Daraja la Kigongo-Busisi rasmi sasa kujulikana kama Daraja la JPM

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Serikali imelibadilisha rasmi jina la Daraja la Kigongo –Busisi linalojengwa kuunganisha barabara kuu ya Usagara-Sengerema-Geita katika Ziwa Victoria ambapo kwa sasa daraja hilo litajulikana kwa jina la ‘Daraja la JPM kama sehemu ya kuenzi na kuthamini mchango wake kwenye sekta ya miundombinu nchini.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini(TANROAD) Mhandisi Patrick Mfugale amesema kuwa "Tumependekeza hilo jina tumeona linafaa tumeliweka na ikumbukwe kuwa daraja hili kwa sasa linajengwa na linafahamika internationally (kimataifa)," Endapo litaitwa Daraja la Kigongo - Busisi hakuna atakayelifahamu.

"Lakini ukisema hili ni daraja la JPM, wanajua JPM ni Rais wa nchi hii, JPM ndiye aliyetoa fedha za kujenga daraja hili karibu Sh bilioni 699.2 na linajengwa hapa kama alivyopendekeza mwenyewe, kwanini tusiliite jina lake?,"


Barabara ya Usagara- Sengerema-Geita ni sehemu ya barabara zilizoko kwenye ushoroba wa ziwa Victoria ambayo inaanzia Sirari mpakani na Kenya hadi Mutukula mpakani na Uganda (Km 774).

Daraja hilo lenye lenye urefu wa mita 3,200 na upana wa mita 28.45 litakapokamilika litakuwa ni daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki na la sita katika Bara la Afrika.

Busisi.jpg
 
Big mistake !

Ingekuwa mimi ni Magufuli ningekataa, hiyo ingempa heshima zaidi kwamba hapendi makuu, ...
 
“Yeye ndiye katoa ...”? Huyo Mfugale anachanganyikiwa sasa, pesa wametoa wanachi ansema “Yeye ndie katoa...”??!!
 
Back
Top Bottom