Dar yote Umeme umekatika

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Hii sijui ni dharula, bahati mbaya ama nini, ila hakuna taarifa yoyote, ila mji mkuu wa Kibiashara na shughuli za Kiserikali Dar es salaam hauna nishati ya umeme tangu saa 12.30 asubuhi, nimewasiliana na wakazi wa Kawe, Mbezi Beach, Mbezi Kimara,Ubungo, Temeke,Mbagala, Buguruni ,Ukonga, Vingunguti, Lumo,Kwa Gude, Manzese na hata Kigamboni kote wamenithibitishia hakua stima.
Nimekua nafatilia matangazo ya TV , Radio mpaka saa hizi hakuna mjuzo wowote kwa umma juu ya kinachoendelea.
Kweli huu ni uungwana ? kwanini hata kama kuna dharula wasiujuzem Umma kuwa kuna itilafu ?
 
hata huku Tanga umeme umekatika mpaka muda huu ,nadhani ni tatizo TZ yote
 
kama kuna tatizo la ghafla, mtandao wa mawasiliano ni mkubwa kwanini wasitoe taarifa, na umma ukaelewa, maana watu wanaenda makazini wanaishia kupiga soga, sasa kama TANESCO wangetuelewesha mapema, mtu unatulia home, unaokoa hasara yakwenda kazini bila kufanya kazi.
 
Naona Grid ya Taifa ili trip nchi nzima, kwani hadi huko mikoani umeme ulikuwa umekatikla. Hata hivyo umeme umeanza kurejeshwa baadhi ya maeneo. TANESCO wanapaswa wawe makini, au mpaka mteja mmoja wafungulie kesi ya madai ndipo waelewe!!!!!
 
Tulioko mikoa ya Kusini raha mustarehe, poleni nyie wadau
 
Hata Mbeya umekatika.
Lakini kwa Dar mpaka sasa ni 45min toka urudi.
 
Huku Mtwara tushasahau mambo ya huooo... tunabonyeza tu switch za ATUMAS.. ila jamaa mabingwa wa kusoma meter hata uweke ****** wataiona tu
 
Someni mwananchi pg 12 maeneo yameainishwa ndo maana kinondoni haujakatika.
Maeneo mengi umeme utarudi saa 11 mpaka 12 jioni
Thax
 
Wabongo bana, is this a breaking nuwz? How many times this event occurs in a yr?
 
Musoma ulikatika kuanzia alfajiri hadi mida hii... uzuri huku hakuna majasho
 
Wabongo bana, is this a breaking nuwz? How many times this event occurs in a yr?
kukatika umeme ni jambo ambalo halistuii sana hapa nyumbani, ila kwakawaida wanakata umeme kunapokua na matukio makubwa kama mechi kubwa za mpira, ama kunatukio mnalingojea kwa hamu kwenye vyombo vya habari, umeme Tanzania ni anasa tu, nasikia mtu yoyote pale TANESCO hata mfagiaji anakata tu umeme...
tukio la leo kukatika umeme sehemu kubwa ya nnchi ni tishio kiusalama, kiuchumi na ni usumbufu.kwetu, kama kuna dharula ni vyema ikatangazwa, na watu wakajipanga.
Juma hili linaloisha kumeripotiwa vifo pale hospitali ya Temeke vilivyotokea katika vyumba vya upasuaji baada ya TANESCO kukata umeme kwa makusudi (maana hakuna taarifa hadi leo kwanini walikata) na jenereta za dharula kushindwa kumudu kuhudumia Hospitali nzima....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom