Dar yang’ara darasa la saba

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Dar yang’ara darasa la saba
Maulid Ahmed
Daily News; Monday,December 22, 2008 @21:15

Mkoa wa Shinyanga umeshika nafasi ya mwisho katika mtihani wa darasa la saba huku Mkoa wa Dar es Salaam ukiongoza kwa kufanya vizuri. Katika matokeo hayo, asilimia 80.73 ya wanafunzi 433,260 waliofaulu darasa la saba wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza katika shule za serikali, wakiwamo wasichana 188,460 sawa na asilimia 82.13 na wavulana 244,800 sawa na asilimia 79.69 waliofaulu.

Hata hivyo, ufaulu wa masomo ya Hisabati na Kiingereza uko chini. Akitangaza matokeo hayo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe alisema kati ya wanafunzi wote 1,017,967 sawa na asilimia 97.51 ya walioandikishwa, walifanya mtihani huo na wanafunzi 536,672 sawa na asilimia 52.73 wamefaulu.

Katika matokeo hayo ambayo yataanza kutangazwa na kila mkoa leo, wavulana walifanya vizuri zaidi ambapo walikuwa 307,196 sawa na asilimia 59.75 huku wasichana waliofaulu ni 229,476 sawa na asilimia 45.55. Aliitaja mikoa iliyofanya vibaya na kiwango cha ufaulu kwa asilimia kwenye mabano ni Shinyanga (34), Lind i(40.7), Mara (42.6) na Tabora (43.2). Kwa mikoa iliyofanya vizuri ni Dar es Salaam (73.9), Arusha (69.2), Iringa (64.1) na Kagera 63.5.

Kwa upande wa wanafunzi waliobainika kufanya udanganyifu, alisema “watahiniwa 102 wamefutiwa mitihani wakiwamo wasichana 41 na wavulana 61.” Akifafanua juu ya ufaulu wa masomo ya Hisabati na Kiingereza ambayo kwa miaka miwili mfululizo umekuwa wa chini, Profesa Maghembe alisema Hisabati ni asilimia 18.07 huku Kiingereza ni asilimia 31.5.

“Matokeo ya Kiingereza ni sawa na mwaka jana na Hisabati mwaka jana ni asilimia 18.72, tumeweka mikakati ya kuboresha masomo hayo ikiwamo vyuo vyote vya ualimu kutoa nyenzo kwa wanafunzi wa ualimu kuweza kufundisha masomo hayo, kuwapa mafunzo walimu waliopo na tunatoa wito kwa wanafunzi wasiyaogope masomo haya,” alifafanua Waziri huyo.

Ufaulu wa masomo mengine na kiwango katika asilimia ni Kiswahili (73.4), Sayansi (68.24) na Maarifa (61.03). Waziri Maghembe alisema kati ya wanafunzi 346 wenye ulemavu waliofanya mtihani huo, wanafunzi 221 sawa na asilimia 64 ya watahiniwa wamefaulu na wote wamechaguliwa kuingia kidato cha kwanza.

Wanafunzi wa darasa la saba walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi Septemba 10 na 11 ambapo wanafunzi 1,017,967 kati ya wanafunzi 1,043,969 walioandikishwa walifanya mtihani huo wakiwamo wasichana 515,179 na wavulana 528,790.

Wakati huohuo, Waziri Maghembe amesema katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, Idara ya Sekondari itahamishwa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi). Alisema mchakato unaendelea na tayari maofisa Elimu wa Wilaya wameshateuliwa na majalada yote ya sekondari yameshapelekwa Tamisemi.
 
Je, kuna mkakati wa kuwa'tap hao wanafunzi waliofeli 65% wa Shinyanga kwenye any productive sector? Or are they doomed to never acquire any supported productive skills.
 
Nionavyo mimi miaka zaidi ya 45 baada ya uhuru na bado tunashindwa kuwapatia vijana wetu wote elime ya sekondari ni uzembe wa hali ya juu sana! La ajabu ni kuwa badala ya kujaribu kubalisha huo utaratibu ili tuweze kuwapatia vijana wetu wote elimu inayolingana na dunia ya sasa, viongozi wetu wote bado wanang'ang'ania hayo maneno ya kufaulu na kufeli darasa la saba. Je, kama mwana JF mwenzetu alivyochangia hapo juu hao wanaoishia darasa la saba waende wapi?, ama bado ile tabia ya kusema inabidi waende kijijini kulima bado twaiendeleza? jembe bila hata elimu ya awali kuna kitakacho vunwa kweli?
 
Choveki,
Mkuu bado kuna hili moja kubwa zaidi kuliko yote.. Tanzania kufaulu mtihani haina maana umechaguliwa kwenda moja kwa moja shule ya sekondari...
Nimesoma mahala kwamba huko Mbeya kuna wanafunzi (walioshinda) watakosa kuingia shule ya sekondari kutokana na uchache wa madarasa na mchezo huu umekuwepo toka tumepata Uhuru..Kwa hiyo hapo asilimia 52 itapungua na kushuka chini zaidi.
 
Tunacheza makida... kuna maana gani mtoto anafaulu halafu anakosa nafasi ya kuendelea sekondari. Inashangaza sana kwamba kati ya sekta ambazo serikali inaniipiga upatu kuwa imefanye vizuri ni elimu!!!!
 
[B said:
Hivi ni uungwana kutupa matokeo/taharifa ya/za miaka ya nyuma wakati sasa hivi tunasubili ya mwaka huu?[/B]
Umesoma imepostiwa lini au unalalmika tuu?
 
Back
Top Bottom