Daraja la Buguruni

fdizzle

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
1,900
2,394
1460981968296.jpg


Napenda kutoa pongez zang za dhati kabisa kwa serikali kwa kutambua umuhim wa ujenz wa daraja ambalo litatumika kama kivuko kwa waendao kwa miguu.

Ikumbukwe pia ujenzi wa daraja hili utasaidia kwa asilimia kubwa kutokea kwa ajali pale maeneo ya buguruni sheli. Kimsing darajahili limejengwa kwa kutambua mahitaji ya watu mbalimbal haswa walemavu wa miguu wanaotembea kwa baiskel kwani kuna sehem yao maalum ya kupandia hilo daraja.

Wasiwasi wangu upo kwa hawa madereva wanaojua aheria kuliko madereva wote duniani nikimaanisha bodaboda. Hawa jamaa si ajab ukawakuta wanapanda hilo daraja na bodaboda zao kwenda upande wa pili wa barabara kwa kutumia hiyo njia iliyotebgwa kwa ajili ya walemavu.

Hii italeta usumbuf mkubwa kwa watumiaji wa hilo daraja. Nishauri tu wanaohusika na ujenzi watafute namna ili kuzuia hawa watiifu wa sheria bila shurut maaruf kama bodaboda.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom