Darasa huru, Jifunze hapa kusuka amplifiers

Unasuka kwa gharama gani na vipi kuhusu ubora mkuu? Unapatikana wapi
Nipo singida mkuu garama ni kulingana na wewe unataka ya ukubwa gani mkuu afu kuhusu ubora sijawahi pata malalamiko kwa amp nazosuka mm kwahiyo usijali kua na amani mkuu we unahitaji ya ukubwa gan na unaenda kutumia kwenye spika za aina gani mkuu
 
Mtililiko wa somo unaendelea
Tumeshaangalia power supply na amplifier yenyewe
Ila kuna kitu muhimu sana san sana chakukitambua zaidi
Ikumbukwe kua hakuna amplifier ya bass au ya twita au ya mid ila wewe unachokitaka ndio utakachokipata
Kwa mfano tuchukulie kichwa cha semi la scania
Unaweza kuvutia contena
Pia unaweza kuvutia tela lakawaida au kupigia misele chenyewe (masikhara) au vyovyote vile
Hivyo hivyo ndivyo amplifier kama amplify ilivyo
Unaweza ingiza freqnc za bass ikapiga bass au mid au tweta
Najua hujanielewa....... ila taratibu
Maana yangu ni kua ukisuka amplifier itakupa mziki wa stereo au mono tu
Ambao utasikia vocal na beat na mambo yoote kwenye spika moja hiyo hiyo ila ili idunde kama subwoofer za nyumbn na magari kama zilivyo hapo unahitaji kitu kinaitwa operation amplifier (op amp)
Ambayo hiyo op amp itapokea signal kutoka kwenye deki au simu kisha itapokea ili kuzitengeneza!!!!


Je kwanini nasema kuzitengeneza
Ikumbukwe kua assume una amplify 3 umezisuka
Unataka moja ipige bass moja twita kari nyingine iimbe maneno yasikike utafanyaje kutengeneza hizo signals tofauti?
Hapo unahitaji op amp ili izitengeneze hizo sauti tofauti tofauti ili zisikike kwenye amplify zako
Na opamp huongeza nguvu ya amplify yaani kama vile turbo kwenye gari
Kwahyo signal zitatoka kwenye deki zikiwa stereo (naposena stereo namaanisha mziki kama wa kwenye earphones)
Kisha opamp itazipokea itaziongezea nguvu na kuzigeuza
Kisha zitaenda kwenye amplify
Kwahyo amplify itaongezea nguvu mziki ule ulioingia kutoka kwenye op amp!


Kwahyo amplify haibadilish aina ya muziki
Yenyewe inaongezea nguvu mziki ulioingia
Kazi yakubadilisha ndio hizo opamp na equalizer
 
Napenda sana electronics, nimepata vitabu ili niweze kupata basic ... Kisha nitakutafuta mkuu.

Hapo kwenye soldering gun unashauri nichukue ya aina ipi? (Yenye ubora)

Kwako kelphin kepph
 
Now we go....
Baada ya kupata umeme tunakuja kwenye amplifier yenyewe
Ambayo msukaji yani wewe mwenyewe utaamua usuke kwa kutumia nini yaani ic Au transistor
Nikukumbushe tu kua unapoanza kusuka lazima uwe na imaginations kichwani ya aina ya sound unayoitaka
Kisha ndio uta select aina ya circuit (tuite ramani) unayotaka
Na hizi ic zimetofautiana uwezo
Kwahyo kabla ya kusuka utachagua ic na kila ic ina specification zake yaani ina mashart na maelezo yake kuihusu yenyewe
Kwamfano kuna ic kama TDA2050 na nyingine TDA 7379 hizi zoote ni za amplifier lakini kila moja inauwezo wake na mashart yake
Kwamfano hiyo 2050 inaingiza hadi volts 25 na inakupa hadi watts 50 lakini ni inakupa channel moja tu (kuhusu channel ntakuelezea baadae)
Lakini hiyo 7379 inakupa channel 4 ila ina watts 38

Sasa basi kabla ya kusuka kujua unachohitaji ni kitu cha muhimu sana
Kwahivyo basi ni muhimu kuisoma ic husika kabla yakuanza kuitumia il kuijua kabla yakuanza kuisuka
Hiyo itakusaidia usiunguze na kuiharibu
Na hiyo itakupa hasara sana.
Kwa wale wenye android wanaweza ku download datasheet za ic husika kwa kuandika neno pdf mbele kisha ita downtown
Kwamfano
Andika Tda 2030 pdf download ukisha download itakuja mfano wa kitabu kisha utakisoma ili kusijua
Na waweza download nyingi ili kuzijua kwa wingi


TDA 2050
.......2030
........7379
........2040
........2003

KA2206
LA4440
na nyinginezo nyiiiiingi mno
(Utachagua wewe tu kulingana na matumizi yako)
Kwanini nasema kulingana na matumizi yako

Kwa mfano wewe una sora hizo tda 2050 zinaweza kua sio rafiki kwako kutokana na umeme wako
Kwahyo itakubid utumie za single power supply ingawa zote ni ic na zote zina fanya jazi moja.
Mkuu Ic ya sauti ya sabufa ya sunder inaungua mara kwa mara je niweke ipi ambayo itaweza kuhimili, sabufa volme yake mwisho ni 60, asante
 
Mkuu Ic ya sauti ya sabufa ya sunder inaungua mara kwa mara je niweke ipi ambayo itaweza kuhimili, sabufa volme yake mwisho ni 60, asante

Volume zile ni programed digits hazina uhusiano na chochote
Ndio maana yako inaenda hadi 60 wengine 50 lakin uwezo ni sawa!

Kuhusu kuunguza ic ni kwasababu kua
Speaker ndani ina coil ile coil ina insulator (rangi)
Kwahyo unapopiga mziki ile rangi inakua inapukutika Kwahyo coil inashikana inapunguza ohms ya speaker
Ukija kupima inakupa 4ohms ile ile ila wakati huo speaker inakua imepoa


Solution weka speaker nyingine mpya uangalie
 
Volume zile ni programed digits hazina uhusiano na chochote
Ndio maana yako inaenda hadi 60 wengine 50 lakin uwezo ni sawa!

Kuhusu kuunguza ic ni kwasababu kua
Speaker ndani ina coil ile coil ina insulator (rangi)
Kwahyo unapopiga mziki ile rangi inakua inapukutika Kwahyo coil inashikana inapunguza ohms ya speaker
Ukija kupima inakupa 4ohms ile ile ila wakati huo speaker inakua imepoa


Solution weka speaker nyingine mpya uangalie
Zinauzwa kweli speaker mkuu
 
Back
Top Bottom