Story of Change Daraja kati ya Shule, Elimu na Maisha

Ntiyakama

Member
Sep 19, 2021
22
45
Miaka 0-5; umri huu watoto wengi katika jamii zetu huwa bado wapo nyumbani wakijifunza kuongea, kunawa, kula, kutambaa, kutembea, kukimbia, kurukaruka, kucheza na mambo mengine mengi wanayoyahitaji kwa ajili ya kuishi vyema na kwa furaha.

Muda huu ni mzuri na wenye kufaa zaidi, kwa sababu mtoto anaweza kupata maarifa yenye msaada zaidi katika maisha yake kutoka kwa wazazi, jamii inayomzunguka na katika mazingira kwa ujumla wake.

Inasikitisha, watoto wengi siku hizi hawapati nafasi ya kukua wakiwa katika mikono ya wazazi wao. Wengi hupelekwa shuleni mapema zaidi, wengine wakiwa hawajaweza hata kuongea vizuri!

Mbaya zaidi hawapewi tena muda wa kupumzika watokapo shuleni ili wakae na wazazi wao, kwa sababu jioni wanahitajika tena kwenye masomo ya ziada (tuition).

Mh! Katika umri mdogo kiasi cha chini ya miaka 5 na hata kipindi chote cha shule ya msingi, watoto hawa wanajifunza vitu gani kiasi cha kutokupata muda wa kupumzika, kukaa na wazazi wao, kucheza na wenzao pia kufanya mambo mengine zaidi ya kuwepo shule. Tujitafakari:

Usimkimbize mtoto shuleni mapema akiwa bado haelewi wala hawezi kujisaidia kwa lolote. Mlee kwanza apate ufahamu wa kujitunza, kujisimamia, kutambua na kujiepusha na hatari anapoona dalili zake.

Mjengee msingi mwema utakaompa uthabiti mara atakapoambatana na watu wengine. Mjengee uwezo wa kuamua vyema na kuyajali maamuzi yake kwanza.

Inasikitisha kuwa baadhi ya wazazi siku hizi huwapeleka watoto wao shuleni mapema, kwa sababu ni wasumbufu; waondoe kero nyumbani au kwa sababu hawana wa kubaki nao nyumbani.

Wengine wanawapeleka shule za bweni mbali na nyumbani wasipoweza hata kurudi kwa urahisi nyumbani kwa sababu wameshindikana kuwalea nyumbani!

Mtoto aliyekushinda kumlea wewe akiwa mmoja, kisha unampeleka akalelewe na mwalimu ambaye tayari anao 10 wengine wa namna hiyo (anaopaswa kuwalea wote); unategemea atamrekebisha kiasi cha kuwa mtu wa thamani na maadili baadaye.

Au wewe ndiye, utakaye kuja kuwalalamikia, walimu kwamba wameshindwa kukulelea mtoto. Tujitafakari.

Miaka 5-6 madarasa huanza, Darasa la awali (chekechea), 7-13 shule ya msingi (darasa la kwanza mpaka la saba), 14-18 sekondari (kidato cha kwanza mpaka channe), 19-20 kidato cha tano na sita. 21-25 vyuo na vyuo vikuu.

Wastani, umri wa kuishi kwa mtanzania ni miaka 63.9 (mwanamume 62.0 na mwanamke 65.8: WHO, 2018), tunatumia karibu nusu ya umri tunaopaswa kuishi duniani, tukiwa shuleni huku wengi wetu kama siyo wote, tukijifunza namna ya kutumikia na si kutumika.

Kwa sababu tunaambiwa elimu ni ufunguo wa maisha, tunapo tunukiwa vyeti kila tumalizapo ngazi moja, tunadhani kwamba vyeti hivyo ndizo funguo za kufungulia makufuli ya maisha yetu! Pasipo kujua kuwa vyeti hivyo ni kibeba ufunguo tu (KEY HOLDER).

Ufunguo wenyewe ni maarifa tuliyoyapata na utashi wa kuyatumia vyema maarifa hayo.

“Usihangaike kutembea mtaani na vyeti (key holder) mkononi mwako ukitafuta kufuli (kazi) la maisha yako! Beba maarifa kichwani mwako na ufahamu akilini mwako (funguo) kisha itazame dunia katika mapana yake”

Si A, B+ au B pekee unazopata ndizo zitakazo kufanya uishi vizuri kama yalivyo matarajio ya wengi. Kuishi vizuri ni zaidi ya hapo, unahitaji mambo mengine mengi ya msingi na muhimu zaidi ya kuwa na GPA (kiwango cha ufaulu) nzuri pekee.

Shule zipo si kwa ajili ya kutufanya tuishi, bali kuchochea ndani mwetu, kupatikana na kukua kwa maarifa tunayohitaji kuishi. TUNAHITAJI MAARIFA NA KUELIMIKA ILI KUISHI; KUISHI VYEMA.

Elimu ni zaidi ya kwenda shule pekee, elimu ni zaidi ya GPA nzuri (kubwa), elimu ni zaidi ya kukaa darasani, kuandika, kusoma, kujibu mitihani na kufaulu, kisha kuhama madarasa kila mwaka unapobadilika. Elimu ni zaidi ya kuwepo shuleni.

Elimu: hujumuisha maarifa, ujuzi (humwezesha mtu kujitambua na kujiweka sawa katika kupambana na mabadiliko ya mazingira pia changamoto za mara kwa mara za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kiimani) na maadili ambayo hupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

MATOKEO YA MFUMO WA SHULE KWA ELIMU

Yako mazuri mengi tuyapatayo kutokana na elimu katika utaratibu wa shule pekee, kwani tunapata wataalamu katika mambo mbalimbali kama, walimu, wauguzi, madaktari, wahandisi, marubani, n.k.

Pia kutokana elimu hiyo wengine wachache kati ya wengi wanaosoma wanaweza kujipambanua kutoka katika msingi wa maarifa hayo na kuitazama jamii na dunia katika upana wake, kisha kuona fursa na kuzitumia kufanya mambo mengine yaletayo maendeleo kwao na katika jamii zao.

Wengine hujiwekea ukomo wa kufikiri katika mishahara na mafao yao ya uzeeni wanayoyatarajia baada ya kustaafu!

Mtazamo wangu unawagawanya wanafunzi wanaojifunza na kuelewa katika makundi mawili; wanaoelewa ili wafaulu mitihani na wanaoelewa ili elimu iwasaidie maishani.

WANAOELEWA ILI WAFAULU MITIHANI

Kundi hili ndilo kubwa zaidi na ndilo linaloathiriwa zaidi na mfumo wa utoaji elimu kwa njia ya kuwepo darasani, kufundishwa na kujibu mitihani.

Lengo lao kubwa zaidi watu hawa ni kuhakikisha wanafaulu vizuri masomo yao na kusonga mbele zaidi.

Zaidi huathiriwa na fikra kwamba kufalu vizuri ndiyo njia pekee ya kufanya maisha yao kuwa mazuri zaidi; hujibidisha kusoma na wakati mwingine kukariri sana ili kuhakikisha wanafaulu vyema mitihani.

Hawa ndio wale ambao wakipewa swali; (Mfano. Tafuta thamani ya x; 2x + 3 = 7 – 3x) watafanya swali hilo vizuri kabisa na wakati mwingine huamua kujiongezea mbinu nyingine nyingi zaidi za kujibu maswali ya namna hiyo.

Faida za wanafunzi waliopo katika kundi hili, ni kuwa na uwezo mzuri wa kukumbuka waliyojifunza na kujisomea hivyo mara nyingi hufanya vyema katika mitihani yao. Husonga mbele zaidi na kufanikiwa kitaaluma.

CHANGAMOTO; hawa hubakiza mawazo yao katika kusoma, kukariri na kujibu mitihani peke.

Wao huamini kuwa wanachokisoma darasani hakina uhusiano na maisha yao halisi (thamani ya X kwao haina chochote cha kufanya katika maisha yao!), isipokuwa wanahitaji kusoma zaidi ili wafaulu vizuri, wapate kazi nzuri maisha yawe mazuri kwao na familia zao. Wengi huishia kuajiriwa na kuwa watumishi.

WANAOELEWA ILI ELIMU IWASAIDIE MAISHANI

Naliona kama kundi dogo la wanafunzi wanaojifunza katika namna hii; hawa hulinganisha kila wanacho jifunza darasani na uhalisia wa maisha yalivyo katika mazingira yao.

Mwanafunzi wa namna hii akipewa swali (Mfano. Tafuta thamani ya x; 2x + 3 = 7 – 3x) hataishia tu kusema, x = 2, bali ataitafakari njia aliyoitumia kuitafuta thamani hiyo ya kitu kisichojulikana (x) kama njia inayoweza kumjengea uwezo kifikra wa kutafuta vitu vingi ambavyo anavihitaji katika maisha yake.

