Darasa Huru Part 4: Umuhimu Wa IT Rescue Bag Kwa Fundi Computer/Simu

Mtwara Smart

JF-Expert Member
Jun 6, 2019
666
1,480
Habari zenu wakuu na poleni na majukumu, Leo ningependa tujue umuhimu wa I RESCUE BAG Kwa Fundi Computer Na Simu, Vitu Hivi Ni Muhimu Sana Kwa Fundi Yoyote Anayetaka Kutoa Huduma Express, Delivery Na Outreach.

IT RESCUE BAG
Ni Mfuko Au Kitu Chochote Kinachoweza Kuhifadhi Vitu Muhimu Ambavyo Fundi Computer Au Simu Anatumia Akiwa Nje Ya Eneo La Kazi.

Rescue Bag Inatumika Pale Ambapo Fundi Anapata Kazi Nje Ya Ofisi Na Mteja Anaona Kazi Kuja Ofisin, Lakini Pia Inatumika Pale Ambapo Mteja Anahitaji Kuhudumiwa Kwa Dharula Akiwa Eneo Lolote, Kazi Nyingi Za Namna Hii Huwa Na Malipo Ya Ziada Tofauti Na Kazi Za Ofisini.

UMUHIMU WA IT RESCUE BAG
1.Unaogeza Idadi Ya Wateja Wa Muda Wote.

2. Inarahisisha Kazi Za Nje Ya Ofisi

3. Inasaidia Kupunguza Muda Wa Kuandaa Vifaa Vya Kazi

4. Inampa Uhuru Mteja Kupata Huduma Mahali Popote

5. Inakuza Jina La Biashara Na Kukupa Faida Zaidi.

6. Inarahisisha Maandalizi Ya Kazi Unayoenda Kukutana Nayo.

VITU VINAVYOTAKIWA KWENYE IT RESUCE BAG
Kwa kuwa wewe kama fundi Computer Au Simu Haujui Ni Kazi Gani Utaitiwa, Inaweza Kuwa Ya Hardware Au Software Kwa Upande Wowote Simu Au Computer, Hivyo Idadi Ya Vifaa Inatakiwa Iwe MakinI Na Isiwe Na Vitu Vingi Kama Ifuatavyo;

Drive Tool Set (Vifaa Vya Kufungulia Pair Moja Inatosha)

External HDD (Yenye Software Zako Zote Na Laptop Na Crack Box Za Simu)

Flash Drive Mbili ( Moja Iwe Na Multboot Ya OS Na Nyingine Empty)

Portable Hot Air Gun (Hizi Zinauzwa 50 HADI 65 Kariakoo)

Portable Soldering Iron

Portable Multimeter (Zinauzwa 10 had 30 kariakoo)

Flux

Tweezers 2

Soldering Wire

Bag/Kibebeo Chochote

Laptop 1 (Hakikisha Inaweza Kukaa Na Chaji)

USB Wire 3 (Type C, Normal Android Na Iphone)

Tukutane Tena Wiki Ijayo Kwa Ajili Ya Somo Linalofuata Litakalohusu ADVANCED WINDOWS INSTALLATION FOR TECHNICIAN.

Kwa Matatizo Yoyote Ya Computer Na Simu, Tuwasiliane

Mtwara Smart Group
Tiffany Road, Near Skylline Apartment
Chikongola, Mtwara

+255 624 410 406

Wasalaam
 
Ila tatizo we ndo wakule ndanda Kuchele.

Ukiinama nchale ukisimama nchale na ukikimbia nchale.

Powaa ila ungesogea town ingekuwa vyemaaaaaaaa
 
Back
Top Bottom