER REPAIR KWA SASA TUISHIE HAPA

TUIFUNGUE LAPTOP


Moja kati ya vitu muhimu na vya kuvifahamu sana na ni mtihani wa kwanza kwa mafundi wengi ni kujua kufungua laptop (DISASSEMBLE) Pamoja na kuirudishia, Hapa ndipo unapomaliza kuifunga laptop yote na kukuta Screw Zinabaki Hazijafungwa na hujui za wapi.
Kabla Hujafungua Laptop Hakikisha Una Vitu vifuatavyo:

1. Screwdrives (Kariakoo Set Elu 5-10)
2. Pry Tools (Hii kwa ajili ya kutolea lock za case ya laptop naa simu)
3. Tweezers (Kazi nyingi lakin hapa kubwa ni kutolea Ribbon cable)
4. Screw Container and Organizers (Hii ni simu haswaa kwa wale wanaobaki na screw baada ya kufungua)
5. Meza Safi Ya Kufanyia Kazi ( Hakikisha mahali unapofanya kazi ni safi na salama, hakuna vimiminika, hakuna uchafu uchafu, pako na mpangilio mzuri, hii itakurahisishia kutopoteza muda na vifaa)

HATUA ZA KUFUNGUA LAPTOP

1. Hakikisha laptop haina chanzo chochote cha umeme, Toa battery na hakikisha umeichomoa kwenye charger. (Hii inasaidia kuepuka short wakati wa kutoa cable cable slot zake, na pia kuepuka madhara ya umeme kwako pia inagawaje umeme unaokuja kwenye motherboard sio mwingi)
2. Anza Kufungua Screws Zinazohusika Na Vitu Muhimu Nyuma Ya Laptop, Kuna Screw Za KEYBOARD, CD DRIVE na Za Hard Drive Kwenye Bahadhi ya laptop za zamani haswaa dell mfano: 620, So anza kufungua kwanza hizi kama zipo.
3. Fungua Screw zote za nyuma ambazo zipo katikati au zimeshikilia part ya nyuma inayoweza kutoka kirahisi mfano: Cover la nyuma lenye Hard drive, RAM na Network card.
4. Jaribu Kutoa Hilo cover la nyuma, kama lipo na kama ukifanikiwa basi fungua nut nyingine zote unazoziona nyuma ya laptop yako.
5. Jaribu kuitoa keyboard na kama utafanikiwa basi fungua pia screw zilizopo chini ya keyboard ambazo huwa zinashikiria motherboard moja kwa moja. HAPA KUWA MAKINI NA CONNECTOR YA KEYBOARD NI RAHISI KUKATIKA
6. Hakikisha screw zote zimeisha, Then Anza Kujaribu Kutoa Cover Lolote Laptop Kwa Kutumia Pry Tools Fanya Taratibu Kubandua Ili Usije Vunja Lock Za Case, kwa laptop nying cover la juu ndio linatoka then la chini ndio linashikilia keyboard ila usikariri, laptop mpya kama Lenovo Case ya chini huwa inatoka kwanza, HAPA KUWA MAKINI SANA NA CONNECTOR ZA TOUCHPAD, SPEAKER, POWER BUTTON, Hakikisha zote umezichomoa.

7. Ukifanikiwa Vyote Hivyo Basi Utakutana Kitu Kama Hiki Hapa Chini, Wewe ni Shujaa Kwa Part Hii

Sio vitu vigumu ukijifunza unaweza.

1b6a0369cc014912888dfb2eb4decf37.jpg



Toshiba-SatelliteA45-hinges-19.jpg


Naomba Kwa Leo Tuishie Hapa,

Softcopy Ya Notice Hizi Imeambatanishwa hapo Chini.

Tukutane Wiki Ijayo Kwa Ajil Ya PART 2 EP02.

Usisahau Pia Kupita Hapa Kwa Utangulizi Wa Laptop Repair Upande Wa Software PART 1 EP01
.


Wasalaam

Mtwara Smart
 

Attachments

  • TUIJUE LAPTOP NA TUIFUNGUE KISHA TUIFUNGUE.pdf
    785.7 KB · Views: 124
Upo vizuri ila naona ukiiweka kwenye Uzi mmoja inapendeza zaidi, muhimu ni kuweka namba ya page uhusika ya topic flani inaanzia wapi.
 
Sijajua Mkuu, But Practice Na Complication Za Kila Siku Za PC

Mkuu laptop yangu nimeiwasha jana ikawaka na kunipeleka mpaka sehemu ya kuweka password ile nimeweka tu nika press ENTER ikaanza kuleta rangi nyeupe screen nzima aisee.

Tatizo linaweza kuwa ni nini mkuu...?
 
Mkuu laptop yangu nimeiwasha jana ikawaka na kunipeleka mpaka sehemu ya kuweka password ile nimeweka tu nika press ENTER ikaanza kuleta rangi nyeupe screen nzima aisee.

Tatizo linaweza kuwa ni nini mkuu...?
Hata Uki Restart Bado Hivyo Hivyo
 
Mkuu laptop yangu nimeiwasha jana ikawaka na kunipeleka mpaka sehemu ya kuweka password ile nimeweka tu nika press ENTER ikaanza kuleta rangi nyeupe screen nzima aisee.

Tatizo linaweza kuwa ni nini mkuu...?
Next time ukitaka msaada ambao ni technical weka full details za kifaa chako....
Mfano.
Brand and model
Hadware specifications
-Ram
-HDD
- processor
- graphics

Na pia tabia za ajabu ambazo umewah kuziona kwenye kifaa chako kabla hakijawa mahututi.

Unaposema laptop ziko za aina nying sana.
Na troubleshooting procedures zinakuwa tofaut hata Kama ni brand ya manufacturer mmoja.
 
Asante sana mtoa mada...... Uzi umeenda vizur kabisa....
Kwa kuongezea tu hapo ukitaka kufungua charger ya laptot haina haja ya kuvunja, chukua petrol na kitambaa. Loweka kitambaa kwenye petrol then pakaza hiyo petrol kwenye mstari wa maungio ya hiyo charger...
Hapo ni dk 1 tu utaona ile mistari inafumuka vizuri kabisa bila kutumia nguvu.


Tahadhari ni muhimu sana wakat unataka kufanya repair ya adapter, umakin unahitajika sana maana AC part ya power supply inafanya rectification kubwa sana ya umeme na madhara yake ni makubwa.
Please handle this with care and precautions.

Asante
 
Next time ukitaka msaada ambao ni technical weka full details za kifaa chako....
Mfano.
Brand and model
Hadware specifications
-Ram
-HDD
- processor
- graphics

Na pia tabia za ajabu ambazo umewah kuziona kwenye kifaa chako kabla hakijawa mahututi.

Unaposema laptop ziko za aina nying sana.
Na troubleshooting procedures zinakuwa tofaut hata Kama ni brand ya manufacturer mmoja.

Next time ukitaka msaada ambao ni technical weka full details za kifaa chako....
Mfano.
Brand and model
Hadware specifications
-Ram
-HDD
- processor
- graphics

Na pia tabia za ajabu ambazo umewah kuziona kwenye kifaa chako kabla hakijawa mahututi.

Unaposema laptop ziko za aina nying sana.
Na troubleshooting procedures zinakuwa tofaut hata Kama ni brand ya manufacturer mmoja.

Daaaah nitashindwa kujibu kiufasaha jibu lako coz sasa hivi nimeipeleka kwa jamaa yangu ambaye aliitengeneza kwa mara ya mwisho ili-cost around 90k sasa ni almost mwezi tu inafanya hivyo.

Mwanzo ilikuwa ukii-charge haiingizi charge wala haiwaki jamaa akasema motherboard imekorofisha tukanunua nyingine pamoja na adaptor akaiweka sawa ikawa inapiga mzigo kamazing kawaida.

Sasa juzi nili-install FL Studio kwa kutumia flash sasa sijui ilikuwa na virus hata sielewi matokeo yake ndio ikaleta hilo tatizo mkuu.

Ila kwa haraka haraka brand ni Lenovo, ram 4,HDD 500, vitu vingine nashindwa kutaja coz niko mbali na mashine mkuu. Thanks.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom