Dar: Watu wawili kizimbani kwa meno ya tembo yenye Kg 3500 na thamani ya sh bilioni 4.2

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
WATU wawili wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kwa kosa la kusafirisha meno ya tembo kiasi cha kilogram 3500 yenye thamani ya zaidi ya Sh 4.2 bilion.

Watuhumiwa hao ni Kassim Said kwa jina maarufu Bedui (50) Mkazi wa Arusha na Joachim Minde (Kennedy Kimaro) (55) Mkazi wa Kinondoni, Dar es Salaam.

Akisoma mashtaka hayo leo Salim Msemo, Wakili wa Serikali mbele ya Amilius Mchauru, Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo amedai kuwa, watu hao wanakabiliwa na mashtaka mawili.

Msemo amedei kuwa, watuhumiwa hao walijihusisha na genge la wahalifu na kudaiwa, kati ya Machi 2013 na Agosti 2015 walijihusisha na genge la uhalifu la kusafirisha nyara za serikali bila kibali cha Ofisi ya Wanyamapori.

Shitaka la pili linalowakabili watuhumiwa hao ni kusafirisha nyara za serikali ambazo ni vipande vya meno ya tembo kilo 3500 venye thamani ya Shilingi 4,202,275,000 walivyokuwa wakivisafirisha kutoka nchini hadi Hong Kong, China na Thailand bila ya kibali kutoka mamlaka husika kitendo ambacho kinyume na sheria.

Upande wa utetezi umedai kuwa, upelelezi haujakamillika. Watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote katika mashitka hayo kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo bila ya kibali cha Mwendesha Mashtaka (DPP). Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 10 Oktoba mwaka huu.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Kg 3500 yaaani tani 3.5, idadi ya meno mangapi? na hatimaye ni tembo wangapi? Nadhani huo utakua ni mtandao mkubwa sana
 
Ndugu tuma na picha kama hutojar
 
Hii biashara ni ngumu kuisha, wanunuaji wakuu wa pembe za Tembo ni wachina na wamejazana hapa Tz, serikali inatakiwa kuwa wanafatilia sana nyendo zao, la sivyo hao tembo wataisha tu.
Nilishaandika nyuma kwamba pembe za tembo liko kiimani zaidi China hasa wanaoamini dini ya Buddha, ili mtu akamilike kiimani lazima awe na mapambo yalichongwa kwa pembe za tembo,
Jamii ya Buddha inazaa Buddha kwa hiyo mtu akikua lazima anunue sanamu iliyochongwa kwa pembe za tembo
 
Tatizo ni pale ninapojua bei yake.
Kwamba ni 1.2ml/kg.

Pembe moja tu nina zaidi ya million 6.
 
Binadam mtu wa ajab sana. Waswekwe ndani bila huruma na wale mvua za kutosha
 
Back
Top Bottom