Darasa huru la ujenzi chini ya program ya UVIMO maktaba

frabel

Member
Mar 13, 2021
96
60
Uvimo Maktaba
UVIMO tunafaya kazi zote kwenye nyumba pamoja na mafunzo

Tunatambua ahadi yetu ya kuangazia namna Uchaguzi wa ramani inavyoweza kuongeza gharama za ujenzi.

Je, uchaguzi wa ramani unaweza kupunguza au kuongeza gharama za ujenzi?

Jibu ni ndio.

Uchambuzi wetu utaanzia baada ya ramani kukabidhiwa kwa mtathimi, hapa tutapata hoja ya kuongezeka kwa gharama za ujenzi.

Kimsingi, ramani ikisha chorwa ,mtathimini hutumia ramani hiyo kukadiria vifaa jenzi na kufanya makisio ya kiasi kitakacho tumika.
Kumbuka mtathimini hutumia vipimo vilivyo ainishwa katika ramani kukadiria vifaa jenzi.

Mtathimini hukabidhi kwa mpimaji wa msingi.

Katika hatua ya upimaji msingi daima nyumba huongezeka au kupungua hapa. Na kama ni nyumba kutokulingana kona basi chanzo chake ni ktk hatua hii.

Kama mtathimini alifuata kanuni za kutathimin, na mpimaji asifuate principal basi, utashuhudia uhitaji wa ongezeko au baki salia ya vifaa jenzi kuanzia msingi hadi hatua ya mwisho.

VISABABISHI VYA ONGEZEKO LA GHARAMA ZA UJENZI
1-Vipimo.
Ongezeko lolote la vipimo hupelekea uhitaji wa mahitaji zaidi na huu ndio msingi wa gharama.
Hi huathiri ,tofali, sementi, maji, mchanga, tiles, bati ,rangi n.k

2-KONA NYINGI
Kila nyumba ina kona ,
Karika kuchora ramani, kila kona ina nguvu ya kuongeza gharama.
Chukua nyumba mbili zenye ukubwa sawa na vyumba na mengine sawa, ila tofauti yake iwe katika mpangilio ( floor layout )
Yupo mmoja atalazimika kuongeza kona (vikwapa) ili apate mlalo mzuri wa vyumba vyake.
Mwisho usipo chagua mlalo mzuri utakupa kutana na gharama changamfu.

3-UTAWANYAJI WA VYUMBA NA VITUO VYA MAJI -complicated dr
Vyumba, vyoo, bafu , dinning na jiko vikisha tawanywa wakati wa uwekaji mfumo wa maji kwenye nyumba ya ndoto yako itakugharimu zaidi.

UCHAGUZI BILA UTULIVU
Kuna watu hawajitulizi wakati wa uchaguzi ramani , na hujikuta wakichagua kitu ambacho si hitaji lao, ba baada ya kujenga hujikuta wakibomoa bomoa kwa lengo la kuongeza au kupunguza kwa dhana ya manoresho. Hii huwakuta wengi hasa ambao hawakutaka ushauri au hawakushirikisha wataalam wa kada.

Kumbuka
Kama nyumba yako inajengwa na hakuna engineer/mtaalam msimamizi hasa nyakati za uchoraji au upimaji na kuendelea ,basi tegemea makosa mengi. Kwetu uvimo tuna wataalam wasimamizi hasa ktk baadhi ya hatua.

Mfano
Kuset nyumba/msingi
Kuseti upauaji
Kuset bomba -I
Kuset umeme-I
Kuset floor
Kuset brandaring

Hapa viongozi wasimamizi lazima wawepo.

Hata hivyo ,richa ya kuwa tuna ramani za ndoto za nyumba zetu, bado tunahitaji ushauri wa wataalam.
Haigarim chochote kupata mawzo mchanyato kwa umakini.

Uvimo tunaendelea na darasa huru chini ya UVIMO MAKTABA kwenye kupitia kundi letu la -WhatsApp

Wasiliana nasi kwa
0629361896
0753927572-WhatsApp

Katika angazio lijalo MAKTABA itaangazia sababu za ubovu wa nyumba au baadhi ya maeneo ya nyumba.


FB_IMG_1632710481368.jpg


IMG-20211012-WA0038.jpg
 
Uvimo Maktaba
UVIMO tunafaya kazi zote kwenye nyumba pamoja na mafunzo

Tunatambua ahadi yetu ya kuangazia namna Uchaguzi wa ramani inavyoweza kuongeza gharama za ujenzi.
Haya mambo ya Mivumo sasa sio Uvimo tena😅😅😅
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom