Daraja la Ileje kubomoka: Uhandisi Tanzania umeshuka Viwango?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,555
19,426
Nimeangalia picha ya daraja lililojenga na kuanguka nikajiuliza, ni mhandisi gani aliyejenga daraja lile, je bado amesajiliwa na leseni yake ya uhandisi bado iko hai anafanya kazi kama kawaida?

Daraja hili limefeli kwa mchanganiko wa torsional deflection na bending deflection, na hayo ndiyo mambo ambayo structural engineer yeyote huangalia katika design. Sasa huyu design wa hilo daraja alikuwa na degree ya engineering kweli?

1616001579087.png

=====

Daraja lililojengwa Machi 14 labomoka

JUMANNE , 16TH MAR , 2021

Daraja linalounganisha Tarafa za Bulambya na Undali, lililopo wilaya ya Ileje mkoani Songwe, limezidi kuzua taharuki baada ya kujengwa na kudondoka kwa mara ya pili mfululizo hali iliyopelekea wananchi kukosa mawasiliano kwa Tarafa zote mbili.

Daraja hilo ambalo lilikarabatiwa na kukamilika jioni ya Machi 14, 2021, na ilipofika majira ya usiku daraja hilo likaanguka tena ambapo hadi sasa uongozi wa serikali umeendelea na taratibu za kujenga kivuko cha muda ambacho kitaondoa kero za wananchi wa tarafa hizo.

Wananchi wa Kata hizo wamedai kuwa daraja hilo ni mkombozi kwao hivyo tangu kuvunjika kwa daraja hilo imekuwa ni vigumu kwao katika nyanja ya kibiashara lakini pia wanafunzi wa shule za msingi wengi wamekwama kuendelea na masomo kutokana na daraja hilo kuvunjika.

Hali imezidi kuwa tete kwa upande wa usafiri kwani kutokana na daraja hilo kuanguka, sasa kumejitokeza biashara ya vijana kuvusha watu na pikipiki kwa kiasi cha shilingi 2,000 hali ambayo haikuzoeleka na wananchi.

Pamoja na jitihada za kujenga kivuko cha muda, wananchi wamedai kuwa kama kutakuwa na mvua katika kipindi hiki huenda kivuko hicho kikaondolewa na maji kwani si cha uhakika na kuiomba serikali kuwatengenezea daraja la uhakika ili mawasiliano katika Tarafa hizo mbili yaweze kurejea
20210317_214803.jpg
20210317_214818.jpg
 
Nimeangalia picha ya daraja lililojenga na kuanguka nikajiuliza, ni mhandisi gani aliyejenga daraja lile, je bado amesajiliwa na leseni yake ya uhandisi bado iko hai anafanya kazi kama kawaida?

Daraja hili limefeli kwa mchanganiko wa torsional deflection na bending deflection, na hayo ndiyo mambo ambayo structural engineer yeyote huangalia katika design. Sasa huyu design wa hilo daraja alikuwa na degree ya engineering kweli?

Mkuu usilaramie fani unazozisoma kwenye magazeti.
kwanza kabisa hilo ni Bailey Bridge, one of strongest bridges that can carry heavy loads.
Pili jiridhishe na abbutments za huo mto zinazoonekana kufeli kutokana na erosion.
Mode of failure inaonekana wazi kuwa ni settlement ya abbutment.
 
Utetezi wako ni kuwa injinia huyo hakujali uwekaji foundation, bali yeye alikimbilia kuweka beam tu; nimekuelewa? Hiyo ni engineering gani sasa!
 
Scouring,hata kama hizo member trusses zingekuwa imara na msingi sio imara lingeli pata madhala.
Tatizo hapo ni wingi wa maji,bajeti kuwa ndogo kujenga daraja kubwa,uharibifu wa mazingira kwenye vyanzo vya Maji na uchakavu wa daraja /matengenezo kulingana na umri wa muundombinu husika.
Kwenye majenzi ya daraja kikubwa ni kuzingatia yafuatayo:-
1.Taarifa ya mvua/vyanzo bus maji na wingi wake/hydrological .
2.Tabia ya udongo liwekwapo daraja.
3.Madhumunu gani!/linajengwa kwa ajili ya kupitisha vitu gani /uzito /kwa wingi gani wa kupita /Traffic.
4.Ni ujazo gani wa Maji unaotakiwa kupita na kwa kasi ipi katika eneo lote /Surveyed /Topography nature.
5.Nini athali za mazingira kwenye Mardi husika /EIA.
6.Ni daraja gani linafaa kujengwa kutokana na 1,2,3,4, na 5
Note.
Ujenzi wa daraja sio jukumu la Structural Engineer pekee, bali ni TEAM WORK ya wadau walioko hapo juu ingawa kwa kilichofanyika /kuonekana yawezekana kikamlenga moja kwa moja mhusika na yeye asiweze kusema chochote.
 
Na wewe unaamini kuwa kuwa injinia huyo hakujali uwekaji foundation, bali yeye alikimbilia kuweka beam tu; nimekuelewa? Hiyo ni engineering gani sasa!
 
Utetezi wako ni kuwa injinia huyo hakujali uwekaji foundation, bali yeye alikimbilia kuweka beam tu; nimekuelewa? Hiyo ni engineering gani sasa!
Hayo madaraja huwa ni ya serikali.

Waulize wazee wa Fosi Akaunti!!
Huwa wanajenga kwa mtindo wa value for money!
 
Elimu yetu imeshuka sana zimebakia PhD za majungu na kubuni sheria za kumdhibiti kidogo wa tweter
 
Na wewe unaamini kuwa kuwa injinia huyo hakujali uwekaji foundation, bali yeye alikimbilia kuweka beam tu; nimekuelewa? Hiyo ni engineering gani sasa!
Majibu na ufafanuzi rejea kwenye mchango niliutoa.
Kabla ya kupost ungefanya analysis kidogo ya umri wa daraja na kujilidhisha walau na mazingira lilipo hilo daraja na ni kwanini iwe leo na sio jana kubomoka!!!!
 
Hayo madaraja huwa ni ya serikali.

Waulize wazee wa Fosi Akaunti!!
Huwa wanajenga kwa mtindo wa value for money!
Mimi nazungumza from engineering point of view siyo mteja. Mojawapo ya sifa za injinia ni kumwambia mteja wazi kuwa ili mradi ufanikiwa lazima msingi uchimbwe kiasi kadhaa kuwe na zege na ndondo kiasi kadhaa, pamoj na hizo u-channels kiasi kadhaa. Kukubali malipo ambayo hayatoshelezi mahitaji ya mradi siyo professionalism
 
Majibu na ufafanuzi rejea kwenye mchango niliutoa.
Kabla ya kupost ungefanya analysis kidogo ya umri wa daraja na kujilidhisha walau na mazingira lilipo hilo daraja na ni kwanini iwe leo na sio jana kubomoka!!!!
Kuna mtu kaongezea kwenye post yangu ya awali, nadhani ni modereta. Daraja ninalozungumzia siyo lile la zamani bali lile lililojengwa baada ya lie la zamani kusombwa. Sasa hilo lililojengwa nalo likadidimia ndani ya siku tatu tu, na hapo ndipo ninapouliza uhandisi gani ulitumika pale!
 
Tz bado hatuna uwezo. Kuna kampuni Moja ya Ujenzi ya MEKO na Wahindi.....NYANZA ROADS CONSTRUCTION. Ina jenga barabara zote Kanda ya Ziwa na Kgm kwa jina la Mkubwa. Barabara zake ni mbovu na kichefuchefu tupu
 
Nimeangalia picha ya daraja lililojenga na kuanguka nikajiuliza, ni mhandisi gani aliyejenga daraja lile, je bado amesajiliwa na leseni yake ya uhandisi bado iko hai anafanya kazi kama kawaida?

Daraja hili limefeli kwa mchanganiko wa torsional deflection na bending deflection, na hayo ndiyo mambo ambayo structural engineer yeyote huangalia katika design. Sasa huyu design wa hilo daraja alikuwa na degree ya engineering kweli?

=====

Daraja lililojengwa Machi 14 labomoka

JUMANNE , 16TH MAR , 2021

Daraja linalounganisha Tarafa za Bulambya na Undali, lililopo wilaya ya Ileje mkoani Songwe, limezidi kuzua taharuki baada ya kujengwa na kudondoka kwa mara ya pili mfululizo hali iliyopelekea wananchi kukosa mawasiliano kwa Tarafa zote mbili.

Daraja hilo ambalo lilikarabatiwa na kukamilika jioni ya Machi 14, 2021, na ilipofika majira ya usiku daraja hilo likaanguka tena ambapo hadi sasa uongozi wa serikali umeendelea na taratibu za kujenga kivuko cha muda ambacho kitaondoa kero za wananchi wa tarafa hizo.

Wananchi wa Kata hizo wamedai kuwa daraja hilo ni mkombozi kwao hivyo tangu kuvunjika kwa daraja hilo imekuwa ni vigumu kwao katika nyanja ya kibiashara lakini pia wanafunzi wa shule za msingi wengi wamekwama kuendelea na masomo kutokana na daraja hilo kuvunjika.

Hali imezidi kuwa tete kwa upande wa usafiri kwani kutokana na daraja hilo kuanguka, sasa kumejitokeza biashara ya vijana kuvusha watu na pikipiki kwa kiasi cha shilingi 2,000 hali ambayo haikuzoeleka na wananchi.

Pamoja na jitihada za kujenga kivuko cha muda, wananchi wamedai kuwa kama kutakuwa na mvua katika kipindi hiki huenda kivuko hicho kikaondolewa na maji kwani si cha uhakika na kuiomba serikali kuwatengenezea daraja la uhakika ili mawasiliano katika Tarafa hizo mbili yaweze kurejeaView attachment 1728290View attachment 1728291
Unafaamu daraja lilijengwa na watu gani? Usiwe unaongea vitu usivyo na uhakika navyo.
 
Mkuu usilaramie fani unazozisoma kwenye magazeti.
kwanza kabisa hilo ni Bailey Bridge, one of strongest bridges that can carry heavy loads.
Pili jiridhishe na abbutments za huo mto zinazoonekana kufeli kutokana na erosion.
Mode of failure inaonekana wazi kuwa ni settlement ya abbutment.
Usiwe mmoja wa wanaomaini kuwa wengine hawajui mambo unayoweza kuwa unajua wewe. Mara zote jadili na watu ukiwa na open mind kuwa inawezekana wao wanajua zaidi yako. Siwezi kuweka technical post kama hii bila kujua technical details zilizomo ndani yake. sasa kama unaamani kuwa nimelaramia ya magazetini, basi stick kwene technical details tu unipe sababu ya kuuhalalisha failure hiyo bila kumgusa engineer aliyejenga daraja hilo. Kujenga ninaunganisha designer, consultant, na construction engineer mwenyewe wote kwa pamoja.
 
Mimi Naona kama kuna kazi/ tenda ya ujenzi imetokea then muwaajiri engineers BOTH wa nje na ndani-Tanzania, I’m sure vichwa vikiwa tofauti then matokeo yatakua positive. Huyu wa nje ana exposure wa mambo mbali na huyu wa Tanzania ana local knowledge, challenges zetu anazijua, vikiwa combined Haya madaraja yanayovunjika itakua history...,,

Kingine ni Mkuu Rais kutenga fungu kubwa la vitu Kama madaraja, Sio engineer anapewa limited funds then mna expect he do wonders!
 
Back
Top Bottom