Dar yaongoza sampuli za kifua kikuu, UKIMWI

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,319
33,125
Muhimbili%289%29.jpg

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Mkoa wa Dar es Salaam, unaongoza kuwa na sampuli nyingi za ugonjwa wa kifua kikuu na za Ukimwi kutokana na kuwa na mwingiliano wa watu wanaotoka mikoa mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Maabara ya kituo cha Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu kilichopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dk. Prosper Ngowi, kati ya sampuli 80,000 za ugonjwa wa kifua kikuu na ukimwi ambazo zimepokelewa kwa mwaka huu kituoni hapo 5,000 zinatoka mkoa wa Dar es Salaam.

Dk. Ngowi aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa maadhimisho ya NIMRI ya miaka 30 kutoka kuanzishwa kwake.

Alisema sampuli nyingine zilizobaki zinatoka katika hospitali nyingine zilizopo mikoani hapa nchini ambazo hupokelewa hapo kwa ajili ya utafiti.
Aidha, Dk. Ngowi alisema mwaka 1980 wagonjwa wa kifua kikuu walikuwa karibu 11,000 lakini kwa sasa idadi yake ni zaidi ya 60,000.

Mkurugenzi Msaidizi wa Tiba na Afya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Peter Mmbuji, alisema utafiti ambao unaendelea kufanywa na kitendo hicho utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la ugonjwa huo.

Dk. Mmbuji ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo, alisema kuwa mikakati ya serikali ni nchi iweze kuwa na uwezo mkubwa wa kiutafiti wa ugonjwa huo ili kuweza kuuthibiti usiendelee kuua.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa NIMRI, Mwele Malecela, alisema tafiti ambazo zinaendelea kufanywa na taasisi yake, zimesaidia kwa kiwango kikubwa ubadilishaji wa sera na kusaidia kuwa na wataalumu zaidi ya 20 wa masuala hayo.

Mkurugenzi wa NIMRI kutoka kituo cha Muhimbili, Dk. Sayoki Mfinanga, alisema hadi sasa asilimia 80 ya wagonjwa wa kifua kikuu wameingia kwenye mpango huo wa utafiti.

Mtaalamu wa maabara kutoka kituo hicho, Grayson Malewo, alisema maabara yake kwa siku hupokea sampuni 20 kwa ajili ya utafiti.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom