Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,498
- 9,279
Waandaaji wa tamasha la kila mwaka la Fiesta, Clouds Media Group wamelazimika kuwarudisha wasanii wote waliotolewa kwenye 'list' ya watakaotumbuiza baada ya muda kuonekana kuwa kikwazo.
Kurudishwa huko kumetokana na muda wa kumalizika kwa tamasha hilo kusogezwa hadi saa 11 alfajiri kwa kibali maalumu kutoka Serikalini.
Fiesta imekuwa ikifanyika kila mwaka na kuisha 'majogoo' lakini siku chache zilizopita Uongozi wa mkoa ulitoa kauli kuwa tamasha lolote linalofanyika baada ya saa 6 usiku linalazimika kufanyika kwenye klabu na si eneo la wazi.