singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
NI eneo la Vijibweni na Kurasini wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam, ndipo utakapolikuta daraja la kisasa linaloning’inia kwa nyaya mbalimbali ambazo kiitaalamu ndio zinazobeba uzito wa magari na watu wanaolitumia daraja hilo.
Ukifika eneo hilo, utashuhudia mandhari ya kuvutia ya barabara za kisasa zilizopambwa na taa za rangi mbalimbali, hasa nyakati za usiku pamoja na barabara za juu zinazoelekea pande mbalimbali za jiji hilo la Dar es Salaam. Daraja la Nyerere ni daraja la kipekee kujengwa nchini Tanzania na Afrika Mashariki na Kati, kutokana na ukweli kuwa ni daraja la kwanza kujengwa baharini lakini pia ni daraja lililojengwa kwa gharama kubwa kutokana na ujenzi wake kutumia teknolojia ya kisasa zaidi katika eneo la kuhimili uzito.
Urefu wa daraja hilo lililopewa jina la muasisi wa Tanzania na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere ni mita 680 na upana wa mita 32, na lina barabara sita, tatu zikitoka Kigamboni kwenda Kurasini na tatu kutoka Kurasini kwenda Kigamboni. Aidha daraja hilo lina urefu wa mlazo wa kilometa mbili na nusu.
Ukweli ni kwamba mtindo wa ujenzi wa daraja hilo ni wa kipekee katika nchi za Afrika Mashariki na Kati kwa kuwa linakuwa daraja la kwanza kujengwa kwa mtindo wa kuning’inia ambao kwa lugha ya kitaalamu unaitwa ‘cable stayed bridge’. Kumalizika na kuanza kutumika rasmi kwa daraja hilo, kunahitimisha usemi maarufu unaosema hakuna marefu yasiyo na nchi na waswahili husema ‘hayawi hayawi sasa yamekuwa’.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba daraja hilo limekuwa likisubiriwa kwa hamu na wakazi wa Dar es Salaam hususani wa maeneo ya Kigamboni kwa muda mrefu. Historia ya ujenzi wa daraja hilo, inaanzia miaka mingi iliyopita 1930s ambapo kumekuwepo na mipango na mikakati ya kujenga daraja hilo ikiwa ni moja ya njia ya kuwarahisishia wakazi wa ‘kisiwa’ hicho cha Kigamboni usafiri wa kufika eneo la katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Pamoja na kwamba ujenzi wa daraja hilo ulionekana kama ndoto isiyotimia hasa kutokana na ukosefu wa fedha wa Serikali na suala lenyewe kuchukua muda mrefu, sasa hali imebadilika kwani tayari ujenzi wake uko katika hatua za mwisho lakini matumizi ya daraja hilo, yameshafunguliwa rasmi. Kwa mujibu wa Meneja Mradi wa Ujenzi wa daraja hilo la Nyerere, Mhandisi Karim Mattaka kutoka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) daraja hilo ni imara na litaweza kudumu na kutumiwa na watanzania kwa zaidi ya miaka 100.
Anasema daraja hilo linahusisha mihimili ya chini 202, vitako vya juu ya mihimili ya chini, nguzo fupi 20, sehemu ya daraja iliyoungana na barabara ya lami, daraja kuu na nguzo ndefu. Naye Mkurugenzi wa shirika hilo, Profesa Godius Kyarara, anasema ujenzi wa daraja hilo uliogharimu kiasi cha Sh milioni 214.6 umetokana na ushirikiano baina ya Serikali na shirika hilo, ambapo NSSF ilichangia asilimia 60 na Serikali asilimia 40 ya gharama za ujenzi wake.
Anasema daraja hilo limejengwa na kampuni ya China Railway Construction Engineering Group ikishirikiana na China Major Bridge Engineering kwa takribani miezi 51 kwa gharama hiyo ya Sh bilioni 214.6 na msimizi wa daraja hilo gharama yake ni Sh bilioni 7.
“Daraja hili lina barabara za maingilio zenye urefu wa kilometa 2.5 ambazo zimekamilika kwa kiwango cha zege la lami. Lakini pia kwenye eneo la daraja hili kuna kituo cha polisi ambacho kitakuwa na mahabusu. Tutakuwa tunakamata watu wakorofi wasiotaka kutii sheria na kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa daraja,” anasema Kyarara. Anafafanua kuwa daraja hilo litakuwa na mizani ya kupima magari ya kubeba mizigo yatakayokuwa na njia yake maalum ili yasisababishe foleni kwa magari mengine. “Daraja hili pia litakuwa na ofisi mbalimbali, kamera kwa ajili ya kuangalia mwenendo wa daraja, tutakuwa na watu wa usafi muda wote kwa sababu daraja hili litakuwa la kimataifa na la mfano na pia kutakuwa na vyoo ambavyo vitakuwa vya kulipia,” anasema.
Anasema ili daraja hilo liweze kuwa na ufanisi litakuwa na ujenzi wa upanuzi wa barabara zinazopokea na kuleta magari darajani kama vile ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara yenye urefu wa kilometa 1.5 kwa upande wa Kigamboni na Kurasini. Ufanisi mwingine utatokana na upanuzi wa barabara ya Vijibweni- Mjimwema, upanuzi wa barabara ya Feri-Kibada, upanuzi wa barabara ya Bendera Tatu-Kamata ambayo inatarajiwa kufanyika kwa udhamini wa Serikali ya Japan.
“Pia Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itagharimia ujenzi wa barabara za juu za Uhasibu na Chang’ombe chini ya awamu ya pili ya mradi wa mabasi yaendayo haraka,” anafafanua. Wakati akizindua daraja hilo rasmi, Rais John Magufuli, alibainisha wazi kuwa daraja hilo alilolipatia jina la Mwalimu Nyerere ni la kipekee ambalo watanzania wanapaswa wajivunie. Alisema historia ya ujenzi wa daraja hilo, ilianzia tangu miaka ya ukoloni 1933 na baadaye katika kipindi cha uongozi wa Mwalimu Nyerere mwaka 1971 lakini lilishindikana kutekelezwa kutokana na uhaba wa fedha.
Anasema kiukweli katika awamu zote juhudi zimekuwa zikifanyika kuhakikisha ndoto ya ujenzi wa daraja hilo inatimia lakini tatizo kubwa lilikuwa ni uhaba wa fedha. Anafafanua kuwa hatimaye katika kipindi cha uongozi wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa, Shirika la NSSF, liliwasilisha ombi la kutaka kujenga daraja hilo, ambalo lilitekelezwa rasmi katika kipindi cha uongozi wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete.
“Mimi nimekuwa Waziri katika nchi hii kwa kipindi cha miaka 20 na kati ya miaka hiyo 15 nimekuwa Waziri wa Ujenzi nawahakikishia nafahamu fika juhudi za viongozi katika ujenzi wa daraja hili,” alisema. Alisema kukamilika kwa daraja hilo, kunakaribia kutimiza ndoto ya kuufanya mji wa Kigamboni ambao sasa tayari ni jimbo la uchaguzi kuwa mji wa kisasa kama ilivyo katika mipango miji ya jiji la Dar es Salaam.
Anabainisha kuwa wakazi wa Kigamboni wana bahati kwa kuwa ndio watakaounganishwa na barabara ya Chalinze-Kigamboni itakayokuwa na barabara za juu takribani tano ambazo zitakuwa katika maeneo ya Tazara, Ubungo, Kurasini, Mlandizi na Chalinze. Aidha Dk Magufuli alisema lengo kuu la ujenzi wa daraja hilo ni kuondoa kero ya muda mrefu ya wakazi wa mji wa Kigamboni ambao wamekuwa wakitumia usafiri wa vivuko katika eneo la Magogoni ambavyo navyo vikiharibika, hulazimika kutumia mitumbwi.
“Nafahamu kuwa watu wengi wamepoteza maisha kutokana na ugumu na matumizi ya usafiri usio salama. Lakini sasa kupitia daraja hili ndoto yetu watanzania imetimia, kero hii imefika mwisho tulitumie kwa kujivunia na kulitunza,” alisisistiza. Alisema daraja hilo, ndilo litakalochukua nafasi ya kuwaunganisha wananchi wanaoishi eneo la Kigamboni na katikati ya jiji la Dar es Salaam, hali ambayo kwa namna moja itasaidia kupunguza tatizo la usafiri na kukuza uchumi kwa wananchi wa maeneo hayo.
Alisema baada ya kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo ni lazima sasa fedha zilizotumika katika ujenzi wake, zirejeshwe kwa njia ya kutozwa kwa wananchi wanaotumia daraja hilo lakini fedha hizo hazitotozwa kwa watu wenye ulemavu na watembea kwa miguu kwa sasa. Akafafanua kuwa watu watakaotozwa malipo ya matumizi ya daraja hilo ni wenye magari, pikipiki, guta, pikipiki ya matairi matatu (bajaj) na baiskeli.
Aidha alisema kutokana na ubora na uzuri wa daraja hilo, anatambua kuwa lazima wenye harusi zao watapenda kwenda kupiga picha hivyo aliagiza nao watozwe fedha ili kufidia malipo ya ujenzi wa daraja hilo. Dk Magufuli alitumia fursa hiyo kuwaomba wakazi wa Dar es Salaam na watanzania kwa ujumla kulitunza na kulithamini daraja hilo pamoja na mali nyingine za umma hususani miundombinu kwani wanapoiharibu hawaikomoi Serikali bali wanajikomoa wenyewe kupitia kodi zao.
“Kwa hili nitakuwa mkali, naomba vyombo vya ulinzi msimamie kikamilifu ikibidi mtu yeyote atakayegonga hata taa atozwe faini kubwa ili kujenga heshima ya mali za umma. Lakini pia naomba mzingatie suala la usafiri. Ni marufuku biashara kufanyika pembezoni mwa daraja hili,” alisisitiza Dk Magufuli. Baada ya uzinduzi wa daraja hilo imekuwa kawaida kwa sasa wakazi kutoka maeneo yote ya jiji hilo la Dar es Salaam pindi wanapopata muda kutembelea eneo hilo la daraja kwa ajili ya kujionea lilivyo lakini pia hata kupiga picha zikiwemo za harusi.