Fursa, mahusiano mazuri, makazi mazuri, pesa, n.k, vyote ni thamani ya X (havipo wazi kuonekana kwa kila mtu), mwanafunzi wa kundi hili tayari anajenga msingi na uwezo wa kifikra kutafuta kilichojificha kutoka katika kuitafuta thamani ya X iliyokuwa ikifichwa katika namba na herufi nyingine wakati akisoma darasani.

Kwangu mimi hili ni kundi bora, na ndilo hutengeneza watu wanaofanikiwa zaidi katika maisha yao.

Hii ni faida msingi ya kundi hili, ingawa wengi wao huwa hawajiendelezi zaidi kitaaluma, huona kama elimu kiasi waliyonayo inawatosha kusimamia mambo yao.

Ni kundi hili ambao wengi wao hujiajiri katika shughuli zao wenyewe, huwaajili wengine na wengine hufika mbali zaidi na kuwa wawekezaji.

Si wote wanaosomea taaluma fulani basi huajiliwa kufanya kazi katika taaluma hiyo, wengine hukosa ajira kwa sababu ya uchache wake na wingi wa wahitaji, pengine wangalikuwa na maarifa kidogo ya kutumia ufahamu wao (kuitafuta thamani ya X) na si kutegemea taaluma pekee wangeweza kufanya jambo, lakini kwa kukosa ufahamu huo hubaki wakilandalanda na kulalamika kila iitwapo leo; watu wa namna hii huathiriwa zaidi na matokeo yafuatayo;

1. KUKOSA KUJIAMINI

Anayefaulu masomo darasani, ndiye anayeonekana ni mwenye akili na muelewa na ndiye hupewa nafasi kila mara, wengine wenye mawazo na uwezo binafsi mzuri zaidi nje ya masomo, hawapewi nafasi na pengine mawazo yao na kile wanachoweza kukifanya hupuuzwa.

Hali hii huwafanya kujihisi kuwa wao ni duni mno na hawawezi kufanya makubwa kisha hukosa kujiamini.

2. KUWA TEGEMEZI

Hatuwezi mpaka tuwezeshwe, hatusomi mpaka tufundishwe, hata kucheza tu lazima awepo mwalimu au kiongozi wa kutusimamia!

Hakuna chochote tunachoweza kufanya pasipo mwalimu. Haya ni mazingira ambayo wengi hujengwa kwayo wawapo shuleni.

Jambo hili huwafanya wengine kuendelea na hali hiyo ya utegemezi hata watakapo ondoka shuleni.

3. KUKOSA UTHUBUTU

Viboko na adhabu nyinginezo, huongeza hofu zaidi ya kuogopa kukosea, pengine mwalimu anadiriki kusema azomewe aliyekosea!

Hali hii huongeza wasiwasi na kufanya wanafunzi wasijaribu kabisa kwa hofu ya kukosea wasije wakaadhibiwa.

Hofu hii hukua na kuendelea ndani mwao na kupelekea kukosa kwao uthubutu wa kufanya mambo mengine nje ya taaluma zao.

4. UBINAFSI

Shule zinawaandaa wanafunzi kuwa waajiriwa pekee tena wengi wao wakitazamia mishahara mikubwa pasipo kujali inatoka wapi na nani ameitengeneza.

Wengi baada ya shule hufikiria wapate kazi nzuri walipwe mishahara mizuri na waishi vizuri. Kwa sababu hiyo basi hawawezi kufikiria juu ya namna wanavyoweza kutengeneza kazi nzuri na kuwalipa mishahara mizuri wengine. Ubinafsi huo huwafunga kuwa wajasiriamali.

Shule ni nzuri kwa sababu inatupatia ramani na inatuelekeza barabara ya kufuata katika maisha yetu, ingawa hata mara moja shule haielezi uwepo wa alama za barabarani, ubovu wa bararaba na changamoto zingine nyingi tunazoweza kukutana nazo katika barabara hiyo, na namna gani tunaweza kuzikabili.

Jiandae kuishi, safari katika barabara hii siyo nyepesi.
 
Upvote 0

Big Simba

Member
Sep 7, 2019
15

Thanks ...!
Mchanganuo mzuri , then we have to decide what should be done. Tuondoke apo tulipo .
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom