Daraja la Kigamboni au Reli ya kati? Kipi kina kipaumbele? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Daraja la Kigamboni au Reli ya kati? Kipi kina kipaumbele?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Hakeem makamba, Jan 20, 2012.

 1. Hakeem makamba

  Hakeem makamba Senior Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  SubalKheri wana jamii.

  Jamani mwenzenu ninatatizwa na hizi gharama kubwa ambazo serikali inaziingia kujenga daraja la Kigamboni kama zina ulazima wowote. Ni kweli kuwa muwekezaji ambaye ni NSSF amaechangia 60% ya hizo shilingi 100bn zitakazo tumika na serikali itatoa 40% iliyobakia.

  Swali langu ni kuwa hivi hizo pesa kwa nini zisingetumika kuimarisha reli ya kati ambayo inahudumia mamilioni ya watanzania kuliko kujenga daraja kwa mamia ya watu wa Kigamboni ambao tayari wana njia mbadala za kufika na kutoka makwao via panton au barabara?

  Kipaumbele ni kipi hapa jamani? hivi hili pia litahitaji elimu kung`amua?
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Jibu liko kwenye ballot boxes
   
 3. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,237
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  kaka hii serikari wewe jiulize kati ya reli ya kati na daraja la kigamboni kipi kitakuwa na tija kwa serikali i mean kipi kitaiingizia serikali mapato??

  kumbuka daraja la kigamboni pamoja na kuwahudumia wananchi wa kigamboni pia litakuwa ni eneo la kitalii, pia kumbuka tunaelekea kwenye mji wa kitalii wa kigamboni.
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  Hakuna nchi yoyote duniani ambayo imeendelea kama haikutilia mkazo haya yafuatayo:-

  Miundombinu mathubuti - Hasa Reli ambayo kwetu ingeunganisha mikoa ya Dar es salaam - Mwanza hadi Kigoma kupitia mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga. Hata wakoloni walivyotutawala walijua bila kuwa na usafiri wa uhakika kuunganisha mikoa hiyo mikuu basi uchumi hauwezi kupanda. Leo hii usafiri ni malori - jamani ukweli utabakia ukweli kwamba serikali yetu imeamua kufanya utani mkubwa kwenye hii secta muhimu.

  Viwanda: Hakuna nchi yoyote duniani yenye uchumi dhabiti ambayo imebeza viwanda, leo hii viwanda vilivyobakia tumewauzia hawa hawa tunaowaita wawekezaji -- Viwanda lazima vimilikiwe na wazawa kwa umoja wao, leo hii tumeuza kila kitu, tumebakia kukusanya vijisenti ambavyo vinaishia mikononi mwa wadokozi.

  Kilimo: Kuna nchi nyingi zimetumia kilimo kujikomboa na umaskini, sisi ardhi tunayo ya kumwaga, sera mbovu za udanganyifu mtupu, tumeamua kufanya utani kwenye mambo ya maana kama kilimo, inasikitisha kama tunaagiza hadi mchele na sukari kwakati ardhi ya kumwaga.

  Kubana na kudhibiti matumizi ya umma: Wakuu bila kuangalia unaingiza nini na unatumia nini basi tutatembeza bakuri mwanzo mwisho.

  Mwisho ndugu zangu, tutegemee mateso zaidi - Umeme juu, Sukari juu - Mtanzania mwenzangu huu ndiyo wakati wa kujuta. Kwa wale watanzania wenzangu ambao hada darasa moja hawakwenda na hawana mtaji wowote wa biashara basi waanze kuchimba makaburi yao wenyewe mapema - hapa mateso ni mwanzo mwisho. hali ni tete na inazidi kuwa tete.
   
 5. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Jibu zuri sana BIG up kaka nadhani mleta mada atakuwa amekuelewa na kufunguka macho naomba tufunge mjadala.
   
 6. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Umeuliza swali nyeti!
  Kuna mtu anayehusika na mchezo wa kuua kabisa mipango yote ya kufufuka kwa reli yakati!..Mtu huyo mwenye haulage company ana magari ya kusafirisha mizigo na mafuta kwa wingi, na ana pesa nyingi. Kitendo cha kufufua reli kwake itakuwa ni pigo, hivyo ameona atumie fedha kidogo kusababisha migogoro na kutoelewana kwa wafanyakazi na shirika hilo, huku akiendelea kujiongezea mapesa!
  Daraja la kigamboni halitamuathiri kitu!
   
 7. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tayari wakubwa wana malori yao ya mizigo na magari ya abiria, wakijenga reli, ulaji unaisha.
   
 8. F

  FUSO JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  kaka siasa tu, kigamboni kuna nini cha kumvutia mtalii? yaani bado tunaishi kwa ndoto? nani siku hizi akujengee mji ndugu yangu? Trilion 13 zinahitajika kama ukikuwa hujui ili kukamisha huo mji serikali yako inazo?
   
 9. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Miaka michache ijayo kuna watu watasimama Mahakamani kujibu kuhusu ubadhirifu wa mali za umma, natamani wakati huo ufike wakati Mkapa na Kikwete wakiwa hai ili wawe Mashahidi muhimu katika jinai hizo.
   
 10. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,230
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  labda jk analipiza kisasi kwa watu wa kgm na mwanza kuipiga chini ccm...ndio maana anwapiga danadana kwenye reli..
   
 11. k

  kamimbi Senior Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kusema ukweli ni kwamba reli ya kati ina msaada mkubwa zaidi kwa taifa ukipambanisha na daraja la kigamboni, lakini kwasababu kipimo cha maendeleo ya tz serikali huchukulia ni dsm ndo sababu hilo daraja likapewa kipaumbele, TIME WILL TELL. IM Sure every thing gonna b alright.
   
 12. F

  FUSO JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  kaka mwekezaji yoyote lazima kwanza a-corrupt system inayofanya kazi ili ile yake isonge wa urahisi zaidi. Kwa mfano waligawa NBC bank ili kuivunja nguvu zije benki za nje, Wakaiua Reli ili wafanye biashara ya kusafirisha mafuta kwa malori, Wakaua viwanda ili waagize bidhaa nje ya nchi n.k

  Tusipokuwa makini ukoloni mamboleo utatumaliza.
   
 13. s

  sawabho JF-Expert Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 948
  Trophy Points: 280
  Ujio wa Mji Mpya wa Kigamboni ni jibu sahihi.
   
 14. Kahise

  Kahise Senior Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 144
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Kimsingi reli ni bora zaidi kuliko daraja la Kgn.

  Kwa kuwa serikall yetu imebakia inafanya mambo ya aibu tupu, kwa maslahi ya walio madarakani, basi reli haina faida! Aibu iliyoje. Miradi ya wakubwa kama vilegeza mwendo, dawa za malaria n.k.

  Pamoja na yote, tuendelee kuumbea ukombozi wa nchi
  yetu, uwahi.
   
 15. P

  Peter Nyanje Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi vyote ni muhimu kwa maeneo yake, lakini kama unataka kipaumbele kati ya vitu hivyo, hakuna ubishi kuwa kuimarisha reli ya kati inazidi umuhimu wa kujenga daraja la Kigamboni. Lakini hiyo haimaanishi kuwa daraja la Kigamboni si muhimu.
  tatizo lipo miongoni mwa wanaofanya maamuzi. Tungeweza kuimarisha reli ili ituletee fedha za kutosha kuweza kujenga si tu daraja la Kigamboni, bali na madaraja mengine pia. Sidhani kama daraja la Kigamboni linaweza kuzalisha fedha za kutosha kuimarisha reli ya kati
   
 16. omujubi

  omujubi JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 4,144
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  pia yawezekana mtu huyu ndiye alihusika na kifo cha Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Reli Bwana (Hayati) Rwegasira!
  Mtu huyo ni nani sasa!???
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Mkuu PJ,

  Umeshindwa kuzingatia motto ya JF-"Where we dare to talk openly".
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu,

  Mimi kwa mawazo yangu reli ya kati ni muhimu na ni kipaumbele cha kwanza kuliko daraja la kigamboni.

  As of now kigamboni wanayo mapantoni ya kuwavusha kuingia na kutoka mjini, ama kuzunguka kwa barabara kupitia kongowe.

  Wasafiri wa treni ambao wengi ni watu wa kipato cha chini wako maeneo ya kanda ya kati, magharibi na kanda ya ziwa.

  Lakini pia mizigo inayosafirishwa toka dsm kwenda kanda ya kati, magharibi, ziwa na nje ya nchi kama rwanda, burundi, drc na uganda ingepita reli ya kati na hivyo kuiingizia serikali fedha nyingi sana.

  Daraja la kigamboni haliwezi kuingiza fedha unayoweza kuilinganisha na reli ya kati, wala halitahudumia wananchi wengi kama wanaohudumiwa na reli ya kati.
   
 19. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Kiongozi wako anapenda matanuzi aache kutengeneza kumbi za cinema kg?
   
 20. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #20
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  Zote ni huduma kwa jamii na zipo sawa kabisa pasi na moja kuwa juu ya nyengine bali inategemea vipaumbele vya Serikali katika kutoa huduma kwa jamii ya watu wake.

   
Loading...