Daraja la umoja ni matumizi mabaya ya rasilimali zetu

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Daraja la umoja linalounganisha Tanzania na Msumbiji ni miongoni mwa miradi ya serikali ya ccm ambayo imetumia fedha nyingi bila kuwa na manufaa ya aina yoyote. Daraja lilifunguliwa kwa mbwembwe lakini cha ajabu halitumiki na watu wanaendelea kutumia mitumbwi.
Miradi ya aina hii ni ile inayotekelezwa kwa pupa bila kuwepo upembuzi yakinifu, na kwa staili hii nchi itaendelea kuwa masikini ingawa imejaliwa rasilimali nyingi.
 
Mkuu,

Umechunguza sababu ya kutotumika kwake na watu wa pale?

Mazoea, gharama, ukosefu wa usalama...?
 
Hakuna barabara inayounganisha pande mbili za daraja! Kilichofanyika ni sawa na kununua mouse pad wakati huna computer!


Mkuu,

Umechunguza sababu ya kutotumika kwake na watu wa pale?

Mazoea, gharama, ukosefu wa usalama...?
 
Hakuna barabara inayounganisha pande mbili za daraja! Kilichofanyika ni sawa na kununua mouse pad wakati huna computer!

Nakubaliana nawe, nilishafika pale Mtambaswala, barabara haipitiki vyema, yaani daraja zuuuri ila barabara hakuna. Ni kilometa kumi tu zilizotengenezwa kila upande kutokea pale kwenye daraja

umoja bridge.JPG

Hapa ni upande wa Msumbiji siku ya ufunguzi
 
Mipango mibaya, Njiapanda ya kuelekea Masasi, Mtwara na Mtambaswala ipo hivi unategemea nini?


Mangaka.jpg
 
Back
Top Bottom